Unakutana na mwanaume, katika ongeaongea anakuambia kuwa nilikua naishi na mwanamke na tulichana, anaweza kuwa alikua ni mke, anaweza kuwa alikua ni mchumba tu, unakuta labda walizaa naye au walikua hawana ndoa. Kwanza unatakiwa kujua kuwa, si lazima wewe kikupate kilichompata mwenzako, inawezekana tu yeye hawakuelewana basi au hakujua namna ya kuishi naye basi, hivyo usiwe na wasiwasi.
Lakini wakati nakutoa wasiwasi hembu nikukumbushe tu ili usiingie kichwa kichwa, sasa utajuaje kuwa mwanaume ndiyo alikua ni tatizo na si mwanamke basi angalia mambo haya. Kuna wanaume kweli wanaumizwa na wanawake, kuna wanaume wanateseka kwenye mahusiano mpaka kufikia kuondoka lakini mwanaume ambaye ana tabia hizi huyu hajaumizwa, kuna uwezekano mkubwa ni muongo hivyo ingia kwa tahadhari!
(1) Mwanaume anamlaumu mwanamke, anamuongelea mabaya kila wakati; Iko hivi kiuhalisia wanaume ambao wananyanyaswa na wanawake, wanaume ambao wanasalitiwa hawaongei, hii inatokana na ukweli kuwa wanaume tunaamini kuwa ni udhaifu kunyanyaswa na wanawake na ni kujidhalilisha kuongelea kuhusu manyanyaso. Hivyo wanaume waliokua wananyanyaswa kweli basi wanakua wagumu kuongea kuwa walikua wananyanyaswa.
Lakini kuna wale ambao wao ndiyo walikua vichomi, hawa ndiyo utasikia nilimfumania mke wangu, alikua Malaya, alikua machafu, alikua mchoyo, alikua hivi. Unakuta mtu kazaa na mwanamke lakini anavyomdhalilisha mbele yako basi unamuona kama mnyama, anamuongelea mwanamke mwenzako vibaya mbele yako kama vile hetani. Ukikutana na mwanaume wa namna hiyo basi jua asilimia 90 ya mambaya ya huyo mwanamke anayokuambia ni yake, yeye ndiyo alikua anafanya hayo mambo na si huyo mwanamke.
(2) Ndugu zake wanakushadadia na wanaonyesha kukupenda; Yaani unaingia tu ndugu zake wanaanza kumponda wifi yao wa zamani, mara alikua mchoyo, mara mchafu, mara mbinafsi, wanaongea mabaya yake mpaka basi. Hii hutokea sana kama mwanaume ana pesa, yaani wanajiweka karibu na wewe, na labda kama huyo mwanamke mwingine hajaachwa vizuri wanamtukana na kumdhalilisha mbele yako.
Hapa kuna mawili, kwanza nikwakua mwanaume wako alikua anamtangaza mwanamke vibaya kwa ndugu zake hivyo wanamchukia lakini pili ni kwakua labda mwanaume kwao ndiyo ana vihela hivyo pamoja na kujua utumbo wa Kaka yao lakini wanamtetea na kuwa wanafiki wanakua karibu yake. Pia inawezekana Kaka yao ana pesa ila walikua wanamuona kama wifi yao alikua anawawekea kauzibe na wanamchukia. Kua makini sana na ndugu wa namna hii kwani hata wewe itakuja kula kwako tu, watakuja kukuchukia!
(3) Maneno yake ni tofauti na matendo; Hapa utajionea mwenyewe, anaongea kuwa mwanamke wake alikua Malaya lakini hataki uguse simu yake, mwanamke wake alikua Malaya lakini unakuta ana hasira, ana wivu wa kijinga jinga, unakuta ni mtu mkorofi, anatishia kukupiga na wakati mwingine kukupiga kabisa. Kwamba anaongea kana kwamba ni mtu mwema, anamsingizia X wake kwa kila kosa lakini wewe ukiangalia unaona kabisa mbona kama yeye ndiyo ana matatizo.
Dada yangu sikuambii umuache, ni mtu wako lakini kama anaongea mengine ila anafanya mengine basi jua kuna uwezekano nawewe yatakushinda. Kuwa makini na wanaume wa namna hii, wewe ni mwanamke, unajua uchungu wa kuwa mwanamke kuliko mimi, hembu nikuulize, ukae na mwanaume miaka minne, akuzalishe watoto wawili kama X wake halafu umuache tu na kukimbilia kuchepuka au kuamua kuwa mchafu, mchoyo umuache huyo mwanaume hivi hivi tu?
Najua uanajua jibu, sikuamulii lakini chunguza sana, ukisikia mwanaume kamuacha mwanamke wake ambaye walikaa kwenye mahusiano miaka mitatu au waliishi pamoja acha kusikiliza sababu ambazo mwanaume anatoa, sababu ambazo ndugu zake wanatoa au marafiki zake. Chunguza mwenywe na tafuta sababu zako kwani hao wote kuna uwezekano mkubwa wakakudanganya. Najua una hamu sana ya ndoa ila ndoa haina maana kama unaingia kwenye ndoa unakaa miezi miwili anakuacha
0 Maoni