Nilimuaga mume wangu kuwa naenda Kanisani, yeye si mtu wa ibada na kwakua mtoto alikua ni mdogo na anaumwa umwa niliona hamna shida kumuacha na binti wa kazi, niliamua kwenda misa ya kwanza ili kuwahi kurudi, mume wangu nilimuacha kalala kwani jana yake alichelewa sana kurudi, alikua kalewa sana ni kama alirudi alfajiri. Nilienda kanisani, misa ilipomalizika wakati tunatoka nilipigiwa simu kuwa Mama yangu mzazi anaumwa, hali yake ni mbaya hivyo nahitajika, walikua wanataka mtu wa kumuongezea damu.
Mimi na Mama ni Group moja na ilikua rahisi kwao kunitafuta mimi, nilichukua simu na kumpigia Mume wangu, lakini alikua hapokei, nilijua badi atakua kalala, nilimpigia binti wa kaza kumuulizia akaniambia kuwa Baba katoka asubuhi nilipoondoka tu, nilimuuliza kuhusu mtoto kaniambia ameshaamka anacheza nnje yuko vizuri, nilimshukuru Mungu kwani yeye ndiyo alikua nanipa wasiwasi, mwanangu alikua na mwaka mmoja na nusu na ukiona anacheza basi yuko vizuri.
“Baba akija muambie Bibi anaumwa, muambie anahitaji kuongezewa damu hivyo nimeenda.” Nilimuambia huku nikichukua simu yangu na kumtumia meseji mume wangu, nilimuaga na Dada wa kazi ili hata kama kwa bahati mbaya hatazisoma meseji zangu basi apate taarifa, kwa mume wangu kuondoka bila kuaga ilikua ni sababu kubwa ya kipigo, sikutaka kupigwa. Niliendelea kumpigia simu mume wangu lakini alipoona namsumbua basi aliizima. Nikaendea hospitalini kujitolea damu baada ya kuikamilisha kila kitu niliondoka.
Ingawa niliambiwa kupumzika lakini sikua na namna kwa muda niliokua nimekaa bila ruhusu ya mume wangu nilijua kuwa lazima atakasirika na mimi sikutaka kumkasirisha. Nilirudi nyumbani na kuikuta gari yake, nilijua yupo hivyo niliingia ndani, nilimkuta kakaa sebuleni anaangalia TV alikua tu kawaida lakini baada ya kuniona alibadilika na kuwa mbogo, kabla hata ya kusalimia nilianza.
“Mama anaendelea vizuri, ameshaongezewa damu…” Nilimuambia mapema ili ajue nilipokua, nilijua Dada ashamuambia lakini nilitaka asikie kutoka kwangu. kabla ya kujibu chochote nilisikia kitu kikinipiga juu ya jicho, ilikua ni romoti aliyokua kaishikilia mkononi, nikiwa nimeinama chini kwa maumivu nikisugua jicho langu nilisikia kitu kingine kikinipiga kichwani, nilikua ni jagi la maji la maji na kunipiga nalo kichwani, sikuzimia lakini nilipasuka kichwa, alikuja na kunipiga makofi na mateke mengi huku akiniambia kama namuona Mama yangu ndiyo muhimu basi niende huko huko.
“Mama anaendelea vizuri, ameshaongezewa damu…” Nilimuambia mapema ili ajue nilipokua, nilijua Dada ashamuambia lakini nilitaka asikie kutoka kwangu. kabla ya kujibu chochote nilisikia kitu kikinipiga juu ya jicho, ilikua ni romoti aliyokua kaishikilia mkononi, nikiwa nimeinama chini kwa maumivu nikisugua jicho langu nilisikia kitu kingine kikinipiga kichwani, nilikua ni jagi la maji la maji na kunipiga nalo kichwani, sikuzimia lakini nilipasuka kichwa, alikuja na kunipiga makofi na mateke mengi huku akiniambia kama namuona Mama yangu ndiyo muhimu basi niende huko huko.
