MY STORY; JINSI ‘NILIVYOMBAKA’ MWANANGU WA MIKA ATISA!

Nilikua kwenye gari na wafanyakazi wenzangu, tulikua tunatoka Kibaha, ilikua usiku kwenye saa tano hivi ndipo nilipopigiwa simu kuwa mwanangu mdogo mtoto wa miaka 9 alikua kalazwa hospitalini. Nilipigiwa simu na binti wa kazi ambaye ndiyo alikua akinisaidia kulewa wanangu baada ya kuchana na mke wangu wa ndoa ya miaka 11. Alikua anaongea kama mtu aliyehanganyikiwa, akionyesha kuwa mwanangu alikua katika hali mbaya sana, sikumuelewa vizuri kwani nilianza kupaniki.
“Anaumwa nini? Hali yake ni mbaya?” Nilimuuliza mwanzo alisita kuniambia lakini baadaye aliniambia.
“Kimbia Baba, nimekupigia ili usirudi, kimbia! Anna (sio jina lake halisi) amebakwa, alikua anatoa damu nyingi sana!” Kwanza nilishruka, nilishaau kama aliniambia kimbia, lakini akili yangu ikaishia kwenye kubakwa.
“Kabakwa na nani? Hembu niambie, acha ujinga, niambie yuko hospitali gani, niambie!” Nilimuulizakwa hasira, alinitajia hospitali ambayo mwanangu alikua kalazwa niakata simu.
Niliwaambia w3afanyakazi wenzangu, kila mmoja alinipa pole, kila mmoja akiniambia lake, sikujua kilichotokea lakini niliapa kuwa huyo mwanaume ambaye almembaka binti yangu basi ningemuua. Tulibadilisha safari ambayo ilikua ni kumpeleka kila mmoja nyumbani kwake na kuhamia hospitali ya Temeke ambayo ndipo mwanangu alikuepo. Kila nikivuta picha mwanaume kumbaka mtoto wangu wa miaka 9 nilijihisi kupasuka.
Wenzangu walinisindikiza mpaka Hospitalini, njia nzima nilikua najilaumu mimi.
“Unajua niko bize sana, ni bora ningewaacha wakae na Mama yao, mwanangu akifa sijui nitafanya nini?” nilijiuliza, ndiyo kwanza nilikua nimetengana na mke wangu hata mwezi nilikua sijamaliza. Wakati namuacha mke wangu alikua ni mjamzito na sababu ya kuchana anaye kusema kweli nilikua nampiga sana, nilikua nampiga mpaka ikafikia hatua ndugu zake wakaamua kumchukua.
Nilimuambia kuwa kama anataka kuondoka basi aniachie watoto, aligoma kutokana na tabia zangu, nilihanagika ustawi wa jamaii na kwakua mimi nafanya kazi manisapaa inamaana watu wa ustawi wa jamii nilikua najuananao. Ingawa mimi ndiyo nilikua na makosa kwani nilikua mtu wa pombe na wanawake huku mke wangu akiongea naishia kumpiga lakini mimi niliambiwa kubaki na watoto.
Si kwamba nilitaka kuishi na wanangu, nawapenda wanangu kweli lakini sababu ya kuwataka wanangu nilijua kuwa mke wangu ananijua kuw3a mimi si mtu wa watoto, anajua kuwa naweza kuwadhuru wanangu hivyo nilijua kabisa kuwa nikimtishia mke wangu kuwa anichie watoto basi atabaki na hataondoka. Kwa miaka 11 ya ndoa yangu nilikua nampiga na kumdhalilisha ila kila wakati akitaka kuondoka basi nilimtisha watoto na alibaki.
Safari hii hakubaki, nilimpiga sana, kuna siku nilirudi nyumbani, nilikua na hasiara zangu za kazini, mwanamke niliyekua natembea naye ambaye nilikua nishamnunulia kiwanja na nilishaanza kumjengea alikua anatembea na mtu mkubwa sana, nilikasirika na kutaka kumpigalaklini aliniambia kuwa nikimgusa basi kazi sina na naenda jela kwani anajua madili yangu yote ya wizi. Kutokana na mtu aliyekua naye nilinywea.
Nilirudi nyumbani ili kuangalia mpira lakini kufika nikakuta kifurushi kimeisha, hapo ndiyo hasira zilinipanda nikaanza tu kumpiga mke wangu, nilimpiga sana mpaka watoto wakaingilia, lakini sikujali, mke wangu alizimia, nikaondoka nyumbani nikijua kuwa kafa lakini mwanangu Anna alimpigia Bibi yake na kumuambia kuwa aje amchukue Mama yake kwani Baba anataka kumuua.
Mara zote nilikua nampiga mke wangu, lakini hakuna mtu aliyekua anamuamini, mimi ni wale wanaume wapole, wanaume ambao wanajali watu wa nne, wanaume ambao kila mtu anawaona kama ni malaika.kila mara mke wanngu akilalamika kwa ndugu au wazazi wangu alionekana kuwa yeye dniyo mbaya, kila alipotaka kuondoka basi alionekana kuwa ana kisirani na alirudishwa ukichangia na mimi kudai watoto basi alibaki.
