Weka akiba pesa yako,weka akiba kwa chakula,weka akiba ya maneno yako,weka akiba ukipenda.
Tatizo ni kupenda kupitiliza,huna break.
Penda 70%,30% zinazobaki zikulinde ziwe za dharula lolote likitokea ujue pakukumbilia,pakujificha,kwa maana nafsi na moyo wako uwe na mipango mingine usigande mahali hapo hapo ili hali pana machafuko. ''Siwezi ishi bila yeye'' ''nitakwenda wapi'' ''watoto nitawalea na nani'' ''nitampata wapi kama yeye''.
Ni maneno ya mtu alifika sehemu hakuwaza kesho mambo yanaweza kubadilika,alijiweka mzima mzima bila kuweka akiba endapo kesho ikitokea sivyo awe na plan gani.
Upendo wa mtu anaujua mpendaji moyoni sio mpendwaji,Mimi siwezi jua Mwenzangu Moyoni ana upendo wa kiasi gani,ameniweka wa namna ipi kwake,amenikubali kiasi gani,so najua kwa nje ila kwa ndani anajua mwenyewe.
Mimi najijua mwenyewe nina Upendo kiwango gani kwake yeye anauona kwa nje tu.
Weka akiba usijitoe kupitiliza.
Sina maana uondoe upendo wako woote uliopo,hapana weka akiba kesho likitokea la kutokea usijutie maisha.
Hali ya kuumizana,kuuana,kurogana ni mtu alifika kwa mtu mzima mzima,linapotokea au aliyemuweka moyoni 100% anabadilika hana njia nyingine,anawaza ni bora apotee ampoteze mazima tukose woote.
Angeweka akiba angeanza kujiandaa kabla.
Akiba yake ingemsaidia kuwaza plan mpya,kwa maana maisha ni zaidi ya mapenzi,vipo vitu vya kufanya kupisha pito lako lipite.
Wewe ni yule yule ujapungukiwa na chochote,alichovutiwa yeye kipo atavutiwa na mwingine.
Utapendwa na mwingine na atakujali zaidi ya huyo aliyekwenda.
Daaaah,poleni sana mnaoumizwa na hii kitu Love.
Hongereni wanaoyafurahia hii kitu Love,Mungu azidi kuwaongezea upendo amani itawale maishani mwenu.
0 Maoni