Ogopa sana watu ambao unakutana nao katika mitandao ambao kazi zao hazieleweki eleweki, hana kazi maalum ambayo inaweza kukufanya siku moja ukaenda ofisini kwao kuwatembelea, wanajifanya watu flani wa muhimu lbda usalama, sijui jeshini na wengine wengine ambao wana usiri flani, wanakupa ratiba ya kuwapigia simu, wanakua na safari safari nyingi za kikazi mara mikoani na mara nnje ya nchi.
Wakiwa huko wanajifanya kufanya kazi muhimu sana hata kuongea na wewe hawataki utasikia “Nitakupigia kwa namba nyingine kwani namba yangu inafuatiliwa!” Yaani wanakufanya ufikiri kuwa wao ni watu muhimu sana kiasi kwamba namba zao na mazungumzo yao yanafuatiliwa. Mtu yuko nnje ya nchi lakini akikupigia utakuta katumia namba ileile ambayo unaijua na hata kama ni mpya basi unakuta hakuna Code no ya hiyo nchi.
Labda kwa ambao hamjui nikuwa, code no ya Tanzania ni +255 kama mtu wako yuko nnje ya nchi basi hawezi kutumia namba ile iel kukupigia kwani ni lazima kuwe na Code no ya kule mfano Kenya ni +254, Rwanda +250 marekani +1 UK ni +44 na nyingine nyingi, hivyo ukiona anakupigia nnje ya nchi *(labda kama ni Whatsapp call) na hakuna Code ya huko nnje namba ni ile ile ya Tanzania basi huyo ndugu yangu ni tapeli.
Narudia dada zangu ukikuta mtu anajuka kwako kwenye mtandao anajifanya ana kazi muhimu flani amabyo haieleweki, unakuta ni mtu wa kusafiri safiiri sana anakufanya umuone bize na kazi yake au masomo kaisi kwamba anakupangia muda wa kuwasiliana naye basi ndugu yangu huyo ni TAPELI. Sasa najua dada zangu kama kawaida yenu mkishaahidwa ndoa na mwanaume akituma tuma vizawadi mnapagawa na kusema wakwangu tofauti, hembu endelea naye akishakutapeli nitafute nitumie kisa chako ili wengine wajifunze kwako kwani utakua ni shamba darasa kwa wengine.
0 Maoni