Nilipomaliza elimu yangu ya msingi sikuwa na muelekeo tena kwani mama alishindwa kunipeleka
sekondari kutokana na kipato chake duni. Nimelelewa na mama tu kwani baba alishakufa kitambo, ndugu wa baba hawakuwa na msaada wowote kwetu. Mimi ndio mtoto wa kwanza kwetu halafu nina wadogo zangu watatu. Nilipomaliza la saba nilikuwa nipo nyumbani huku nikizurula mitaani, vijana wajanja wakanilaghai kuwa wananipenda huku wakinipa pesa kidogo kunivutia. Kwa umri wangu ule sikujua anayenipenda kweli yukoje wala anayenitamani yukoje, kila aliyeniambia nakupenda nilijua ni kweli ananipenda kumbe wengine walikuwa wananitamani ila mimi sikujua lile, pia nilipenda sana kusifiwa ukizingatia kila aliyeniona alinisifia kuwa mimi ni mzuri sana hivyo kunifanya nijione ni wa pekee.
Kuna kijana mmoja akanilaghai hadi nikaanza mahusiano nae ya kingono, kama kawaida ya ngono majibu yakajipa nami nikawa mjamzito nikiwa na umri wa miaka kumi na tano ila yule kijana akaukataa ujauzito alionipa na kufanya niteseke sana ukizingatia maisha ya kwetu ni shida.
Mimba yangu ilipofikisha miezi tisa, akatokea kijana na kusema ananipenda sana. Akaniambia kuwa yupo tayari kunilea mimi na mtoto nitakayejifungua bila hata kujali kuwa si wa kwake, kwakweli nilifurahi sana kwani sikutegemea kitu cha namna ile.
Na kweli alinihudumia hadi siku za kujifungua kwangu, nilijifungua mtoto wa kiume kisha yule mwanaume akajitolea kuishi na mimi pamoja na mwanangu bila ya tatizo lolote na maisha yakaendelea kwa mtindo huo.
Kupita miezi mitatu nikapata ujauzito wa yule kijana kwahiyo nikawa nimembebea mimba yule mtoto wangu wa kwanza ila yule kijana alifurahi na kusema kuwa yote yale ni kheri tu.
Ikabidi kipindi kingine aje mama yangu kunisaidia kazi mbali mbali hadi pale nilipojifungua, mtoto alikuwa wa kiume tena kwahiyo nikawa na watoto wa kiume wawili.
Kwahiyo yule mwanangu wa kwanza alipofikisha mwaka alikuwa tayari kapata mdogo wake.
Mwanangu wa pili alipofikisha miezi minne, mume wangu akaniomba niende nae kwao kumsalimia mama yake ili aweze kumfahamu mtoto. Nami sikusita zaidi ya kufurahi tu.
Tulifunga safari na kwenda kwa wazazi wake huko kwenye mkoani.
Kufika kule akamtambulisha mama yake na kila kitu, baada ya wiki akasafiri na kuniacha pale na mama yake kumbe mama yake hakunipenda tena hakunipenda kabisa, hakutaka mimi niishi na mtoto wake kwahiyo akaanza kunifanyia visa vya kila aina bila ya kujali maumivu yangu na wala hakujali udogo wangu ukizingatia watoto wote hawa wawili nimejifungua kwa operesheni.
Kwakweli mambo ya mama mkwe yalinizidia ila kuna rafiki wa mume wangu alikuwa anakuja mara kwa mara kuniona nami nikamueleza kila kitu kuhusu mama mkwe wangu, kiukweli yule kijana alinihurumia sana na kusema kuwa yupo tayari kunisaidia kama nitahitaji msaada ila mimi niliamua kuvumilia pale kwa mama mkwe huku nikiamini kuwa mume wangu akirudi nitaondoka nae.
Mama mkwe akaanza kuniambia kuwa eti nilimpa mwanae madawa ili anipende, halafu akaniambia kuwa mwanae kapata mwanamke mwingine mjini kwahiyo hana mpango wowote tena na mimi ila niliendelea kuvumilia.
Baada ya miezi kadhaa mume wangu akarudi, nikafurahi sana na kumwambia turudi wote mjini ila mume wangu aliitwa na mama yake na kuambiwa maneno ya uongo kuhusu mimi.
Alipokuja tena chumbani alikuwa na hasira sana na kunitukana matusi ya kila aina, kisha akaondoka bila hata ya kuniaga.
Baada ya hapo, mama mkwe nae akanifukuza pale nyumbani, nikaondoka na watoto wangu wawili huku nalia ukizingatia wote wawili bado wadogo na wanahitaji kubebwa ikabidi nimbebe mmoja mgongoni na mwingine mbele.
Sikuwa na pa kukimbilia, ikabidi nimtafute yule rafiki wa mume wangu, ambaye hakusita bali alikuja na kunisaidia kisha nikaenda naye mjini kwenye nyumba yake.
Akaniahidi kunilea na watoto wangu.
Baada ya siku chache akanitongoza na kusema ananipenda sana na yupo tayari kwa chochote kwaajili yangu, kiukweli sikuwa na maamuzi sahihi ukizingatia umri wangu pamoja na mateso niliyokuwa nayo ikabidi nimkubali tu maana sikuwa na jinsi kwani yeye ndio tegemeo langu kwasasa.
