DALILI SABA KUWA MKE WAKO (MAMA WA KAMBO) HUWANYANYASA WANAO!

Related image


Katika ulimwengu wa sasa suala la wanaume kupata watoto kabla ya ndoa limekua kama kitu cha kawaida sana, si ajabu kukuta kujana ambaye hajaoa ana watoto hata watatu kabla ya ndoa na wanawake tofauti tofauti. Lakini hata wale waliopo kwenye ndoa nao hali ndiyo hiyo hiyo, kuwa na watoto na wengi wao wakidaiwa matumizi huwachukua watoto wao ili kuwalea wenyewe.
Wanawake wengi siku hizi kulea watoto ambao si wao wameona kama ni kitu cha kawaida hivyo ule ujinga wa kumnyanyasa mtoto kwakua si wako wa kumzaa umepungua sana ingawa bado upo. Kwa wanaume wengi ni ngumu kugundua kuwa watoto wao huteseka hasa kutokana na ukweli kuwa wanawake wenye tabia za kutesa watoto wanajua kuigiza.
Wanajua kuwatishia watoto na hata kama ni kuwapiga basi hufanya hivyo Baba akiwa hayupo na kama ni kuwaumiza basi hufanya hivyo sehemu za siri na zilizojificha kama vile mgongoni na kwenye mapaja ambazo mara nyingi wababa wengi hawakagui. Sasa kama ni Baba basi hata kama unaona mambo yako vizuri hembu angalia dalili hizi kwani inawezekana mwanao anateseka kimya kimya na wewe hujui!
(1) Anapenda Kuwasifia Na Kujipendekeza Kwao Kila Ukiwepo; Ukiwa upo unakuta wanao wakambo husifiwa, anakuambia kuhusu shule, namna walivyofanya kitu flani vizuri, anajifanya kuwapenda na kusifia mambo mengine mengine ya ajabu. Utasikia flani siku hizi kawa hivi, muonyeshe Baba yako, jana tulienda sijui wapi umemuambia Baba yako.
Hata kama yeye ana watoto wake utakuta hawasifii sana kama wale wakambo, wakati mwingine hata hakuna umuhimu ni kama anajipendekeza. Hapo anajua kafanya makosa na anachotaka ni kujisafisha, kwa kufanya hivyo anafanya mambo mawili. Kwanza ni kama anawaambia watoto mimi na Baba yenu tuko vizuri hivyo hata mkimuambia haitasiadia.
Pili anakuambia wewe kuwa nawapenda na kuwajali wanao hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi. Ukiwepo hata wafanye kosa gani hawaadhibu zaidi ya kuwakemea kwa kucheka cheka lakini hata wewe ukitaka kuwakemea utasikia waache watoto na kitu ambacho mtoto wake akifanya anakasirika yule wa kambo anajifanya kukichukulia poa na utasikia “Ni mtoto muache”.
(2) Anapenda Kushitaki Makosa Yao Madogo Madogo; Pamoja na kupenda kusifia kama nilivyosema hapo juu lakini hawa watu ni wajanja. Hawaishii kusifia tu, mtoto anapokosea au kufanya kitu ambacho hata hakihitaji adhabu au wangemalizana wenyewe basi hamuadhibu na huja kushitaki kwako. Mara flani kafanya hivi, flani kafanya vile.
Hapa hataki kumuadhibu yeye bali anataka wewe utambue kuwa mwanao si malaika, anafanya makosa. Utakuta wanae wakifanya kitu kama hicho anawaadhibu yanaisha au hata siku moja hajawahi kukuambia kitu kuhusu wanae lakini kwako kila saa ni kusema kuwa flani kafanya hivi, flani kafanya kile mpaka inaboa. Huyu wa namna hii anaweza hata asiwe anawasifia hata mara moja.
(3) Anawakataza Watoto Kuwa Karibu Na Wewe; Utasikia muacheni Baba yenu kachoka, nendeni ndani mkamalizie homework, Baba anaongea na wageni, sijui nini na nini! Kama wewe ni mtu wa kusafiri au uko bize na kazi unapokua nyumbani basi hataki kabisa watoto wakusogelee, hataki uwaguse.
