
Nafundisha mpaka nachoka
Jamani, nasema hivi!.
, 👂👂👂
Kua na tabia ya kumkumbuka kumbuka mke/mpenzi wako kwa mambo madogo madogo. Kwa mwanake mapenzi ni vile vitu vidogo unavyomfanyia akiwa atagemei kama utamfanyia. Mpigie simu mchana muulize kama ameshakula na kala nini? Akikuambia bado hata kama unajua anapesa “Au nikutumie pesa ukanunue chips…” kisha tuma hata elfu kumi. Unajua kabisa lazima atapika lakini onyesha kuwa unajali. Amekuambia anaumwa ana dozi, unajua kuwa hajasahau lakini mpigie simu kumkumbusha kumeza dawa.
Alikua analalamika kuwa nywele zishaanza kuwasha, mpe pesa ya saluni, usisubiri akuombe ndiyo utoe. Kwanza nakushangaa kwanini usijichukulie maujiko kama unajali unasubiri mpaka ulazimishwe na kuitwa bahili. Kwa mfano mwanamke anapolalamika kuwa nywele zinawasha jua anataka pesa ya saluni. Sasa kuonyesha uanaume wako jichange mpe kabla hajakuomba, hapo ataona kama ni mapenzi tena mahaba. Lakini kama ukisubiri mpaka akakuomba pesa ya saluni hata ukitoa bila kubisha basi hayo yanakua majukumu.
Lakini ukitoa kwa kubisha na kulalamika basi wewe unakua kitasa! Sasa mwisho wa siku pesa ya saluni utatoa kwanini usiitoe kimahaba kabisa, kajikuna na kulalamika kidogo unampa kwakua ni majumuku yako yeye anachukulia ni mahaba. Unaona nguo za ndani zimeisha, unajua utaombwa na akikukomalia utaitoa tu hiyo pesa, kuwa mtu wa mahaba, angalia saizi nenda nunua hata tano au dazeni nzima mpelekee. Yaani akizivaa vipele vya viamtoka kwa msisimko namna anavyokuona unajua mahaba kumbe ulishamsoma kuwa anakaribia kukuomba ukatoa.
Nishamaliza sasa wewe endelea kujifanya mgumu kila kitu mpaka uambiwe wenzako watamlainisha
0 Maoni