Mambo yote yalianza pale baba yangu aliponilazimisha kuolewa na mwanamme ambaye hakuwa chaguo langu.
Mme huyu alikuwa mlevi kupindukia, hajithamini yeye na kunithamini huku kila siku akinipiga na kuna siku nikiwa na mimba alinipiga na nikaangukia tumbo sakafuni
Wakati huo nilikuwa na ujauzito wa miezi 8 na siku kadhaa na nilikuwa nimebakiza siku zisizopungua 15 ili nijifungue. Siku ya pili asubuhi baada ya kuyavumilia maumivu makali kwa usiku mzima nilienda nyumbani kwa mama na akanichukua mpaka hospitali ambako nililazwa huko mpaka itakapofika siku ya kujifungua.
Siku moja daktari alikuja asubuhi na kunifanyia uchunguzi na baadae akaniambia nimebakiza siku tatu ili nijifungue lakini nitatakiwa kufanyiwa upasuaji wa haraka ili niokoe maisha yangu kwani kwenye utumbo kuna tatizo limeonekana na linaweza kunipotezea uhai wangu.
Nikamuuliza kama mtoto atakuwa tumboni salama lakini daktari akaniambia kuna uwezekano mtoto atakuwa amekufa kwa hali ilivyo.
Nilifanyiwa upasuaji na mtoto alitolewa ingawa alikuwa dhaifu na hana nguvu akawekwa kwenye oxygen na kwa bahati nzuri akapona na kuwa mzima.
Nilitolewa kizazi kwa kuwa kulikuwa na tatizo lililosababishwa na kuanguka kule na nikaambiwa sitaweza kuzaa tena.
Sikurudi tena kwa mme wangu na kuamua kuanza maisha yangu nikimtunza mtoto wangu, nikampa elimu kwa kipato changu kidogo nilichokuwa nikipata mpaka akahitimu chuo kikuu miaka miwili iliyopita.
Mwa neema na mapenzi ya Mungu kijana wangu akapata kazi na kuwa msaada wa kutatua matatizo ya familia kwa kuutumia mshahara wake kwa matumizi yangu pale nyumbani ya yeye huko mjinii.
Tarehe 2 ya mwezi huu wa tatu akaniita niende mjini ambako alikuwa akifanya kazi ili anipe zawadi kwa ajili ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 ya mwezi huu wa tatu.
Siku ya tarehe 5 nikaenda nikiwa njiani nikawa nampigia simu lakini akawa hapatikani nikaenda mpaka nilipofika nyumbani na kuona mlango uko wazi nikakimbia kuingia ndani bila kuogopa ili kumsurprise mwanangu nakuiona zawadi lakini kwa mshangao nikaona mwanangu kalala chini ya zulia akiwa nusu ya kufa.
Pale nyumbani kila kitu kilikuwa kimeibiwa nikakimbia kutoka nje na kuwapigia polisi na kutafuta gari na kumpeleka hospitali ambako tangu kipindi hicho mpaka sasa amekuwa mahututi akisaidiwa kupumua kwa msaada wa mashine na hajafungua jicho.
Nimekuwa nikilia kila siku nikiwa pembeni ya kitanda chake na naamini siku akifa nami naweza kufa kwani ni kila kitu kwangu na tumaini langu kwa sasa na ndio mwanangu wa pekee na kamwe sitaweza kuja kuwa na mwanangu mwingine.
Naumia kwani badala ya kupokea zawadi sasa nimepokea majuto, kilio, huzuni na majonzi.
"Natambua kuna watu hivi sasa wana maumivu na majonzi yenye maumivu makubwa zaidi ya haya yangu, lakini naomba usilidharau hili kwani hata wewe hujui nini kipo mbele yako au kwa wale uwategemeeao"
....
Comment Kama umeguswa na habari hii ya kuhuzunisha inayonikumba mimi na mwanangu kwa wakati huu na hsare ili watu wengi wasome ujumbe huu
MWISHO
0 Maoni