MIAKA 12 YA NDOA KWA MARA YA KWANZA SASA NINA FURAHA

Sijui kama unanikumbuka lakini mimi nakukumbuka na kamwe sitakusahau katika maisha yangu. Labda nikukumbushe kidogo kwani najua unapokea meseji za watu wengi wenye matatizo kama mimi hivyo ni ngumu kutukumbuka sote.
Mimi ni mama wa watoto wanne niliolewa miaka 12 iliyopita, lakini nilikuja kwako na tatizo langu kuwa mume wangu alikua ananinyayasa sana. Si kuninyanyasa kwa kunipiga, kuninyima chakula au kunitukana.
Hapana alikua ananinyanyasa kutokana na maumbile yangu. Kusema kweli kama unavyoona mimi nimezaliwa na sura nzuri lakini kwa mipango ya Mungu sikujaaliwa makalio.
Yaani imepigwa pasi haswaaa na kwakua kifuani nimejaaliwa kidogo basi mimi ni wale namba tisa. Mume wangu tulikutana nikiwa hivyo, alinipenda na kunioa. Sasa tatizo kaka lilikuabaada ya ndoa ambapo alianza kuninyanyasa.
Kila siku alikua akininyanyasa kuwa sivutii, nikivaa nguo mpya nikusema sipendezi, mara kadhaa akisema sijui hata kwanini alinioa wakati haenjoy chochote.
Alipenda kuwasifia marafiki zangu wenye makalio makubwa tena mbele yangu na nilipoongea basi hunicheka na kuniambia nina wivu wanini wakati kashanioa hata kama ni kwa kuibiwa lakini ndiyo hivyo nishamzalia.
Yaani sijui kwanini hata akiona mwanamke kwenye TV humsifia bila hata kujali hisia zangu. Niliteseka hivyo kwa miaka 12 yote ya ndoa ingawa nilishaanza kuzoea lakini nilikua naumia kila siku.
Nilijiona kama kinyago na mara nyingi nililazimika kumnyenyekea kwani niliona kama kanifanyia hisani kunioa, kusema kweli nilijichukia na isingekua watoto kuna mara kahda anilishawahi kuwaza kujiua.
Niliwaza kujiua mara nyingi kwakua sikuweza kuondoka, ingawa nafanya kazi na nina kipato changu lakini nilijiona mbaya sana hivyo nilijua hata nikimuacha nikikutana na mwanaume mwingine mambo yatakua hivihivi kwnai kuondoka kusingeongeza makalio yangu.
Maisha yangu yalibadilika siku nilipokutana na wewe, baada ya kukuelezea tatizo langu nakumbuka ulianza kuniuliza kama anfanya kazi nikakuambia nafanya bishara na nina kipato kizuri tu.
Baada ya maswali mengi kuna ujumbe ulinitumia ambao niliuchukua, mpaka sasa ninao na niliuprint kabisa kwani ndiyo ujumbe ambao ulibadilisha maisha yangu, ulimkomesha mume wangu na ulinipa furaha.
Naomba niunukuu neno hadi neno, nataka na wengine wausome kwani naamini kama umenipa furaha baada ya miaka 12 na naamini utawapa furaha wanawake wenzangu Usichoke maelezo yangu marefu lakini ninafuraha lazima niandike.
“Kwanza pole sana kwa hali uliyonayo, siwezi kusema ni kitu cha kawaida lakini kuna wanawake wengi tu ambao hupitia hali kama yako. Labda kwanza kabla ya kukuambia nini chakufanya labda ningekuambia ni kwanini baadhi ya wanaume hufanya hivyo.
Kimaumbile mwanaume ameumbwa ili kuwa juu ya mwanamke, kwamba kisaikolojia wanaume tunaamini hivvyo, lakini hata katika malezi watoto wakiume wanalelewa kuwa imara, wenye nguvu, wakufanya maamuzi na wajuaji kuliko wanawake.
Mwanaume anayejiamini analijua hilo hivyo hahitaji kumshusha mwanaume ili kujiona kama yuko juu kwani anajua tayari yuko juu. Lakini kuna wale wanaume ambao hawajiamini, inawezekana ni kwakua hawana vipato vikubwa.
Kwakua hawana ujuzi mkubwa kitandani, kwakua wanaona kuawa unawazidi, laba wanaona una akili zaidi yao, kipato zaidi yao au kitu kingine chochote. Lakini wengine hawajiamini, sio kwasababu yenu bali kwakua hata na marafiki zako.
Kwa mfano mwanaume akikuona una marafiki wazuri kuliko yeye, wenye pesa kuliko yeye, elimu kuliko yeye, basi hujiona mdogo, anaweza kudhani unamdharau au akahisi unaweza kumsaliti kwakua yeye hatoshi.
Lakini pia inawezekana unatoka katika familia tajiri, kwenu mna kila kitu hivyo kumfanya kutokujiamini. Pia wakati mwingine inawezekana hata hamna sababu yoyote ya maana ni kutokujiamini kwake tu hivyo anaogopaogopa hata kama hujamzidi chochote.
Wanaume wa namna hii ambao hawajiamini wanahamu sana ya kuwa juu ya mwanamke na hata kama wako juu bado hawajimaini. Kwa maana hiyo hufanya kila kitu ili kumfanya mwanamke kujisikia vibaya, humnyanyasa kiakili mpaka kumfanya ajihisi hana thamani.
Wataangalia udhaifu wako, inaweza kuwa ni akili yako, uwezo wako wa kufanya kazi au ikawa ni maumbile yako. Ukiona mwanaume, hasa mume wako anakunyanyasa na kukusimangia maumbile yako jua hajiamini katika kitu flani.
