SABABU TANO KWANINI USIWE MTU WA KULALAMIKA LALAMIKA

A
(1) Inakera, kila saa mwenza wako kusikiliza unaongelea kitu kile kile, humpi hata nafasi ya kufanya mambo yake. Kila saa unaona kama unaonewa, kana kwamba wewe ni mtakatifu huufanyi kosa lolote, inaboa inaboa na inakera sana, wakati mwingine anavumilia tu na kunyamaza lakini inakera, hembu acha baadhi ya mambo yapite kama hayakuvunji mguu kwanini ulalamike kila siku.
(2) Inakufanya kuwa mtu wa kuona mabaya tu; Ndiyo unapokua unalalamika lalamika kila siku itafikia hatua kuwa huoni tena mazuri, kila kizuri akikifanya unaona kama kibaya. Kapika chakula kizuri hukioni unaona kachumbari ambayo imejaa limau, kakuletea zawadi nzuri ya gauni hulioni gauni unaona mfuko mbovu ulowekea gauni!
(3) Unamfanya mwenza wakoa jihisi hana thamani. Kwamba anaona sasa kwako hana thamani yoyote, hakuna anachokifanya na wakati mwingine anajiuliza kama kila kitu analalamika kweli nastahili kuwa na yeye huyu. Anajiona kuwa juhudi zake hazina maaaa hivyo ataacha hata kufanya mazuri kwani anajua hata akifanya hutayaona.
(4) Inachosha; Ndiyo kila saa unalalamika, kila anachokifanya unalalamika. Unamfanya anachoka, yaani anarudi nyumbani anakuona anachoka hata kufanya mambo ya maana. Amejaribu kufanya kitu kiwe kizuri unakosoa basi anachoka hata kukifanya, ndiyo unapolalamika sio kwamba unampa moyo afanye kitu vizuri zaidi bali unamkatisha tamaa kua hata akifanya vizuri hutaona.
(5) Anaacha kusikiliza; Ndiyo akili ya mwanadamu inajifunza kupambana na changamoto, mtu anapojaribu kukuridhisha kila siku lakini huridhiki akili yake humfundisha kudharau, kusahau na kuzoe akelele zako. Sasa badala ya kukufanyia kitu vibaya basi hatafanya kabisa.
Hapa unaanza kuona kuwa hakujali kumbe akili yake ishamuambia kua hata akijali hutashukuru. Hivyo hembu jifunze kuongea badala ya kulalamika, jifunze kuacha mambo mengine yapite na si kupoteza amani ya nyumba kwa kullamikia kila kitu.

Chapisha Maoni

0 Maoni