Baada ya mwezi nikapata ujauzito wake, kiukweli sikupenda hali hii ila sikujua habari za uzazi wa mpango na ndiomana ikawa hivi kwangu.
Yule mwanaume aliendelea kunihudumia tu, hadi pale nilipojifungua.
Nilijifungua mtoto wa kiume tena, kwahiyo nikawa na watoto watatu ila baba tofauti.
Yule mwanaume akawa mume sasa na kunihudumia kwa kila kitu, mimi pamoja na wale watoto wangu watatu.
Miezi mitatu kupita tangu nijifungue huyu mtoto, alikuja mwanamke pale na watoto wawili kumbe yule mwanaume alikuwa ni mume wa mtu.
Yule mwanamke alichukizwa sana kuniona na kuanza kunifanyia visa vya kila aina, yule mwanaume alishindwa kuniamulia kutoka kwa mkewe hivyo akasafiri na kuniacha na sakata lile.
Yule mwanamke akanifukuza pale nyumbani kwake na kusema kuwa sina haki ya kuwa pale, niliondoka huku nalia na sikuwa na pa kwenda.
Njiani nilikutana tena na yule mwanaume ambaye nilijua ameshanikimbia tayari, akaniomba msamaha kwakuwa sikuwa na la kufanya na wale watoto watatu ikabidi nimsamehe tu.
Akanichukua na kunipeleka kwa rafiki yake pale mjini huku akiniambia kuwa niishi hapo kwa muda wakati yeye ananitafutia mahali pengine pa kuishi, nami nikakubali.
Toka siku aliyonikabidhi pale kwa rafiki yake hakuonekana tena.
Rafiki mtu naye akaanza kunishawishi kuwa niwe na mahusiano naye, nikakataa ndipo alipoanza kusitisha huduma kwangu na kwa watoto wangu hadi pale nilipoamua kumkubalia ndipo alipoanza kunihudumia tena kama kawaida.
Baada ya miezi michache nikapata ujauzito tena na kufanya nishindwe kuwalea vizuri wale watoto wangu watatu hivyo yule kaka akaamua kunisafirisha kwa kunikatia tiketi mimi na watoto zangu ili niweze kurudi nyumbani.
Kiukweli nilipata shida sana kwenye gari hadi nilipofika stendi na kupokelewa na mama.
Hali yangu haikuwa nzuri kwani mimba hii iliniendesha sana kupita maelezo ya kawaida.
Mama alinilea na kunihudumia, kipindi hiko yule kaka alikuwa ananitumia pesa ya matumizi hadi pale nilipojifungua.
Napo nilijifungua mtoto wa kiume, kwahiyo wakawa watoto wanne.
Baada ya miezi kadhaa yule kijana akasitisha huduma kwangu, sikujua nini tatizo ila aliacha kunitumia pesa za matumizi ghafla tu na kufanya maisha yangu yawe ya kubahatisha tena ukizingatia watoto wanne wanangoja kuhudumiwa na mimi.
Nilikuwa mdogo ila akili yangu ilivurugika kwakweli.
Wakati nahangaika huku na huku katika kutafuta riziki ya watoto nikakutana na kijana aliyenihurumia sana, ikanilazimu kumuelezea kila kilichonisibu na yeye alionyesha kusikitishwa sana.
Siku zikaenda, yule kijana akaanza kunifatilia akidai kuwa ananipenda na kuniambia kwamba yeye yupo tofauti na vijana wengine.
Mwanzoni nilimkataa ila baada ya kunishawishi sana, ukizingatia na shida niliyonayo nikamkubali.
Baada ya miezi kadhaa nikapata ujauzito wake, nilipomwambia alikataa kabisa na kuvunja mahusiano na mimi, kwakweli niliumia sana huku nikilia na ile mimba. Nikatamani hata kunywa sumu ile nife tu sema mama akanishauri na kufanya niachane na mawazo mabaya.
Wakati ile mimba ina miezi nane, alikuja yule mwanaume niliyeishi nae mwanzoni na kumwambia mama kuwa anataka kurudiana na mimi na kukiri makosa yake kwa niaba ya mama yake ila aliponiona na ule ujauzito mkubwa alishtuka sana nikamwambia asishtuke, kisha nikamtolea watoto niliokuwa nao, akaishia kushangaa kwani hata mtoto wake hakumtambua tena kuwa ni yupi, aliniuliza kuwa kwanini nimefanya vile? Nilimjibu kuwa ni maisha pamoja na yeye mwenyewe ndio vilivyonifanya hivi, aliniangalia tu bila ya kusema chochote na kuondoka.
Muda wa kujifungua ulipofika, nikajifungua mtoto wa kike.
Sikutaka tena kuwa na mwanaume, sikutaka kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi tena, kwakweli maisha yamenifunza kitu, mapenzi nayo yameniachia kovu.
Nina miaka 21 na watoto watano, sistahili kuwa hivi ila ndio nimeshakuwa tayari.
Kuwalea ndio kazi ngumu ila nitawalea tu, sitaki mume, mchumba, mpenzi wala rafiki wa kiume.
Ni mimi tu na watoto wangu basi.
Msinilaumu mimi ila lawama pelekeni kwenye maisha yangu na wanaume walaghai maana najua kuna watakao nilaumu sana kwa hili.
MWISHO

0 Maoni