Inawezekana hakuridhishi kitandani, ana maumbile mdogo ya kiume, kipato chake ni kidogo, anaona una marafiki wenye pesa au mahandsome kuliko yeye, unawasifia majirani, una ndugu wenye hela, unaakili kuliko yeye, una kismet na watu kuliko yeye, unafanya vizuri kazini kuliko yeye au kama nilivyosema hata hakuna sbabau ya msingi.
Sasa unaweza kujua kwanini hajiamini na ukabaidlisha hicho kitu lakini mara nyingi ni ngumu kwa wanaume wa namna hii kubadilika hivyo unatakiwa kujifunza kuishi nao kwa furaha na kuwabadilisha.
Njia nzuri ya kumbadilisha mwnaaume wa namna hii ni kuonyesha kutokujali kile kitu anachokitumia kukuumizia. Kwa mfano eye anakuumizia makalio, haya ni mamumbile, si kitu ambcho umekigfanya, sio tabia kusema kuw autabadilisha.
Hapana ni maumbile ambayo Mungu kakupa hivyo unatakiw akujifurahia. Kwanz akupewa tu kalio hata la kukalia ni baraka kubwa, kuna watu wa ngapi ambao hawana hata hayo, hivyo mshukuru Mungu kwa hilo.
Kitu cha kwanz amabcho nataka ufanye leo ni wkenda kujiangalia kwenye kioo, vua nguo jiangalie kwenye kioo, zungukazunguka na muambie Mungu ahsante kw amakalio haya kwnai kuna wengine hawana hata makalio.
Jua kuwa huna kasoro bali namna ulivyo ndivyo ambavyo Mungu aliamua kukuumba, angetaka kukupa makalio angekupa lakini kaamua kukupa hayo yanatosha. Sasa ukishakubaliana na hivyo, ukaanz akujiangalia kw amtizamo chanya ukajipend asas atunageukia kw amumeo.
Acha kujali mananeo yake, anapoongea jua haongei kwakua wewe huna matako makubwa, kwnai hicho ni kitu ambcho kinajulikana kwamba anakuambia kila siku hivyo si kitu kipya kabsia.
Pia anajua kuwa huwezi kuyaotesha wala kujibadilisha, anaongea kwakua hajiamini hivyo anataka na wew eusijiamini, mpuuze na tabasamu. Usiishie hapo, muonyeshe kabis akuw ahujali, kwamba akisema basi tabasamua na cheka tu kama vile hujaumia hata kama moyo unachoma.
Usiishie hapo tu, hembu sasa nenda mbali kidogo, mfano mmeongozana naye, ukaona mwanamke anatako kubwa kabla ya kusubiri amsifie msifie wewe kwanza,. Mguse mumeo muambie umeona chombo kile, mambo yako yale cheki lile tako.
Sifia na cheka, utaona anavyonuna. Mnaangalia TV ukaona tako kubwa mstue kana kwmaba hajaona, sifia lile tako. Unawez aukachombeza na kusema “Mungu kweli fundi cheki kitu kile, mume wangu ukipewa lile si unamjengea kabisa”.
Kishac hake na tabasamu. Lakini usiishie hapo, hembu mko chumbani kama kuna kioo hembu jiangalie, angalia tako lako kisha cheka na sema “hii pasi hapa nahitaji skin tight za mahipsa maana hakuna namna hapa.
Mgeukie eti mume wnagu nikipiga na kigodoro hapa si mwake, utapenda au utavumilia hii pasi tu. atakasirika au atacheka, ataponda, kesho nunua jaribu kuivaa na muambie nimepga kiggodoro, kisha unaweza kuvua nakusema ulkua unajaribu ujinga sema bora ubaki na pasi yako.
Amua ahca kukasirika hata kama unaumia. Kumbuka lengo lake ni kukuona wewe unanyong’onyea, unajidharau na unaumiza kichwa juu yake. Usimpe hilo, usimruhusu kukushusha, kukunyanyasa na mambo ambayo huna uwezo wa kuyabadilisha
Kila anapojaribu kutumia udhaifu wakao has amuonekano wako kukufanya ujisikie vibaya basi hembu jifanye hujakasirika. Unaweza kwend ambali zaidi, mfano umekaa akapita msichana akamsifia, wewe nenda msalimie yule msichana.
Msifie muambie umependeza kisha muambie mume wako naye anasema umependeza, ndiyo chekeni na mfurahi na huyo msichana kisha rudi na jifanye kama hakuna kilichotokea. Nina uhakika ukifanya hivi, ukiacha kulia, ukiacha kulalamika na kutokuumia basi ataahca taratibu.
Hii ni sawa na kupiga ngumi ukuta ukidhani utaumia, utachoka mwenyewe na kuacha pale utakapooona unaumia wmenyewe. Ndivyo itakuw ahivyo kw amumeo, baad aya muda ataona anajiumiza tu mwenyewe.
Lakini anaweza kutafuta kingine, akatafuta udhaifu wako, akajaribu kukushusha kutokana nao, wala usijali tumia mbinu hiyohoyo kudili naye mwisho atajiona mjinga na kunyamaza, ataacha
Mwisho nimalizie kwa kusema kuwa huwajibiki kw amaumbile yako bali unawjaibika kwa tabia zako. Mtu anapokosoa maumbile yako hakukosoi wewe bali humkosoa Mungu ni sawa na mtu anayekosoa kwanini jua lisiwe la bluu au likawa jeusi, ni mambo ambayo hayakuhusu.”

Chapisha Maoni

0 Maoni