Nakuelewa sana Mama, lakini mimi sikutoa sadaka

Dada mmoja alifiwa na familia yake yote kwaajali ya gari, mumewe na watoto wawili, baada ya mazishi wiki mbili baadaye alienda kutoa sadaka ya shukurani. Kila mtu alishangaa ni kwanini alikua anamshukuru Mungu wakati alikua amepoteza kila kitu, maneno yalianz akusambaa kuwa labda yeye ndiyo kawaua kwasbabau ya kutafuta mali.
Ndugu wa mume nao walikasirika na katika kikao cha kugawana mali Mama mkwe alishindwa kuvumilia, alianz akumshutumu na kumuambia kuw ayeye ndiyo amemuua mtoto wake ndiyo maana alienda kutoa sadaka kushukuru kwa lile tukio. Huku akijikaza asitoe machozi yule Dada aliseama.
“Nakuelewa sana Mama, lakini mimi sikutoa sadaka kumshukuru Mungu kwa vifo vya wanangu na mume wnagu, hapana mimi nilikua namshukuru Mungu kwa miakja mitano ambayo amenipa ya kuishi na mwnaao na watoto wangu wawili. Mara nyingi tunapenda kwenda kwa Mungu pale tunapopata mambo mazuri kwakua tunajua kuwa ni yake.
Lakini tunasahau kuw ahata mitihani ambayo Mungu anatupa intake pia na tunapasw akuishukuru. Mimi mungu alinipa miaka mitano ya familia, kuna watu wanahangaika huko hawna awatoto, hawana vizazi, hawna andoa na wanatamani hata kupata dakika tano ttu ya furaha, nitakua mbinafsi kama sitamshukuru Mungu kwa kunipendelea mimi na kunipa miaka mitano.”

Chapisha Maoni

0 Maoni