
Dada zangu, umekutana na mwanaume, ana miaka 27 kuendelea bado anaishi kwao, au amefanya kazi zaidi ya miaka mitano lakini bado anaishi kwao au kwenye nyumba ya ndugu yake gani huyo. Wewe umeanza kazi una miaka miwili au mitau, ushanunua kiwanja na unampango wa kuchukua mko[po ujenge, au unaishi kwako unajitegemea na una kila kitu ndani wakati yeye tofauti na TV hana kitu cha maana.
Sanasana ukimuuliza atakudanganya kuwa kuna sehemu na jenga! kama una mwanaume wa namna hiyo mdogo wangu, acha kiherehere cha kumuambia mambo yako, eti unamuambia mambo yako ya maendeleo, unatakakufanya mambo makubwa unamuomba ushauri au unataka mfanye wote! Hivi mwenyewe hujiongezi, mtu yeye bado anaishi kwao unaanza kumuomba ushauri wa mambo makubwa mambo ya watu wazima.
Yaani ni sawa na mtu si fundi ni wa mtaani tu hana hata baisekeli unaanza kumuomba ushauri was pea nzuri za RANGE ROVER moja kwa moja atakuona kama unamdharau. Iko hivi wanaume wa namna hiyo ambao wamefanya kazi muda mrefu na hawana kitu cha maana, wana kipato lakini labda walikua wanaona hakitoshi.
Wanakipato lakini walikua wanaona hakifai kujenga, hakitoshi kufungua Biashara kwa kifupi hawana akili za maendeleo, wanachukia! Narudia wanachukia! Niendelee kusema wanachukia! Wanachukia! Wanachukia wanawake wenye akili za maendeleo, yaani akiwa na mwanamke kama wewe anajiona kama takataka! Anawaza hivi mimi ni kiazi, yaani nalipwa milioni, nimefanya kazi mika 8 lakini sina hata kiwanja, haka kadada kanalipwa laki 5 na kamefanya miaka miwili kana kiwanja!
Mwanzo watafikiri umehongwa lakini ukikaa na kumpigia mahesabu ya watu wenye akili kama wewe atajiona kiazi. Atafanya mambo mawili, asipokushauri ujinga ukaacha kufanya mambo yako ya maendeleo ukamsikiliza yeye na hata atake mfanye pamoja ili atembelee nyota yako, anaweza kukupa mimba, au kajitambulisha kwenu kisha akakuacha tena kw adharau kama tikiti maji lililooza sokoni!
Ni nadara sana kukutana na mwanaume wa namna hii halafu akaona kuwa nimepata mwanamke mwenye akili akakomaa naye. wapo wachache hushtuka lakini wanaume wengi wa namna hii hawapendi kushinwa na wanawake. Hivyo acha kujitia kiherehere cha mke kumuonyesha mwanaume huyu namna ya kufanikiwa, kumuonyesha kiwanja chako, kumuonyesha nyumba yako na vitu vyako ukadhani labda atakupendea nyumba hapana, unamboa! Unamboa! Unamboa!
UFANYE NINI SASA? Anza mahusiano, msome mtu wako, kama itafikia kuambiana iwe mbeleni ukishaona kuwa anajiamini na mko vizuri, wakati mwingine ukimuona mbinafsi sana seme nyumba ya wazazi wangu mimi ndiyo nasimamia au usiseme kabisa kama haleweki na mmeingia kwenye ndoa!
0 Maoni