Ujinga ni pale unapopima uaminifu wa mpenzi wako kwa kumpigia video call

Ujinga ni pale unapopima uaminifu wa mpenzi wako kwa kumpigia video call wakati kila ukipiga anasema hembu Baby sogea pembeni huyu fala anapiga kuhakikisha kuwa sichepuki! Mnaongea usoni anakuchekea unadhani unamsisimua kumbe kuna mtu yuko miguuni! Jiamini ndugu yangu akitaka kuchepuka anachepuka tu huwezi kumchunga na video call haisaidii!
Kuna watu hata ukienda Sokoni wanataka Video call na wanaamini kabisa, ukishafikia hatua huyo kwamba bila video call hulali unahisi unaibiwa basi jua unakaribia kumpoteza huyo mtu. Kwanza anajua humuamini, pili anakuchoka haraka mpaka akikutana na mtu akamuambia ‘Mbona unakaa na mtu mshamba namna hiyo hajiamini…” basi ni rahisi kukuacha na video call zake.
Kama ni Video call piga kwakua unapenda kuona sura ya mwenza wako lakini si wkakua eti atashindwa kuchepuka. Mwingine ananuna kabisa kuwa hajapokea video call yangu atakua alikua anachepuka, jamani hivi kama unachepuka na mtu wa mtu, jamaa yake akapiga video call si mnamuangalia wote mnamchora, anakuambia sogea, kila akisogeza simu nawewe unasogoa, akikata mnamalizia mechi yenu kwa amani.
Najua kuna watu wamekasirika ila ukweli nikuwa, mwenza wako akijua kuwa unampenda sana huwezi kuishi bila yeye mpaka unapiga video call ili kujua kama anachepuka au la basi jua kuwa ushaanza kukuboa, anakuvuimilia tu kwakua hana namna, siku akipata namna atakuacha kwakua anaona kuwa hujiamini na umekua kero!
Image may contain: 1 person

Chapisha Maoni

0 Maoni