Wanaume wengi wana mwanamke zaidi ya mmoja, tena wengine wanawapenda wote na wana wahudumia vizuri tu. Mwanaume anapomhudumia msichanamwanamke vizuri wakati mwingine humchanganya mwanamke.
Kamba mwanamke anaweza kufanyiwa mambo mengi akadhani anapendwa kuwa yeye ndiyo “Main Chick” kumbe yeye ndiyo mchepuko. Lakini wanaume wastaarabu hukuambia mapema kua hatakuoa.
Ingawa wanawake wengi hawaelewi kauli hizi lakini leo nikuambie kama mpenzi wako ameshakutolea hizi kauli, jua alikua anakuambia “Mimi sitakuoa hivyo jiongeze kama unata ndoa timua kabisa”
(1) Mimi Sio Mtu Wa Kuoa Kabisa; Mmekaa wawili, hata hujagusia suala la ndoa lakini unamsikia akisema kua hana mpango wa kuoa, hajioni akioa. Anasema yeye si muoaji, ndugu yangu jua kua amekuona ushaanza kujifanya mke wake anakupa tahadhari kua hana mpango wa kukuoa.
Hakuambii moja kwa moja kua sikuoi wewe, hapana anajilaumu yeye kwa tabia zake za kutotaka kuoa, anataka umuone kama yeye ndiyo ana matatizo hivyo usitegemee ndoa kutoka kwake. Hivyo wewe furahia kile anachokupa kwa wakati huo lakini usiwaze ndoa.
(2) Mwanaume Atakayekuoa Atafaidi Sana; Yeye ndiyo mpenzi wako ushampima kama mume wako, unamfanyia mambo mazuri badala ya kukusifia kua anatamani akuoe anaanza kumuonea wivu mwanaume atakayekuoa. Kwamba anajitoa kabisa kuhusu kukuoa, kwamba pamoja na tabia zako nzuri lakini hatakuoa hivyo anamuonea wivu atakayekuoa.
Kwa kauli hiyo anakuambia kua pamoja na kwamba anakupenda sana, anapenda unayoyafanya, anapenda tabia zako na kusema kweli anadhani wewe utakua mke bora lakini hujatosha bado kuwa mke wake. Ni njia ya kistaarabu ya kukuambia kua nenda kamtafute wa kumfanyia haya.
(3) Sidhani Kama Nitaweza Kukaa Na Mwanamke Nyumba Moja; Hii ni kauli nyingine ya kukukatisha tamaa, yuko na wewe na malengo ya kila mahusiano ni ndoa ila anasema yeye hawezi kuishi na mwanamke. Kana kwamba anataka kuishi na mwanaume, hapana hapo anakuambia wewe kua usijisikie vibaya akikuacha ni kwakua tu hawezi kuishi na mwanamke na si kwkaua hakutaki.
Sasa kama wewe ni mwanaume endelea kujibabysha ila kama ni mwanamke basi hizo ni dalili za kwamba uondoke au umuulize kua anamaanisha nini, akuambie kama anakupotezea muda tu au anakupenda kweli. Kwamba kama mko kitandani nyama kwa nyama wewe ni mwanamke na anasema kua hawezi kuishi na mwanamke inamaana anataka kukutumia tu lakini si kuishi na wewe!
(4) Ukiolewa Usisahau Kunipa Kadi; Nimpenzi wako mnapendana lakini wakati wewe ushavuta picha yeye ni mume wako anakuambia kauli kama hiyo. Wewe ushawaza na harusi yako, huko kichwani ushashona na gauni la harusi lakini yeye anakuwazia na mwanaume mwingine. Hii inamaanisha kua kichwani kwake anawaza mwanamke mwingine na si wewe.
Wewe unaweza kudhani ni utani wake lakini jua nikua anakuambia kua hana mpango wa kukuoa hivyo uanze kutafuta mwingine. Usikae tu kimya kimya muulize anamaanisha nini na anamipango hani na wewe? Tena kama ni kukujibu akujibu majibu ya kueleweka na sikujichekesha chekesha tu!
(5) Mwanamke Nitakaye Muoa; Anaanza sentensi zake na maneno hayo, kisha antoa sifa za mwanamke ambaye anatamani kumuoa na ukiangalia kwenye hizo sifa huna hata moja. Au kama unazo lakini ni chache tena zile ambazo si zamsingi kwake, zile ambazo hajazisisitizia.
Ndugu yangu kama ukisikia kauli hizo jua wewe sio huyo mwanamke hivyo unatakiwa kujiongeza. Kwanza ile hali tu ya kusema mwanamke nitakayemuoa bila kukutaja wewe, bila kuonyesha kusikia raha kua wewe ndiyo utakua mkewe basi jua kuna walakini na unapaswa kujiongeza.
Kwa kumalizia nikushauri tu kua hata kama mpenzi wako hutoa kauli hizi lakini haimaanishi kuwa umuache, wengine hawamaanishi sana au wanakua hawajajipanga na hawajui wanataka nini? Lakini kama kashaanza kuonyesha dalili hizi basi unachotakiwa kukifanya ni wewe kumuuliza kua ana maana gani na kauli zake?
Muambie akuambie mipango yake kuhusu wewe ili ujue mnaelekea wapi. Awe muwazi na kua makini na majibu yake, kwamba anakuambia alikua anatania lakini unaona kabida kuwa ana mchepuko mwingine na anaongea nao kwa uhuru tena mbele yako basi dada yangu, unadanganywa!
Kukaa kimya wakati ushaona dalili ni kujiandalia mazingira ya kuumizwa huko baadaye na hutakua na mtu tena wa kumlaumu kwani alishakuambia kua wewe sio mtu wake. Wanaume wengine wanakua wawazi kabisa wanakuambia kabisa kuwa mimi sitakuoa lakini wewe umejishikiliza ukidhani labda atabdilika, hapana alikua anamanisha.
0 Maoni