Mwanadamu ameumbwa katika namna ya kuwa na haja. Hapa na maanisha kuwa, tunapika chakula kwasababu kuna haja ya kula, tuna vaa nguo kwaasababu kuna haja ya kujistiri, tunaoga kwababu kunahaja ya kuwa wasafi, na mambo mengine mengi ambayo mwanadamu huyafanya ni kwaajili ya haja fulani.
Hata kufanya kazi, hakuna mwanadamu ambaye anapenda kufanya kazi, hilo liko wazi, lakini kwasababu kwakufanya kazi anapata ujira ambao humtimizia haja zingine zote basi tunalazimika kufanyakazi. Kufanya kazi kunatokana na haja ya mahitaji yetu yote ya kila siku na si kwasababu ya utashi wa kimwili.
Hembu jiulize nini kitatokea kama kuna mtu wa kukutimiza haja zako zote. Huna majukumu yoyote na majukumu yako hutimizwa na mtu mwingine. Unakuwa huna haja ya kufanya kazi kwani kila kitu ambacho unakihitaji unakipata kutoka kwa mume wako. Kwakuwa umesoma na ulishaajiriwa basi unafanyakazi kama mazoea tu na si kwasababu ya kutimiza haja zako.
Ni jambo la kawaida kumsikia mwanamke akijisifia kuwa anafanya kazi tu lakini mumewe anamtimizia mahitaji yake yote na hana haja ya kugusa mshahara wake. Na ni rahisi kwa mwanamke aliyeko kwenye ndoa kuacha kazi pale anapokutana na magumu kidogo kuliko mwanaume hata kama wote wana vipato sawa na wanakumbana na magumu yaleyale.
Huu unaweza kuonekana ni ufahari lakini unamuondolea mwanamke ubunifu na ari ya kufanya kazi kwa bidii. Kwa mwanaume hana mtu wa kumtimizaia mahitaji yake, hakuna mtu wa kikidhi haja zake, anapaswa kukidhi haja zake mwenyewe pamoja na familia yake, hii humsukuma kuwa mbunifu kuhakikisha kuwa anakuwa na kipato cha ziada.
Wanaume hujaribu kila mbinu kuhakikisha kuwa wanatimiza mahitaji ya familia zao, wanawake hawana sababu ya kufanya hivyo hasa wanapokuwa na watu ambao tayari wapo kuwatimizia mahitaji yao. Hata kwa wale ambao hawajaolewa nirahisi kwa mwanamke kumuomba Baba yake au ndugu yeyote msaada kuliko mwanaume kufanya hivyo.
Amka, anza kufanya kitu hata kama ni kidogo namna gani, unaweza usijione kama unachangia kitu lakini kwakufanya hivyo akili yako unachangamka,
0 Maoni