Kaka nilinunua Kitabu chako jana usiku na kusema kweli sikulala, nilikua nakisoma usiku mzima, si kwasababu napenda kusoma bali kwakua sikua na kitu cha kufanya. Mume wangu amerudi asubuhi kama kawaida yake na hatusemeshani, tunaishi kama mtu na mke mwenza, lakini baada ya kusoma Kitabu chako na kukirudia mara mbili nimegundua nilipokua nakosea, kuna mambo mengi ambayo mume wangu amekua akinifanyia na nimegundua alikua anataka kuuonyesha uanaume wake.
Nadhani mimi nilitekwa na ile hali ya kutaka kuwa mke mwema nikawa nataka mume wangu kufanya kila kitu ninachotaka mimi, sikujua kama ninakosea kwani nilidhani kwakua mambo ninayomsahauri ni mambo ya maendeleo basi anapaswa kuyafuata. Kaka nimefurahi nilipoongea na wewe asubuhi kwani hukunificha, uliniambia ingawa nina akili ninamshauri mume wangu vizuri lakini mimi si Mama yake hivyo niache kulazimishia mambo kwani nayeye ana akili.
Natamani na mimi siku moja nije nitoe ushuhuda wangu hapa kuwa ndoa yangu imekua na amani. Nashukuru kwamba nimegundua tatizo langu mapema na anaahidi kubadilika, naomba sana Kaka usinichoke wala kuniacha kwani ndio yangu bado changa na nina ujazito sitaki mwanangu alelewe katika mazingira haya. Nashukuru kwa Kitabu na anakuahidi kuwa ninabadilika kwani nimejua makosa yangu, sitakua nikimuendesha tena mume wangu.
NB; Kimuhemuhe cha ndoa na ile hali ya kutaka kuonekana wake bora, ile hali ya kutaka mambo ya maendeleo huharibu ndoa nyingi. Nijambo la kawaida kumsikia mwanamke akisema mume wangu hanisikilizi lakini ukiongea naye na kuchunguza kidogo utakuta alitakiwa kusema “Mume wangu hataki nimuendeshe endeshe!” Nilazima ujue kuongea na mume wako atakusikiliza lakini kama wewe ni mtu wa kulazimishia na kutaka afanye unachotaka wewe tu basi sahau
0 Maoni