Nimekaa kwenye ndoa kwa miaka saba bila kufanikiwa kupata mtoto. Katika kipindi chote hicho mimi pekee ndiyo nilikua nikihangaika na nilipokua nikimuambia mume wangu tuende Hospitali kupima alikua akikataa akiniambia kua yeye hana tatizo lolote. Kweli nilikua naumia sana kwani kila nikienda Hospitalini walikua wakiniambia sina tatizo.
Sasa sababu ya kuleta tatizo langu hapa nikuwa, kama miezi miwili hivi nilipata mwanaume (mchepuko), kusema kweli sijui kwanini lakini nilijikuta tu kwa tamaa ya mtoto na nikijua sina tatizo nilichepuka, nilishahisi mume wangu ana tatizo na ndiyo maana hataki kwenda Hospitalini.
Kweli baada ya kutoka na huyo mwanaume kwa mwezi mmoja tu nilipata ujauzito, kwangu ilikua ni furaha kwani nilijua kua nitamsingizia mume wangu ili na sisi tuwe na watoto hivyo hata huo mchepuko sijauambia kuwa nina mimba. Lakini kabla ya kumuambia mume wangu, siku moja alirudi nyumbani akiwa amelewa sana.
Si kawaida yake kwani hanywi pombe kabisa, nilimshangaa na sikutaka kuongea ila aliniambia kaamua kunywa kwani ana mazungumzo na mimi. Aliniambia alikunywa pombe ili kupata ujasiri wa kuniambia kuwa yeye hawezi kunipa ujauzito, alishaenda Hospitali kivyake kupima nakuambiwa ana matatizo mbegu zake hazina nguvu.
Aliniomba msamaha kwa kunificha lakini ni kitu ambacho kinamuumiza sana kila siku. Kusema kweli nimechanganyikiwa kwani hapa nina mimba na yeye kashasema kuwa ana matatizo sasa sijui nifanyeje, nimuambie mume wangu kuhusu mimba yangu, nikae kimya niitoe au niachane naye na kuendelea na masiha yangu nilee mwenyewe, nipo njia panda.

0 Maoni