MWANAUME FAHAMU NJIA ZA KUMFANYA MWANAMKE ATABASAMU.

MWANAUME FAHAMU NJIA ZA KUMFANYA MWANAMKE ATABASAMU.
Baadhi ya wanaume ndani ya Ndoa hudhani kumfanya mwanamke atabasamu na kufurahi kuwa ni jambo gumu na kwamba inahitaji mambo makubwa, mtazamo ambao sio sahihi.
Kila mtu ana mahitaji mbalimbali ya kimwili, kiakili na kiroho. Kupitia matendo mbalimbali, mtu huyo hujaribu kupata mahitaji hayo ili aishi kwa furaha. Hivyo, kila mwenendo hasi unaouona hutokana na ombwe ambalo halijazibwa. Wanaume wanapaswa kulitafakari sana hili, iwe katika familia, wa ndoa, wa urafiki au wa kijamii.
Wanawake wanahitaji sana kuenziwa na kuwajali ili waweze kuhisi na kupata furaha. Ni kwa sababu leo tunakuletea nasaha na ushauri ambao wanaume wanatakiwa kuufuata ili kuwasaidia kupandikiza tabasamu katika nyuso za wake zao:
1. Ukiomba radhi pindi unapomkosea itapandisha hadhi yako machoni mwake, kwa sababu hiyo ni ishara kuwa unamheshimu na kwamba wewe ni mtu madhubuti na mkweli.
2. Muoneshe kwa kauli na vitendo hisia zako kwa juhudi anazozifanya. Mhamasishe na umuunge mkono. Unatakiwa kuwa mtu wa kwanza kumsaidia pindi anapohitajia msaada.
3. Akifanya jambo linalokukera au halijakufurahisha mbele ya watu, subiri mpaka mtakapokuwa peke yenu na umwambie kwa utulivu mkubwa juu ya kilichokukera na umweleze unachokitarajia kutoka kwa kwake katika mazingira mengine kama hayo.
4. Mtetee dhidi ya mtu yeyote anayeishusha hadhi yake na heshima yake, lakini bila kusababisha ugomvi kati yako na yule aliyemkosea.
Siku zote NAMNA unavyoliendea jambo ndio ufunguo wa moyo wa mwanamke. Ukweli kama kuna jambo ambalo unatakiwa kujifunza kuhusu wanawake basi jifunze NAMNA ya kuongea nao na NAMNA ya kuwafanya wawe na furaha.

Chapisha Maoni

0 Maoni