Unapotaka kufanya jambo lako "fanya" kwa sababu ni jambo lako

Unapotaka kufanya jambo lako "fanya" kwa sababu ni jambo lako ..sio kila mtu anataka kujua unataka kufanya nini....
Wapo watu wanatamani kujifungia ndani ya nyumba zao leo... hii ni baada ya kuwambia mambo yao watu wengine bahati mbaya mambo yale hayakutokea kama walivyotarajia.. Unapowambia watu nimepata mchumba mwaka kesho naolewa ..ilo kwao aliwasumbui wenyewe wanachotaka kuona ni wewe umekuwa mke .. Hivyo akili yao itavyodaka maneno yako itataka matokeo. Matokeo yanavyoenda ndivyo sivyo unageuka kichekesho katika akili zao.
Kuna mambo binafsi na kuna mambo ambayo watu wengine wanatakiwa kujua.
Mambo binafsi ni yale mambo ambayo bado yako katika process...ambayo hayajakamilika.
Na mambo ambayo watu wanatakiwa kujua ni yale ambayo yamekamilika watu huona matokeo tu.
Jifunze kufanya mambo yako binafsi yawe ya kwako hasa yanapokuwa katika process... Sio umeambiwa unapendwa unakuja kuwambia watu napendwa sana na mwakani naolewa ... Hii mbaya sana ...mambo yako binafsi yanatakiwa kuwa mambo yako...hii itakufanya kuishi kwa amani ..maana wakati mwingine wewe ndio utafuta midomo ya watu kwa kuwaambia mambo yako binafsi.

https://www.facebook.com/allaboutrelationshipandlife/

Chapisha Maoni

0 Maoni