HATUA YA KWANZA YA KUFANIKIWA KATIKA BIASHARA NA KUTENGENEZA WATEJA WA KUDUMU NI KUJUA UNAUZA NINI?

Nimekua nikiulizwa sana hili swali, hasa na akina Mama wa nyumbani ambao wanataka kuondoka katika kuwa tegemezi na wafanyakazi ambao wamechoka na kusubiria kukinga mishahara mwisho wa mwezi. Wengi wanauliza nifanye biashara gani ili inilipe?
Nikweli kila mtu anataka kufanikiwa, na kila mtu anataka kuwa na uhuru wa kikipato. Lakini changamoto kubwa ni mitaji, hasa mataji wa fedha, najua una mawazo mengi ya biashara, ukimuuliza kila mtu ni aina gani ya biashara ambayo anaona inafaa watakupa mlolongo mrefu wa biashara.
Hivyo ishu hapa si kujua ni aina gani ya biashara bali namna ya kuifanya hiyo biashara, lakini ili ufanikiwe katika biashara ni lazima ujue unauza nini? Kwa mfano mtu wa duka la nguo ukimuuliza atakuambia kua nauza nguo, lakini mimi nitakuambia hapana.
Kama unauza nguo upo katika biashara ya kupendezesha watu na siku ukilitambua hilo basi ni rahisi kufanikiwa. Mtu anayeuza nguo anasukumwa na pesa atafanya kila kitu ili kuhakikisha kua mteja ananunua hata kama ni kwa kumdanganya mteja.
Lakini mteja aliyedanganywa na kununua kitu basi hawezi kurudi tena hivyo ndiyo unaweza kua mwisho wa biashara yako. Ndiyo maana unaweza kuona sehemu kuna maduka mengi, lakini wateja wamepanga foleni katika duka moja huku maduka mengine yakiwa matupu.
Unaweza kufikiri ni uchawi lakini si kweli, namna ambavyo unawahudumia wateja wako ndiyo itamfanya mteja arudi. Mfano kama unauza nguo, mteja akaja ukambambikizia nguo, ukamdaganya amependeza na unamkaa vizuri, lakini katika kuvaa akoana haimkai vizuri umedanganya.
Mteja huyo utakua umemlia pesa yake lakini hata rudi tena kwakua anajua wewe ni muongo. Lakini kama mteja akaja, ukamuangalia na kumuambia hili shati nzuri lakini kutokana na rangi yako halitakufaa, chukua hili, au subiri niagizie nikienda nikuletee mashati ya aina yako.
Ukamuambia kabisa hili ni kali lakini bei yake ni kubwa kidogo, ukamuambia hili hapa ukivaa na suruali hii ndiyo itapendeza, ukamuangalia na kumshauri kitu kingine hata ambacho huna. Moja kwa moja huwi tu umemuuzia nguo lakini umekua stylst wake. Hivyo katika biashara yoyote nilazima ujue unauza nini?
Kama unauza nguo ujue unauza kupendeza, kama unauza chakula ujue huuzi tu kushiba bali unauza utamu mdomoni na afya nzuri. Hapo ndiyo utawakamata wateja. Najua kuna wateja ambao unaweza kuwapiga au kuwabambikia hasa wale wakupita, lakini hakikisha unakua na wateja wa kudumu.
Mfanye mteja arudi kwako kwani biashara nyingi mzunguko wake ni uleule, kwamba kutakua na wateja wapita njia kweli lakini kuna wale wa kila siku na ambao huelekezana. Hivi wewe siku moja hujawahi kumuelekeza mtu kwa mfano unamuambia ukienda Kariakoo kuna duka flani liko sehemu flani wanauza simu nzuri.
Yaani kana kwamba wanakakiwanda kumbe wala zimefanana na sehemu nyingine lakini nikwakua tu wanawajua wateja wao, namna ya kuongea nao na kuhakikisha kuwa hawanunui simu tu bali hununua mawasiliano mubashara. Nilazima ujue unauza nini, uwauzie wateja kutokana namahitaji yao na si kwakua unataka kutengeneza pesa.

Chapisha Maoni

0 Maoni