Tatizo kubwa la wanawake wanasubiri kupendwa ndiyo wawe na furaha, unakutana na binti mzuri, ana kazi nzuri, ana maisha mazuri lakini hana furaha kwakua tu hana mwanaume. Anajiona kama hana bahari, anajiona kama mtu mwenye laana, yaani anajiona kama ananuka flani kwakua tu hatongozwi, hana mwanaume. Yaani kwa kumuangalia tu anatia huruma.
Wanawake wana matazamio makubwa sana kuhusu wanaume, kwamba nikiolewa nitakua na furaha, nikiolewa nitafanya hiki na kile. Nsasa wanakua na mahuzuni yao kiasi kwamba wakiolewa wanataka wanaume wawape mafuraha ambayo hawkaua nayo. Mwanaume aache pombe kwakua hupendi, arudi saa mbili kwakua huwezi kukaa mwenyewe, akununulie zawadi kwakua hujinunulii?
Yaani unakuta mwanamke kaolewa, mwanaume anarudi saa nane usiku ukimuuliza kwanini hata hulali anakuambia kuwa siwezi kulala bila kujua kuwa mume wangu yuko wapi? dada yangu, mtu anarudi kalewa unataka kuuliza eti ulikua wapi, akuambie msikitini au kanisani alikua anaendesha misa ya usiku! Anarudi amebadilisha nguo bado unauliza, alilala wapi na eti hujalala kabisa!
Tatizo sio wanaume, tatizo mna visirani vyenu vya form II, mwanaume tushajua ni mshenzi anarudi saa nane asubuhi, sasa na wewe ambaye mpaka saa nane hulali ni nani? Najua si rahisi, najua unaumia lakini kama unadhani atabadilika kwakua akirudi anakukuta umenuna hujalala basi Dada yangu utang’atwa na mbu mpaka na mbu nao watakususa watachoka damu yako habadiliki.
Hembu lala, ukose mahaba na ukose usingizi! Ni lazima dada zangu mjue kuwa, furaha zenu ni wajibu wenu na si wajibu wa mume wako! Kama hujui namna ya kujipa furaha, kama bado una kisirani chako cha Darasa la tatu kinakusumbua,
0 Maoni