Lakini baada ya siku hiyo Anna kuwapigia ndugu zake na mke wangu walishtuka, wlaipokuja ndiyo Anna ambaye naye alikua anaona ninavyomnyanyasa Mama yake lakini hasemi kwa uoga aliamua kuongea, aliwamabioa kila kitu, kila mtu alishangaa lakini waliamini kwani mke wangu alilazwa hospitali wiki. Alipotoka niliomba msamaha lakini aligoma kubaki,a kasema anaondoka nilimuambia kuwa nabaki na wanangu lakini hakutaka kubaki tena.
Ndiyo tukafikishana ustawi wa jamii, alipooa nimepewa watoto alitaka kubaki lakini nilimfukuza, nili0na kama kanidhalilisha kunishitaki na nilitaka akae kwao kwanza ajifunze. Aliondoka nakuniacha na watoto tatu mmoja miaka 9, mwingine miaka mitano na mdogo miaka miwili. Wakati huo pia alikua na ujauzito wa miezi saba ambao kidogo utoke. Sikua na mdua wa kukaa na watoto, mdua wote nilikua bize kazini hivyo niliwaacha na binti wa kazi ambaye pia nilikua natembea naye.
Nilikua na mawazo mengi sana, nilienda mpaka kwenye wodi ambayo nilijua mwanangu yupo lakini ile nafika tu nilikamatwa, kulikua na askari mmoaj nnje kasimama nnje ya chumba kile. Nilikamatw ana simu zikapigwa nikashanaga anapelekwa mahabusu. Kwanza nilishangaa, nilianza kuuliza tatizo ni nini mbona nakamatwa wakati mwanangu kafanyiwa ukatili ndiyo nikaambiwa kuwa mwanangu alikua kabakwa, ana hali mbaya na hawajui kama atapona.
”Sasa ndiyo mnikamate?” Niliuliza kwa hasira kwani niliona kama wananipotezea mdua kumuona mwanangu.
“Ndiyo, wewe ndiyo mtuhumiwa wakwanza, kabla ya kupoteza fahau mwanao alikutaja wewe, alisme kabisa kuwa wewe dniyo umembaka na umekua ukimuingilia kimapenzi kwa muda mrefu.” Kwanza niliona kama utani, lakini nilipoanza kupigwa na kutukanwa na polisi ndiyo nilijua kuwa wapo siriasi.
Nilika mkatili sawa kwa mke wangu lakini hata siku moja nilikua siajawahi kuwapiga wanangu, mar azote nilijifanya Baba bora ingawa sikua bora namna hiyo. Nilikaa mahabusu kwa siku tatu, sikulala, sikuweza kufanya chochote, ndugu zangu wlaikuja na kunionea huruma lakini sikuwasikia,a kili yangu ilitaka tu mwanangu apone. Mwanangu alikua katika hali mbaya, alikua kapoteza damu nyingi na alikua anapumulia mashine.
Haikuingia akilini kwa rafiki zangu mimi kumbaka mwanangu wakati nilikua nao muda wote, walijaribu kuongea lakini ilishindikana, walionekana ni rafiki zangu na wananilidna, nilibaki mahabusu kuangalia kama mwanangu atapona au la. Kusema kweli nilikua nalai, nasali mwanangu apone nikimuambia Mungu kuwa nipo tayari kwenda jela lakini wmanangu apone, nilikua naumia sana kutokumuona mwanangu, nilipata uchungu sana nilishindwa kula, nilikua siwezi kufanya chochote.
Ndugu waliokua wanakuja kuniongelesha nilikua naona kama wananipotezea muda. Siku ya nne ndiyo mwanangu alipaata nafuu, aliweza kufumbua macho na kitu cha kwanza lichoulizia ni wadogo zake.
“Wameshaenda kwa Mama, sitaki Baba awaone, nataka mnipeleke na mimi kwa Mama!” Aliongea huku akilia, watu walimuambia kuwa wako salama na mimi siwezi kuwagusa ndipo alitulia, alitaka kumuona Mama yake, mke wangu alikua hospitalini pamoja na hali yake ya ujauzito lakini alikua pale na alitoka kidogo tu. Aliposikia anaitwa alienda mbuio, akamkumbatia mtoto ambaye alikua anamuomba kuwa asimuache.
“Mama tuondoke kabla Baba hajaaja, atatucnukua, Mama usituache tena, Baba atatuua!” Alipiga kelele huku akishuka kitandani, watu walimshika wakimhakikishia kuwa siwezi kumdhuru na siwezi kumchukua. Hapo ndipo alitulia, walitaka kuchukua maleezo ili kuongea kilichotokea lakini aligoma kuongea, walisema aachwe kwani yupo kwenye mshatuka, alipozinduka basi ndiyo nilipelekwa mahakamani na kushitakiwa kwa kosa la ubakaji.