Alimaliza na kuondoka, niliingia ndani na kujikanda, nilijifuta damu na kurudi jikoni kupika kwani yeye hali chakula cha dada wa kazi, nilipoka harahakahara lakini hakurudi mpaka asubuhi yake, alirudi akionyesha kuwa alikua na mwanamke kwani baada ya kuingia ndani nikiwa hapohapo chumbani alianza kuongea naye akikumbushia mambo ya jana, nilitaka kutoka lakini alinikataza, aliniambia sio heshima kutoka wakati anaongea na simu, nilibaki na nilijua kabisa alikua akifanya hivyo makusudi.
Aliongea na mwanamke wake mpaka akamaliza, sikusema chochote, alipomaliza alianza kunitukana, alisema kuwa simpendi akilalamika kuwa simuonei wivu. Alilalamika akisema yeye anchepuka ili kunifudnisha adamu, “Ungekua na akili ungejua kuwa mimi si Malaya, nachepuka ili ujue kuipenda ndoa yako, hata kama Mama yako anakufa unatakiwa kujua kuwa mimi ndiyo mume wako na wala hutakiwi kumjali Mama yako zaidi ya mimi, ona sasa unanipa dhambi za usaliti bure!”
Nilimsikiliza na kuishia kuomba msamaha ili tu mambo yaishe. “Nimekusamehe lakini usije kurudia tena!” Aliongea huku akicheka cheka, nilijilazimisha kucheka kwani nilikua najua fika kama nisingecheka basi ningekula kipigo kingine. Nilimuandalia chai akaenda kazini mimi nilienda kwenye mizunguko yangu kwani na mimi nafanya biashara.
Mchana kwenye saa tano hivi mume wangu alinipigia simu, aliniambia anakuja kunichukua kwani kaambiwa kuwa Mama yangu kafriki dunia. Kwa namna alivyokua anaongea ni kana kwamba kilikua kitu cha kawaida, nilijikuta nalia na kuanza kupiga kelele, nguvu ziliniishia, watu wlaikuja na kuniuliza nikawaambia nimefiwa na Mama yangu. Walitaka kunichukua kunipeleka nyumbani lakini niliwaambia hapana, mume wangu anakuja kunichukua, alishasema hivyo na nilijua kama nitaondoka bila yeye basi ingekua shida.
Kweli alikuja lakini aliniona kati kati ya watu wakinipepea, alinichukua bila kuwasalimia na kuniingiza kwenye gari. Kabla hata ya salamu alinipiga kofi moja la nguvu. “kwanini unanikatia simu, yaani mimi kwa wema wangu nakupigia simu na kuambia Mama yako kafariki unaanza kulia na kunikatia simu, kweli una akili kweli? Hivi mimi na Mama yako ambaye ashakufa nani ana umuhimu? Hivi unajua kuwa ukipata shida mimi ndiyo na hangaika na si huyo marehemu Mama yako?”
Nilikua katika huzuni, nilitamani kulia kutokana na uchungu wa kifo cha Mama yangu lakini nilishindwa, kwa kawaida mume wangu akinipiga hataki nilie kabisa, anataka nivumilie na nmisipige kelele, nilsihazoea hiyop hali tangu kipindi ni wachumba, ananiamiaga hasira zake hazitaki kelele za vilioa na mimi nilishazoea. Alinipeleka mpaka nyumbani, tukaingia chumbani, alianza kuvua nguo, nilijua kuwa anataka kubadilisha nguo ili twenda msibani aliniambia na mimi ni vue.
Nilimuuliza kwanini akaniambia ananihiaji kimwili. Kweli nilishindwa kuvumilia na kutaka kukataa, lakinia linifuata akanichania gauni langu, aliniambia mimi ni mke wake hivyo anaweza kunitumia wakati wowote ule. “Kwani usipofanya mapenzi ndiyo mama yako atafufuka!” Aliniambia, alinirusha kitandani na kunilazimisha kufanya mapenzi, wakati nafanya naye mapenzi alikua akinipiga makofi akinishutumu kuwa sionyeshi ushirikiano ni kama namdharau kuwa hanifikishi hivyo nitakua na mwanaume mwingine.
