Kwa wanawake wengi walioolewa nadhani inawezekana ushakutana na kitu kama hiki. Mmeingia kwenye ndoa hata hamjamaliza mwaka ushaanza kuhisi mabadiliko tena makubwa sana.
Kuna mambo mengi ambayo mume wako alikua anakufanyia kipindi cha uchumba, alikufanyia mwanzo wa ndoa na sasa hayafanyi kabisa au hafanyi kwa ustadi uleule.
Yaani vitu kama kujibu sms zako, kukupigia simu, zawadi, kukusifia kutaka kutoka na kuongozana na wewe na mambo mengi mengi. Anakua kabadilika kabisa na yeye akirudi nyumbani ni chakula kuoga na mechi.
Mechi yenyewe haiwi tena kama ile ya zamnai, yaani ni ile papasapapasa tu, yaani ni kanyaga twende kama analima, hu enjoy tena mpaka unaanza kuwa na wasiwasi.
Hapa unakuwa na mashaka ya aina mbili, kwanza ni kuhsu wewe na pili ni kuhusu yeye. Kuhusu wewe unaanza kuwaza labda umebadilika, umenenepa, umekonda, umekuwa mbaya, hujijali na vikasorokasoro vingine vingi unajipa mpaka basi.
Unashindwa kujiamini na kujiona kama takataka, lakini kuna kuhusu yeye unaanza kuwaza labda ana mwingine, labda karudiana na X wake, unaanza kuangalia kwenye simu yake, unashinda kwenye kumchunguza.
Ndiyo unaanza kuwa na wasiwasi na ndoa yenu, uliyoyategemea kwenye ndoa hukuti tena hata moja. Nadhani ushawahi kuwaza hivyo, hii hali ishakukuta na kama hujaolewa ipo siku hali hii inaweza kukukuta.
Lakini nikuambie kitu, inawezekana hata hachepuki, wala wewe hujabadilika na inawezekana hata upendo haujapungua, bado anakupenda leo kama alivyokuwa akikupenda jana.
Sasa tatizo ni nini? Tatizo nikuwa mwanaume yeye anapooa basi anaona kama ashamaliza kila kitu. Yaani hana kitu kingine cha kuongeza, ameshaonyesha upendo wote.
Haoni tena sababu za kukununulia maua, haoni sababu za kukudekeza, haoni sababu za kukununulia kwa zawadi. Hii nikwakua mwanzoni alikua akikupa hivyo vitu ili akupate sasa ashakupata.
Lakini pia nikwakua anajua wewe ulikua unataka ndoa tu ili uamini unapendwa hivyo ameshakuoa na anaamini kuwa umeridhika na huhitaji kitu kingine.
Nikazi yako kama mke kumuambia kuwa unahitaji kitu kingine zaidi ya ndoa, kwamba yeye kukuoa na kukuweka ndani ndiyo mwanzo wa mapenzi hivyo anapaswa kufanya zaidi.
Kama umeshanunua kitabu changu basi naomba leo rudia sehemu ya pili, ndiyo ni sehemu muhimu, irudie na irudie tena. Hapo ndipo ndoa huanza na ndipo msisimko hutengenezwa.
Kwa wewe mwanaume isome sehemu hiyo vizuri kwani ni muhimu sana utaweza kumuelewa mke wako, kujua anataka nini, kujua kwanini analalamika kuwa uanchepuka kumbe wala huchepuki.
Nikwakua wewe unaona ushakamilisha ndoa kumbe bado, kuna vitu anavitaka hivyo kwa wale wanaume ambao nanyi mshanunua kitabu changu basi someni sehemu ya pili. Huu ndiyo mwanzo wa ndoa ukiharibu katika kipindi hicho jua unatengeneza ndoa ya mateso tu.
Narudia tena sikuandika kitabu ili nikuuzie kitabu kama makaratasi, niliandika ili nikuuzie furaha ya ndoa yako. Kuna vitu vidogo viodogo sana ambavyo vitaharibu ndoa yako, jifunze namna ya kuviepuka.

0 Maoni