katika mahusiano, mimi naitumia na inanisaidia sana “Kama huna uwezo wa kumuacha mpenzi wako basi fanya juu chini usimfumanie!” Naomba nitumie maneno haya ili muelewe, kumfumania mpenzi wako, hasa mwanaume ni sawa na kumtoa mwanamke Bikra, narudia tena, kumfumania mpenzi wako ni kama kumtoa mwanamke bikra, ikishatoka imetoka, uaminifu ukishapote aumepotea.
Kama huna uwezo wa kumuacha, kama huna uwezo wa kumuambia “Chagua mimi au huyo mwingine!” basi usimfumania, usiguse simu yake, usisikilize maneno ya watu, usihack mawasiliano yake na furahia tu kwa ananipenda basi. Lakini ukimumania mara ya kwanza, ukamsamehe, ukamuambia ukirudia tena na kuacha, akarudia, ukamsamehe tena, akarudia na ukamsamehe mara ya tatu basi jua kuwa huyo mtu anazoea. Ataanza kuchepuka bila shida, badala ya wewe kufuatilia simu yake basi simu zake ndiyo zitakua zinakufuatilia.
Atakakua hajali tena kwani anajua kwa yule fala hata nikitembea na dada yake haniachi! Aniache aende wapi? Aisee utajipa mapresha bure! Halafu wadada wana hiki kitu ambacho naomba nisimung’unye maneno niseme ni cha kipuuzi. Unajua kabisa jamaa anachepuka, unajua kabisa kuwa hata nikimkuta anafanya mapenzi sebuleni siwezi kumuacha lakini unahangaika kutafuta uhsahidi ili tu uombwe msamaha!
Yaani kuna mtu kutwa kucha anahangaika na simu ya mpenzi wake, au utasikia anamuuliza kiri kama ni kweli nikusamehe, jamaa anakubalia nayeye anasamehe. Mwanaume akishajua kuwa wewe ni wa namna hiyo basi jua kuwa hawezi kuacha uzinzi. Mtu huna kazi, huna Biashara, badala ya kuwa bize kutafuta kazi au kufanya Biashara upo bize kumfumania, unafumania unarudi kwenu wiki mwanaume anaomba msamaha unamrudia kwakua kwenu nako washakuchoka, kila siku unakua mtu wa kuondoka na kurudi.
Yaani unakua kama mfanya Biashara kuzunguka na mabegi kwenda kwenu na kurudi kwa mume, kama unauza vitenge kila mwezi kwenda Congo kuchukua mzigo! Tafuta kazi ya kufanya zaidi ya hiyo kazi ya kumfumania! Mfano wewe unatafuta ushahidi wa nini wakati mwanamke wake kakupigia simu? Umeona picha kapiga kitandani na X wake, unaanza kuuliza eti ni kweli sasa nini hapo cha kuuliza?
Ukweli ni kwamba anachepuka, na ukweli mwingine nikuwa haachi kwakua ashakusoma kila siku unafumania unasamehe, hivyo kwanini uhangaike mpaka unaanza kupata magonjwa ya matajiri Mapresha wakati hata pesa ya kununulia chips kavu kuna! Kaa tulia tafuta pesa ukichoka unaenda kwako na si kwenda kumsumbua Mama yako ambaye naye anapambana na kelele za dingi yako! Au unafikiri dingi yako nayeye ana afadhali? Unafikiri mama yako alivyokua anakuambia ndoa ni uvumilivu alimaanisha anavumilia kula kuku!
Nadhani mmenielewa, kama huna mpango wa kumuacha acha kumfumania, akishazoea kufumaniwa utashangaa huna haja ya kujua passwed yake maana michepuko yake itakua inakutumia mapicha moja kwa moja. Mimi binafsi sihanagiki na simu yake, kama anachepuka achepuka kivyake, nikimfumania najua siwezi kumsamehe nitamuacha, sasa mambo ya kuanza kutafuta mpenzi mpya sasa hivi nani anataka? Mtu anachelewa kidogo unakua na wasiwasi unampigia mpaka bosi wake, rafiki zake wote halafu ukimfumania unasamehe kisa kakuambia sitarudia tena!
Najua sauti inatosha ila kuna ataendelea na kesho atanitafuta kuwa kamfumania ila mwanaume hajaomba msamaha!
0 Maoni