SIO KILA MTU UNAWEZA KUISHI NAE.

Related image

Ni kama spear za magari,Engen ya Fuso halifungwi kwenye Noah,Taili la Scania haliendani na Taili la Corola.
Ni kama ladha za Matunda,utamu wa Embe haufanani na utamu wa Nanasi,Utamu wa Chungwa haufanani na utamu wa Pera,Utamu wa Tikiti Maji haufanani na utamu wa Apple.

Ndivyo ilivyo kwenye Mahusiano.
Kila mtu na mtu wake,,,''Kila shetani na mbuyu wake''
Maana yake,tunapishana maelewano,tunatofautiana picha,,,ile unaambiwa ''Mimi na Kimnana Picha haziendi,hazienzi kwa sababu hatuivi chungu kimoja,hatupatani.

Why?
Mapenzi yana barabara zake,yana mkondo wake,mkondo wa mapenzi haupindishwi kwa chochote,ni kama njia ya maji (Mfereji),hauzuiliki utapouziba utatafuta njia nyingine yatafika yanakotaka kwenda.

Mapenzi hayana Shotcut,sio kwa uganga sio pesa,hakunaga nikupende kwa pesa,hakuna mapenzi ya kudanganyana,je atakapoupata ukweli kuna nini,,?
Penzi likifuata njia zake hakuna kitu kitabomoa penzi lako,kwa sababu akikupenda anajikosoa,juzi niliandika,nampenda ananipenda,atajikosoa nitajikosoa,maisha yataenda mbali.

NJIA NI IPI.
Acha lizaliwe lenyewe.
Sio mimi sio wewe,nafsi,moyo unasema na nafsi zinasafiri mpaka kwa yule unaumiza kichwa,unakososa usingizi kwa ajili yake.
Unaumia moyoni,na yeye anakuvutia akikuona na anangoja tu ombi lako kumuhitaji.

Njia sahihi sio sex,sio pesa sio kutoka out.
Wengi wanaambiwa kama unanipenda nitumie picha yako ya utupu,mtandaoni,tusex,ninunulie 1,2,3.
Wengine wakitamkiwa wanapendwa matatizo yoote wanayakabidhi kwake,nadaiwa,vikoba,kusuka,njaa inauma,vocha.
Uliwezaje kuishi bila mimi leo kukutamkia nakupenda ni kero,,hapana sio njia sahihi.

NI WAZURI,WANAVUTIA,SAWA.
Sio wako,sio kila kizuri lazima ukimiliki,sio kila king'aacho ni dhahabu,ni mapambo tu ya Dunia,huendani nae ndio maana anakusumbua,acha yupo wa kufanana nae.
Leo kuna watu wanalia sana ninao wanakuja kulalamika,anasema ''kaka nampenda sana nifanyeje''
Sawa unampenda ndio kwa mateso

Anasema kila mara ni wa kulazimishwa tendo,anachepuka mpaka ndini kwake,anaondoka siku 3 kwa mchepuko na pesa ya matumizi aachi,
Akirudi akimuuliza kichapo,wakati mwingine aachi pesa ila akikuta chakula mboga asiyoipenda anasusa kula.

Chapisha Maoni

0 Maoni