Mara kadhaa akikuona na mtoto atatafuta sababu ya kukutenganisha naye, hafanyi hivyo kwa watoto wake na wakati mwingine hata wakitaka kuongea atawakemea ili tu wasiongee. Mtoto anapokemewa naye hunyamaza kwa uoga na haendelei, unapotaka kutoka na mtoto yule ambaye si wake basi atamuambia na yule wake mfuatane hata kama hukutaka hivyo.
(4) Watoto Wanaomba Ruhusa Kutumia Vitu Vya Kawaida Kabisa; Unaona wanao huomba ruhusa kufanya vitu ambavyo kikawaida watoto hawaombi ruhusa, anamuomba Mama yake kuangalia TV, anaomba kuchukua Glasi, anaomba kunywa maziwa, anaomba kwenda chumbani, wakati mwingine anaomba hata kwenda kujisaidia au kunanyuka mezani.
Unaweza kudhani ni nidhamu, lakini hapana mtoto kama huyu ni muoga na kazoeshwa hivyo, kuna vitu haruhusiwi kugusa hivyo kashazoea hata kama alishaambiwa Baba yako akiwepo usiombe lakini anajisahau kwa uoga. Mama yeke sasa mtoto anapoomba utasikia anajishaua “Kwani ni lazima uombe…huyu naye si uende au si ufanye…” Ukiona hivyo basi jua kuna walakini chunguza.
(5) Watoto Wanamuogopa, Hawana Raha Mbele Yake; Anajaribu kujichekesha, anajaribu kuwa karibu nao, anajaribu kuwasifia, anajaribu kujifanya kawaida na kuwapa vizawadi zawadi lakini watoto hawana raha kabisa mbele yake. Kila wakimuona wanaacha kucheza, wanaacha kula, walikaa kwenye makochi wanashuka, walikua wanakula wanaacha, unawaona wanakua na nidhamu ya ajabu.
Hawawi watoto tena wanaanza kufanya mambo kama watu wazima, hata kuongea inakua ni shida, wanakua hawana raha kabisa. Wakipewa ruhusa kuondoka basi ni kama wanashangili, kila mara wakifanya kitu wanakua kama wanamuangalia yeye ili kujua kama kakasirika au la? Wanamuogopa Mama yao kuliko wanavyokuogopa wewe na hawafanyi kitu mpaka awaruhusu wakati mwingine hata wewe ukiwaruhusu.
(6) Watoto Wana Makovu Mengi/Wanakua Na Maumivu Ukiwashika; Unampakata mtoto, unamgusa sehemu analia maumivu, anamakovu mwilini ambayo hayaelezeki, mara nyingi ukimuuliza mtoto ananyamaza au kulia lakini Mama akiona umeyaona utasikia. Huyu naye kazidisha michezo, nishamuambia aache kupigana huko shuleni… na mambo kama hayo.
Kwama umemuona mtoto kaumia, unamuuliza kabla ya mtoto kujibu basi mkeo kashajibu na anatoa majibu ambayo hata hayaeleweki. Mtoto kwa uoga kabisa unaona anakubaliana na mke wako bila kupinga, hasemi kitu anatingsia tu kichwa kukubali kilichosemwa na Mama na kama akisema kitu unamuona kabisa analengwa lengwa na machozi.
(7) Mama yao mzazi/ndugu/jirani ameshalalamikia; Mara nyingi watoto hawa wanakua na ndugu ambaye humuamini kama Mama zao wapo basi huwaambia yanaowakuta, wanaweza pia kumuambia ndugu mwingine au hata Dada wa kazi. Ameshakuambia kuwa kuna mambo hayaendi sawa wakati mwingine ni jirani lakini kaambiwa na inawezekana kashakuambia.
Hembu kama ukiona dalili hizi na hata kama umeambiwa, kabla ya kuongea na mkeo, ukamuuliza fanya uchunguzi, angalia mwenyewe kwani ukishamambia tu tayari ashaandaa jibu la kukupa hivyo kama huna ushahidi utajikuta unamuamini. Hembu usimuambie kwanza fanya uchunguzi wako, kuwa Baba na acha kudanganyika na mapenzi anayokupa kwani makovu aliyonayo mwanao yatakauka lakini kamwe hayataondoka

Chapisha Maoni

0 Maoni