Mwanamke ni kituo cha wema na ni kiumbe chenye hisia kubwa sana. Kuwepo kwake hutegemea huruma na upendo. Huwa na shauku ya kupendwa na wengine na jinsi anavyopendwa zaidi ndivyo anavyofurahi zaidi. Hujitolea sana ili apendwe na wengi. Tabia hii ina nguvu sana ndani mwake hivyo kwamba akigundua kwamba hakuna mtu anaye mpenda, basi atajichukulia kuwa mtu duni na aliyeshindwa. Atakasirika na atahisi kuvunjika moyo. Kwa hiyo, kwa hakika ninaweza nikasema kwa dhati na kwa kinywa kipana kwamba siri ya mwanamume aliyefuzu katika maisha ya furaha ya ndoa ni jinsi anavyoonesha mapenzi kwa mke wake.
Kaka mpendwa! Mke wako kabla ya kuolewa na wewe, alikuwa anafaidi mapenzi ya wazazi wake na wema wa wazazi wake. Sasa ameingia kwenye mkataba wa ndoa na wewe na sasa amechagua kuishi na wewe katika maisha yake yote, anatarajia wewe umtimizie matakwa yake ya mapenzi na huba. Anatazamia wewe kuonyesha mapenzi zaidi kwake zaidi ya yale aliyokuwa anayapata kutoka kwa wazazi wake na marafiki zake. Amekuamini wewe sana na ndio sababu amekupa udhamini wa maisha yake.
Siri ya ndoa yenye furaha hutegemea jinsi unavyodhihirisha mapenzi yako kwa mkeo.
0 Maoni