Kesi yangu ilisomwatu na kuambiw auchunguzi bado unaendelea, nikarudishwa mahabusu, sikupewa dhamana. Kukaa jela hakukunisumbua bali ile hali ya kila mtu kuamini kuwa mimi naweza kumbaka mwanangu iliniumiza sana. Ndugu wlaigoma kuja kuniona, mtu pekee ambaye alikua anakuja ni binti wa kazi, hata Mama yangu mzazi alishindwa kuja kuniona, iliniuma sana kuona kuwa Mama yangua naweza kuamini kuwa naweza kumbaka mwahangu.
Nilikaa mahabusu miezi miwili ndipo siku moja tu askari mmoja alikuja na kuniambia kuwa naweza kuondoka. Nilishakata tamaa lakini nilitoka bila kujua nini kimetokea. Niliambiwa kuwa nipo huru kwani sikuhusika, kuna vijana wawili wa bodaboda ambao waliongea. Kumbe mwanangu alikua hataki kuishia na mimi, hivyo alijua kuwa kama akisema kuwa nimembaka basi mimi nitafungwa na kuozea jela huku yeye na wadogo zangu wakibaki na Mama yao.
Sijui alipata wapi hilo wazo lakini alitafuta Derava wa bodaboda ili atembee naye na arudi nyumbani kunisingizia mimi. Siku hiyo nilienda Site hivyo sikwenda kazini, mwanangu kuona gario yangu nyumbani alijua nipo nimelala, kwenye saa mbili hivi alimuita huyo dereva, akamuambia amuingilie na alimpa laki mbili ambazo ni pesa zangu alichukua chumbani kwangu alikua anaiba kidogo kidogo.
Kweli yule dereva alimuingilia, ilikua ni mara yake ya kwanza kufanya mapenzi na hakujua mapenzi ni nini, alipoanza kusikia maumivu alianza kupiga kelele lakini yule kija nahakuacha, alizidi kumuingilia kw anguvu mpaka kumchana sehemu za siri, damu zikawa zinamtoka na yote hayo yalifantika nyumbani kwangu, nyuma tu ya chumba changu.
Kelele zake hazikusikika nnje kwani kuna h=geti kubwa na ndani walikua wanaangalia TV, yule dereva alipoiona kazidiwa alikimbia, mwanangu alijaribu kukimbvia,a aktoka nnje akipiga kelele kuwa kabakwa ila hakusahau, pamoja na maumivu yote lakini alipiga kelele kuwa kabakwa na mimi Baba yake. Hapo nnje aliishiwa nguvu na kudondoka watu wakahdani kuwa nimembaka mwanangu na kukimbia, kwakua gari ilikua ndani wakajua kuwa kweli nilikuepo ndipo nikaanza kutafutwa na ndiyo sababu binti wa kazi kunipigia simu ili nikimbie.
Kusema kweli sikujua nawaumiza wanabgu kiasi hicho mpaka kufikia kuamua kubwakwa ili tu wakaishi na Mama yao. Yule dereva mpaka leo hajapatikana, kilichonisaidia nikwakua mwanangu aliwaomba madereva wanne wa bodaboda kabla ya kumpata aliyekubali. Niliumia sna aingawa si mimi nilifanya hicho kitendo ila mpaka sasa naamini kuwa mimi ndiyo nilimbaka mwanangu kwani kama si tabia zangu asingefanya hivyo.
Nilikua nampiga mke wangu kwakua nilikua sijiamini, mwanzo nilikua najua kuwa sina nguvu za kiume. Tangu nasoma sekondari siajwahi kufanya mapenzi na kwenda zaidi ya dakika tano wala zaidi ya raundi moja, hali hiyo imeniotesa maisha yangu yote. Nishakunywa madawa sana ila haikusaidia. Kila siku nilihisi mke wangu ananidharau, anataka kuniacha ndiyo maana nilikua nampiga.
Baada ya kuanza kukusoma mwaka jana na kusoma kitabu chako cha Mwanaume ndiyo nimejua kuwa siko peke yangu na sina tatizo kubwa nilipaswa tu kujiamini. Ni miaka mitano sasa, mwanangu yuko kidato cha kwanza lakini katika hiyo miaka mitano tulionana mara mbili tu, hataki kuniona. Mke wangu alishanisamehe tumerudiana, niliapa kutokumpiga mwanamke tena.
Natamani siku moja mwanangu mkubwa anisamehe, natamani aniite tena Baba, natamani asinione mnyama tena, anaishi kwa Bibi yake na hataki kabisa kuonana na mimi, hata likizio haji. Angalau hawa wadogo wakati namnyanyasa Mama yao walikua hawajawa na akili ila huyu ni wakike na ananiona kama mnyama. Kila nikisoma stori jinsi baadhi ya wanaume wanapiga wake zao najiona kama mimi nakumbuka maivu niliyomsababishia mwanangu nashindwa chakufanya. Kama hujiamini basi acha kushushia hasaira kwa mke wako, unapompiga mke wako humpigi mkeo tu bali unapiga familia.
MWISHO

Chapisha Maoni

0 Maoni