Moja ya malalamiko makubwa ambayo huwa nayapata ni kwa wanawake kuibiwa wanaume zao. Kimekua kama kitu cha kawaida kwani hata hao ambao wanalalamika kipindi cha usichana wao (au hata wakati wanalalamika) walikua wanafanya hivyo na hawakujali kama hao wanaume wameoa na kuna mwanamke mwingine ambaye wanamuumiza.
Lakini hiyo si mada yangu, mada yangu ni kwanyinyi mabinti ambao hujaolewa unatembea na mume wa mtu unaanza kumfanya kama wako. Kila siku mtaani unaonekana naye, unaonyesha dhahiri na watu wanajua. Najua unaona kama ni sifa na kwa namna flani unajihisi kama unapendwa kuliko mke wake au kuna namna unahisi kama unamkomoa mke wake!
Jamaa si ana hela, si anakuhonga, anakupa kila kitu unachokitaka na hata ana mdharau mke wake, lakini kuna wale ambao mnajiambia kuwa nimemuambia amheshimu mkewe, au wale ambao mkewe anakujua na ameamua kukubali tu kwani naye hataki kuachia ile nafasi, inawezekana anampenda sana au labda hana pakwenda na ana watoto hivyo anaamua kuvumilia pamoja na mashauzi yako.
Labda niwakumbushe tu kitu kimoja kua umri unaenda na mnapunguza uwezekano wa kuolewa. Iko hivi moja ya vitu ambavyo vijana wengi hawapendi ni mwanamke ambaye anatembea na mume wa mtu, unaweza kua Malaya sana na mwanaume asijali, lakini akishasikia umewekwa au ulishawekwa kinyumba na mume wa mtu.
Akasikia ulikua unapika na kupakua na mume wa mtu basi atakuogopa kama ukoma. Atakuchukua na kukuchezea tu lakini kuoa mwanamke ambaye anatembea na mume wa mtu, hapa sizungumzii wale ambao mnagongwa siku moja hujui hata jina lake, hujui hata kama kaoa au la, hapana!
Nazungumzia nyie ambao umemchukua mume wa mtu umemfanya kama wako, mpaka mtu ambaye hakujui basi anajua ni mume wako. Unaweza kuwa unadhani unamkomoa mkewe ila ni ujinga wa hali ya juu. Kwanini usiliwe kimyakimya kwanini uringie mume wa wakati bado una nafasi ya kupata wakwako!
Au unaona kwakua anakupa hela kuliko mkewe labda anakupenda kuliko mkewe, hapana anakupa pesa kwakua wewe anakununua na anajua kuwa uko kwake kimaslahi. Acha kujidanganya kua unapendwa, mtu akishakua mume wa mtu anajua tu uko kimaslahi. Kwamba hata kama humuombi pesa na unavumilia kama mke anajua wewe uko kimaslahi, anajua humpendi!
Kibaya hapa nikua mwisho wa siku ukishazeeka atarudi kwa mkewe, ataomba msamaha yataisha au kutafuta mchepuko mwingine, lakini wewe utabaki na sifa ile ile, “Huyu si ndiyo yule Dada alikua anatembe ana mume wa flani…” Baada ya muda hutapata mwanaume wa kukuoa na ukipata basi jua naye atakua kichomi.
Ningumu sana kwa mwanaume kumuoa mwanamke ambaye anajua fika kuwa yeye hutembea na waume za watu. Hii ni kwasababu wanaume tunaamini kuwa kama binti anatembea na kawekwa kinyumba na mume wa mtu basi yeye ni wakupenda pesa tu na hawezi kutulia na mwanaume mmoja. Sasa mwanamke kama huyu ni wa kugonga na kupita tu kwani si wakuoa.
Anajua akikuoa siku akiwa hana pesa basi unaweza kumuacha na kwenda kutafuta Mzee kwaajili ya kukuhudumia. Lakini pia wanaume huamini kuwa mwanamke anaweza kumchoka mwanaume lakini hawezi kuzichoka Pesa. Hapa nikimaanisha kuwa anajua kama una mzee wako basi hata ukiolewa hutaachana naye kwasababu anapesa.
Tunajua ukicheche kweli, tunajua unahongwa zaidi lakini hembu tulia iba kimyakimya kama wenzako, kutembea na mume wa mtu si ujanja ni kuonyesha tu kuwa huna bahati ya kijana wako ambaye anaweza kukuhudumia na kukupenda kweli. Hivyo wala si sifa ya kukufanya uanze kujitangaza na kujiona kama una bahati na unapendwa hapana umedoda hivyo doda kimya kimya!
0 Maoni