Wakati nawaza kuandika kitabu, akili yangu ilikua kutafuta mchapishaji, niliwasiliana na makampuni kadhaa, kuangalia bei zao na ubora ninaoutaka. Lakini pia nilikutana na changamoto ya usambazaji kuona ni namna gani nitaifikia nchi nzima.
Kusema kweli nilikata tamaa na kuona kuwa biashara ya vitabu hailipi. Lakini nilirudi nyuma na kujiuliza hivi ninachotaka hapa kuuza ni nini? Je nataka kuuza makaratasi ya vitabu au nataka kutoa elimu flani na kuwasaidia watu katika mahusiano yao? Jibu langu lilikua ni la pili, kuuza furaha, kuwasiadia watu.
Hivyo niliangalia ni kwa namna gani nitaweza kuuza furaha kulingana na uwezo wangu na niliona kuuza vitabu kwa njia ya ki electroinic ni njia bora zaidi ambapo mteja hupata ujumbe uleule tena kwa urahisi zaidi bila kumuongezea gharama za bure.
Sasa hali ni hiyo hiyo katika biashara nyingine, karibu kila mtu anayeniomba ushauri huniambia ana mtaji wa milioni moja afungue biashara gani? Kiuhalisia kwa mtu hasa aliyeko mjini, milioni moja inaweza kuishia kukodisha fremu na hata isikamilishe ukarabati na hivyo kuishia sifuri na kushindwa kufanya biashara, ukakata tamaa na kulala tu ndani.
Lakini katika makala zangu huko nyuma niliwahi kusema kuwa unapotaka kufanya biashara jiulize unata kuuza nini. Kwa mfano unataka kufanya biahara ya nguo, chakula, mbogamboga na vitu vingine. Tuende na mfano wetu wa biashara ya nguo, hapo unataka kuuza mavazi, kupendeza.
Sasa unatakiwa kujiuliza, nikipi cha muhimu zaidi, fremu au nguo zenyewe, kwamba je ukiwa na fremu utakua umeuza nguo au ukiwa na nguo. Kama ukiwaza hivyo basi unaweza kujikuta kwenye milioni moja, uanchukua laki mbili kwenda kununua nguo, ukaziweka chumbani kwako,ukapiga picha na kuziuza katika mitandao.
Lakini pia uanweza kuzizungusha kwa majirani, marafiki na hata maofisini. Lakini pia kama lengo lako ni kuwa na kibanda, kwa milioni moja unaweza kuchukua laki mbili tatu ukapata fremu, lakini badala ya kuchukua laki nane zilizobaki kwenda kukarabati na kupendezesha chumba ukazitumia katika kununua nguo ana kuweka katika chumba kile kile.
Hapo umeona utakua umefungua biashara kwa milioni moja huku mtaji mkubwa ukiutumia katika huduma unayoitaka. Lakini tuseme unatamani kufungua mgahawa, badala ya kutafuta chumba, ukawa unapikia nyumbani, unafunga chakula vizuri na unasambaza kwa majirani, maofisni ni na shemu nyingine.
Ukawamabia kabisa unafanya “Delivery Services”. Ndiyo unaweza kufanya chochote kama ukijua ni kipi kitu cha msingi katika biashara husika. Mimi nilitambua kitu cha msingi na sasa nimegundua kuwa kuuza kitabu kwa njia hii ni nzurui zaidi kwani mteja ambaye hajaridhika, ambaye hajalelewa nilichoandika anaweza kuniuliza.
Kwamba mteja angenunua kitabu mtaani na kisimsaidie, akaishia kulalamika kua kapoteza elfu kumi yake. Lakini kwakuuza mimi kwa njia ya mtandao nawasiliana nammtejea moja kwa moja, akiona hajaelewa sehemu basi huniuliza na mimi humuelewesha, kimegeuka kuwa darasa na si kitabu tena.
Wajue wateja wako wanataka nini na wauzie wanachotaka. Muhimu zaidi hakikisha unajua ni wapi pakuanzia, hata nyumba wengi wanaojenga nyumba huanza msingi wakiwa hawana hata hela ya tofali achilia mbali hela ya bati hawajui wataipata wapi na mwisho wa siku wanazipata kwani tayari walishaanza, anza sasa.
0 Maoni