1) Kila kitu kipo kichwani kwako zaidi; Wakati mwingine unaweza kudhani kuwa una matatizo ya kimuonekano lakini ukweli nikuwa hayo mambo yapo kichwnai kwako. Wewe ni Mama ndiyo umetoka kujifungua hivyo kila mtu anatagemea kuwa nilazima utaongezeka, ni hali ya kawaida na zaidi ya wewe hakuna hata mtu anayekushangaa.
Hapa nikimaanisha kuwa, hakuna mtu anajali wewe kunenepa, mume wkao hajali hiyo michirizi, anajua kuna mtoto, anajua ni mabadiliko hivyo hajali. Yaani ni sawa na mtu ashangae mwanaume mtu mzima kuota ndevu, hawashangai na hawajali kwani ni kitu cha kawaida.
(2) Mume wako hajali; unaweza kuamini lakini asilimia 90 ya wanaume hawajali mabadiliko amayo hutokea katika miili ya wake zao baad aya kujifungua. Wengine hata hawjaui kama kuna mabaidliko, sanasana atasema mimba imekunenepesha lakini huanza kugundua pale unapowaambia.
Unapoanz akulalamika nimekua mnene, kulalamika dieti haifanyi kazi, kuanz akuchagua nguo za kuvaa, kuanza kuchagua sehemuz a kwenda hapo ndipo huanza kuwaza hivi kumbe kweli mke wangu kabadilika. Lakini huwaza huku wakijua kuw ani kitu cha kawiada
(3) Vaa nguo zinazokufanya uwe huru, unazozifurahia wewe; inawezekana kuna msukumo na presha kubwa ya kutaka kupendeza, unataka miezi kadhaa uanze kufiti katika nguo zako zazamani. Unataka kutoaka na unataka kwenda na wakati hivyo unajiangalia kwkaua hakuna nguo inakutosha.
Hembu nunu au vaa nguo ambazo zitakuweka huru na zinakupendeza wewe zaidi na si zile ambazo unadhani watuwa tazipenda. Unapovaa nguo, ikakufanya uwe huru, utulie basi nirahisi watu wengine kukuona una mvuto. Lakini ukijilazimishia katika nguo, viatu na vitu vingine, hutakua huru na hata huyo mumeo naye
(4) Muangalie mwanao; najua wakati mwingine ni vigumu kaucha kushaau kuhusu tgumbo, kuhusu miachirizi na mabadiliko ya mwili wkao, lakini kila unapokua na mawazo ya namna hiyo, hembu kabla ya kuanz akulia na kujilaumu.
Hembu kabla ya kuanza kumlaumu Mungu kwanini hataki kukufanya uwe kama zamani muangalie mwnaao. Jinsi alivyolala hapo vizuri, jinsi anavyokuangalia na vimacho vyake, namna ambavyo naakuhitaji na anavyocheka bila hata sababu.
Halafu shika tumbo lako, angalia michirizi na kujiuliza hivi ukiambiw auchague kati yake na hayo mabadiliko ungecghaga nini! ndiyo najua haitabdilisha muonekano lakini iyabadilisha namna unavyojiona na kuona kuwa kumbe ulichokifanya ni cha thamnai kubwa zaidi ya mabadiliko uliyoyapata, utajikuta unajipenda zadi
0 Maoni