Kama wewe ni binadamu naamini katika kipindi flani cha maisha yako ulishawahi kumchukia Mama yako, hata kama si kumchukia kwa kumchukia bali hata kumkasirikia, na kumsema vibaya huko kichwani kwako. Alikuambia kitu kikakukasirisha na wewe kwakua hukua na silaha yoyote basi ukamtukana huko kichwani. Hapa sisemi kwamba unamchukia Mama yako, hapana, lakini wakati wa utoto, wakati Mama akitimiza majukumu yake ya kukulea na kukunyoosha katika mstari basi ulimchukia ila sasa baada ya kuwa mtu mzima unampenda, unamshukuru na unaelewa kwanini alifanya vile.
Alikua na kawaida ya kukuambia, umekula, kwanini umefanya hivi, nimesema fanya kile, mbona hujafanya vizuri darasani, hiki chakula umepikaje, mbona hujapiga deki vizuri, kwanini umeacha rimoti kwenye kitanda, sitaki uongee na flani, sitaki uende sehemu flani, mwisho wa kurudi nyumbani ni saa flani. Hata kama Mama yako alikua poa kisi gani nina uhakika kwa asilimia mia moja kuna kitu ambacho alishawahi kukukataza na ukachukia, kama hajawahi basi huyo hakuwahi kuwa Mama yako. Ndiyo kazi yake ndiyo jukumu lake kuhakikisha kwamba unayooka na kua mtu bora baadaye.
Sasa kuna baadhi ya wanawake ambao hutaka kuwa Mama hata kwa waume zao, kwamba anataka kumpangia mume kila kitu, kumrekebisha kwa kila kitu, kumkatisha wakati anaongea, kumpangia vitu na kumuonya kila mara. Inawezekana mumeo ana matatizo mengi, usipoongea hafanyi kitu flani. Lakini unapaswa kujua kuwa huyo si mwanao ni mume wako hivyo mnapaswa kuongea badala ya wewe kumpangia. Acha kua rimoti yake na kutaka afanye mambo kama unavyotaka wewe. Hilo ni jukumu la Mama na si la mke, jukumu la mke ni kuwa rafiki yake.
Kwamba mnaongea, mnashauriana, mnabishana na kutofautiana, kwamba sio yeye afanye kila kitu kwa namna unavyotaka wewe. Hapana nilazima nayeye afanye kwa namna anavyotaka hata kama ile namna haikuvutii. Inawezekana unamuonyana unamuelekeza katika mambo mazuri, lakini kama ukizidisha, ukilazimisha na kununa kabisa kwamba hafanyi kama unavyotaka basi Dada yangu jua utampoteza. Kwanza kama nilivyosema kuwa kila mtu alishawahi kumchukia Mama yake.
Ataanza kukuchukia kwa kutaka kumuendesha, lakini kwa Mama yako ulikua ni utoto, ukakua na ukampenda, ila mumeo hana chakukua tena, akikuchukia kwa tabia yako ya kumuendesha basi kitakachofuata ni kukutandika makofi na kukufukuzia mbali kwani mwanaume yeye akichoka hakuna cha kusema vumilia. Naamini umenielewa, kama una hivyo vitabiatabia vya kutaka kumlazimishia Baba watoto kufanya unachotaka basi badilika. Lakini kama hujui namna ya kubadilika namna ya kuishi na mumeo basi hakikisha unapata kitabu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu”. Kuna matatizo mengi ya ndoa mbayo unaweza kuyakwepa kama utajia namna sahihi ya kuishi na mwenza wako.
0 Maoni