Nilijitahidi kumridhisha lakini nilishindwa, akili yangu ilikua kwa Mama tu, bila kupanga nilijikuta nasimama na kumuacha kbla yeye hajakojoa, huwezi amini alinikololea usoni na kuanza kunipiga haphapo kuwa nimemdhalilisha simtako. Mimi nilinyamaza, lakini kumbe wakti tunaingia mlangi ulikua wazi, mtoto wetu mdoogo wa mwaka na nusu alingia na kumuona Baba yake akinipiga, katoto kalinikimbilia na kunikumbatia, nilijikuta nakapakata ili angalau Baba yake kuniacha.
Kwakua nilikua na mtoto, lakini sikujua kuwa wakati mtoto nanikimbilia na mimi niko bize kumnyanyua mume wangu alishaokota pasi ambayo ilikua pale sebuleni. Aliinyanyua na kunirushia ili kunipiga, wakati huo nilikua ndiyo nanyanyuka, ile pasi ilimpiga mtoto kichwani, karibu na kisogo. Mtoto alipiga ukulele mmoja akanyamaza, nilijua tayari shakufa, nilimlaza kitandani na kumuangalia, alikua bado anapumua lakini nkichwani alikua anavimbavimba tu.
Mume wangu kuona vile alianza kupaniki, alivaa nguo harakaharaka na kuniambia kuwa mimi ndiyo nimemsababishia.
“Yaani unamtumia mtoto kama ngaao! nakupiga unaniwekea mtoto! Nakupiga unaniwekea mtoto!” Alipiga kelele huku akimchukua mtoto.
“Huyu mtoto akifa nakuua kwa mikono yangu, mshenzi mkubwa kabisa!” Nilivaa nguo nikataka kuongozana naye mpaka hospitalini lakinia likataa, aliniambia wewe si unampenda Mama yako basi nenda kamzike na usirudi tena mimi naenda kumuuguza mwanangu.
“Yaani unamtumia mtoto kama ngaao! nakupiga unaniwekea mtoto! Nakupiga unaniwekea mtoto!” Alipiga kelele huku akimchukua mtoto.
“Huyu mtoto akifa nakuua kwa mikono yangu, mshenzi mkubwa kabisa!” Nilivaa nguo nikataka kuongozana naye mpaka hospitalini lakinia likataa, aliniambia wewe si unampenda Mama yako basi nenda kamzike na usirudi tena mimi naenda kumuuguza mwanangu.
Aliondoka naye na sijui nini kilitokea, nilishindwa hata kwenda kwenye msiba wa Mama, alikaa huko mpaka jioni, ndugu walikua wananitafuta nilikua sipokei simu kwani nilishachanganyikiwa. Jioni alikuja na kuniambia kuwa mwanangu hali ni mbaya na niende huko kumuangalia, alinipeleka mpaka hospitalini ambapo kumbe alidanganya kuwa mtoto kadondoka kwenye ngazi. Nilikaa hospitalini kwa wiki mbili, hata mazishi ya Mama sikuhudhuria, mwanangu alikua ICU mpaka pale alipoaga dunia mwezi mmoja uliopita.
Baada ya mazishi ya mwanangu nilishindwa tena kuvumilia, sikuona thamani ya maisha, nilikunywa sumu mara mbili lakini naamini Mungu alitaka kuniadhibu kwani sikufa ingawa hata maziwa sikunywa. Mume wangu ameniacha ananiambia hawezi kushi na mimi kwani nimemuulia mtoto wake, ingawa hakuna mtu mwingine anajua kilichotokea lakini mpaka leo mume wangu ananilaumu kuwa mimi ndiyo nimemuua mtoto kwakumtumia kama ngao wakati ananipiga, nikweli nimemuua mwanangu na hilo linaniuma kila siku.
Najua na sihitaji yeye kuniambia ila najua nimemuua kwa kushindwa kuondoka mapema kipindi mume wangu ananinyanyasa. Nalia kila siku na kuna vitu vingi nikisoma katika ukurasa kwao natamani kurudisha siku nyuma niishi tofauti lakini siwezi. Kaka Iddi wewe ndiyo mtu wa kwanza kukuambia hiki kitu, sijali hata ukitaja jina langu kwani sioni kama maisha yanathamani tena, nimechoka, sioni hata haja ya kuishi ingawa bado najipa moyo kuwa ipo siku nitapona.
***MWISHO

0 Maoni