KAMA RAFIKI ZAKO WANAKUSHAURI HIVI KUHUSU MKEO NA KUKUSIFIA KWA OFA UNAZOWAPA JUA WASHAKUONA WEWE NI FALA!

Related image
Katika maisha kuna watu ambao hawawezi kujisimamia wenyewe, wanafanya mambo yao kwa kuangalia nitaonekanaje, kwao kusifiwa na kuonekana kama wana hela, wana akili na wanajua kutumia basi hujiona wamaana na kujiona kama ndiyo wanakua wanaume zaidi. Hapa nazungumzia wanaume zaidi ingwa hata kwa Dada zangu kuna watu wana hizi tabia. Kama una rafiki zako, labda unakunywa Pombe, lakini hunyi ila unapenda starehe.
Kila wakitaka kutoka nilazima wakutafute wewe na mara nyingi wanaishia kusema kuwa Pombe bila wewe hainogi kabisa, yaani hapa tukikukosa hakuna raha kabisa. Wanafanya kazi lakini kwakua wewe una mshahara mkubwa kidogo au hata mshahara ni sawa lakini unalipa wewe. Sasa ikitokea wana shida basi wanakutafuta wewe uchangie yaani kila tatizo ni wewe uwepo utoe hela ndiyo wafurahi, wanakusifia na wanaweza hata kukutafutia kamachepuko kakutoka nako na kukusifia.
Wewe ukiwa na shida wanakua hawana hela lakini wao wakiwa na shida watakuelekeza hata sehemu ya kukopa ili uwasiadie na hata kukuonyehsa namna ya kuzipata. Wao wanafanya mambo ya maendeleo kimya kimya hivyo mkitaka kuongelea mambo ya maendeleo hawasemi chochote kwani wanataka uendelee kuongea upuuzi na kufanya starehe, hawakuambii madili ya hela wanakuamba madili ya wanawake, viwanja vipya na starehe mpya.
Sasa kama wewe ni kijana, una marafiki kama hao na unafurahia kuwa nao basi jua wewe ni FALA, lakini sio kwamba wewe ni fala tu, hapana nikuwa hao watu unaowaita marafiki washakuona fala, mbulula, limbukeni na wanakuchora, hawakupendi na wala hawatamani hata kukaa meza moja na wewe lakini kwakua ni fala basi utalipa bili lazima wakuite. Tena kitu kingine nikua marafiki kama hawa siku wakiwa na mitoko ya madili ya maendeleo hawakuiti.
Lakini walivyo wajanja na mashetani nikuwa wanaweza kukaa kikao cha hela, wakaoangea madili wakishamaliza wanakupigia na kukuambia tuko sehemu flani njoo, ukifika ndiyo wanaanza kunywa. Kama ishakutoke hivi najua unasoma lakini nikukumbushe tu wewe ni fala na rafiki zako wanajua ni fala ndiyo maana wako hivyo. Sasa inawezekana umeoa, una mke mzuri ashagundua mume wangu ni fala limbukeni hejielewi.
Mke kajitahidi sana kukubadilisha, amekushawishi mmeanza mambo ya maendeleo. Ulivyo fala limbukeni ukienda kwa marafiki zako unaanza kuwaambia mke wangu kaniambia hivi, mke kasema hiki mke hataki ninywe Pombe. Kwakua wana akili wanakuambia “Utapangiwaje na mwanamke, hela zako kwanini akupangie, wewe mwanaume bwana utamsikilizaje, hawa wanawake ukiwasikiliza sana basi watakutawala”.
Ndugu yangu kama unatabia za kutoa toa na rafiki zako wanakuambia hivyo jua kuwa washajua kua wewe ni fala na sasa kuna mjanja anataka kukustua na watakosa mtu wakulipa bia kwani wao wanajenga na hawana hela za kupoteza. Rafiki zako hawa ni mashetani wanaweza kukusababisha hata uache mke na kukutafutia Malaya hapo baa ili ujihisi kidume, watakusifia kwa kuchepuka na unaweza hata kumaucha mkeo kwaajili yao.
Sasa rafiki kama hawa siku ukipata shida hutawaona kwani wanakujua wewe ni fala hivyo hawataki kua karibu na wewe, tumia tu hela zikiisha utaona namna watakavyokua bize na maisha yao. Nimalizie kua najua unasoma hapa, najua unajua tabia zako nikuambie hata kama ni mimi nilikua nakusifia ujinga jua nilikua nakuona FALA ndiyo maana nakusifia hivyo hao rafiki zako nao wanakuona fala endelea kulipa bili wakati wao wanajenga.
Najua kuna watu roho zinawasuta na wanatamani MAFALA WAO wasisome hapa, niwaambie tu msijali watu kama hawa hawajiamini ukiona kastuka endele akumsifia kwakua ni fala atasahau na ataendelea kujihisi kidume atalipa bili tu. Kama una tabia hizi endele kulipa bili endelea kununua chakula, endelea kulipia Malaya kwani ili maisha yaendelee mafala kama nyinyi mnahitajika ili wengine wajenge na bia zinyweke!
Nishamaliza najua utasoma kimya kimya ila jua wale unaowaita marafiki wanakuchora tu lakini wanajua wewe ni Fala TU! Watakutumia kwa muda mambo yakiwa mabaya watakukimbia. Lakini kwakua wewe ni fala hata baada ya kusoma hapa bado utaona kama nimeandika upuuzi kwakua badala ya kusoma na kuona nilichoandika utakachotoka nacho hapa ni neno “FALA” ulivyo fala utaona kama nimekutukana kwa kukuita fala lakini kumbe tu nimeongea kwa nguvu jina wanalokuita rafiki zako “FALA”
KAMA UNA UNA UJASIRI BASI #SHARE KUNA FALA MMOJA ANAWEZA KUSTUKA HUKO!

Chapisha Maoni

0 Maoni