
(1) Mume wako ameenda sehemu bila kukuaga, au si kawaida yake lakini kachelewa kurudi, alitoka na washikaji kachelewa. Anarudi nyumbani unamuuliza ulikua wapi anakuambia jibu, iwe uongo au kweli lakini unalikataa ushatengeneza majibu yako kichwani. Unanuna wiki nzima kisa mume hajakuag, kweli mume hajakuaga unamnunia wiki nzima, kwamba angekuaga ungepata faida gani?
Ungempa nauli au ungekua mzuri zaidi? Dada zangu mwanamke anatakiwa kumuaga mume wake kila wakati lakini si lazima mume kumuaga mke kila wakati. Tena wakati mwingine mwanaume fanya makusudi, yaani hata kama huna pakwenda ondoka tu nenda hata mochwari kakague maiti bila kumuaga. Dada zangu hivi ni vitu vya kijinga, akirudi muulize ila acha kununa kwani utaharibu ndoa yako bure.
(2) Umegombana na jirani, shoga yako, hamuongei, mume wako hajui au hata anajua umeshamuambia, lakini unaona ansalimiana na huyo jirani unanuna? Aisee, yaani mwanaume uingilie maugomvi ya wanawake ambao hujui wanagombania nini? Mimi naona ni upumbavu kwa mwanaume kuingilia ugomvi wa wanawake.
Kwanza ugomvi mwingine ni wa kijinga, wanaweza kuwa wanagombania kamjba ya kuanika nguo, ddodoki la kusugulia miguu labda mmmoja kachukua, ndoo ya maji sijui imepotea au wakati mwingine wanamgombania mpangaji mwingine kila mmoja anamtaka eti na wewe uingilie na kumnunia huyo jirani. Dada ukimnunia mume wako kwa kitu kama hiki ni upuuzi tu na unavunja ndoa yako.
(3) Mwanaume yuko online eti hajajibu meseji yako; Hili hata wanaume wanalol unamkuta mpenzi wako online, mtu kaingia kwasababu zake, ana mambo yake,a anchata na washikaji kuhusu hali ya Yanga wewe unaanza kutuma meseji, asipojibu unanuna eti upo online hunijibu. Dada angetaka kuchata na wewe angekuanza, pili kama hajajibu wakati mwingine hayupo kwenye mood ya kuchata na wewe.
Yaani sio kwavile wewe umeboreka huna mtu wa kuchata naye unilazimishe na mimi nichata na wewe. Iko hivi ukimtumia mtu meseji akiisoma asipojibi basi jua kuwa hayupo kwenye mood ya kuchat na wewe. Ana mambo yake mwenyewe, lakini kama akijibu kifupi basi jiongeze kuwa ana mambo yake, kununa eti hujachata na mimi ni ujinga, ushamba na kutokujiamini, na ukinuna kwakua nimeandika hivi ni ushamba zaidi.
(4) Kuna dada unamchukia, tena bila sababu, labda kwakua anatako kubwa kuliko wewe, umeshasikia kuwa ni Malaya huko mtaani ingawa hujawahi mkutam anapendwa na watu na ni mtu ambaye amezoeana na wanaume wanamchangamkia, au unamchukia tu kwakua tu unakisirani chako, unamuambia mume wako sitaki uongee na flani. Mume anakuambia sababu humuambii unataka asiongee naye, siku unakuta wanaongea basi unanuna wiki nzima, aisee unavunja ndoa yako, huwezi kuniambia nimnunie mtu ambaye hajanikosea kisa tu wewe unahisi kakuzidi kitu!
(5) Umetoka huko kwenu, umemkuta mume wako na marafiki zake, inawezekana kweli ni Malaya, walevi na wana kila aina ya tabia mbaya. Huzipendi, unaanza kumuambia mwanaume sitaki nikione na flani, yaani awanunie washikaji zake kisa tu unadhani kuwa watamuambukiza tabia mbaya. Dada yangu, utanuna, utapasuka.
Utavimba na kuvimbiwa lakini hawezi kuacha kuonge anao kisa wewe, tena jinsi unavyozidi kuongea ndiyo anaona unataka kumpanda kichwani. Rafiki zake hao wakikuona unawanunia watamuambia mbona shemeji ananuna, atawamabia, watamuambia mwanaume gani unapangiwa na mwanamke, atawasikiliza atakucha na mnuno wako hapo nyumbani ukipambana na nepi kwakua Pampas hanunui atawafuata wasioonuna kwa vitu kama hivyo.
(6) Kila kitu anachofanya mume wako unanuna kisha uansema kuwa utakua hunipendi; Hajakununulia nguo mpya kwakua hana pesa wewe ushasema ni kwakua hupendwi! Hajapokea simu yako kwakua alikua kwenye kikao wewe ushasema ni kwakua hupendwi! Hajakusindikiza kumuangalia Mama yako hospitalini kwakua alikua tu kalewa hata hana sababu wewe ushaanza ni kwakua hupendwi!
Aiosee wanawake wa namna hii wanaboa, yaani kila kitu ni kwakua hunipendi, kwakua hunipendi? Mtu anakuambia kwakua hunipendi mpaka unaanza kuwaza hivi inawezekana kweli, hivi huyu mwanamke nampendea nini kama kila siku kanuna kama kiporo cha senene!? Mwanaume unajikuta unaanza kuona kasoro za mke wako kwkaua tu analalamika, dada yangu hii inaboa kluna siku ataacha kukupenda kweli ndiyo utanyamaza.
(7) Unafuatilia ma X wa mwanaume wako kisha unakuja kumnunia; Wanaweza kuwa ni ma X, michepuko ambayo ishaachwa, mtu alishakukosea labda kakuomba msamaha yameisha au hata hakukukosea ni ma X kabisa, mwamaume alishawasahau, lakini wew eunatafuta namba zao, unawatafuta kwenye mitandao, unaangalia kila kitu kisha unanuna.
Unaruidi kwa mwanaume wako unaanza kulalamika kuwa wanakuwekea vijembe status, mpaka unajiuliza hizo statusi walikuwekea kwenye chakula au walikuletea nyumbani au ni kumbelembele chako kuwafuatilia. Yaani mimi umeenda huko kwenye mitandao unayachukua, umenuna unaniletea eiti nikuombe msamaha kwakua mchepuko wazamani au X wangu kakuwekea kijembe, dada umeyatafuta mwenyewe, nuna mwenyewe kama huwezi maisha mafupi rudi kwenu ukamnunia Baba yako hata yeye ni mwanaume tusichoshane!
(8) Nyie ambao mnasoma hapa badala ya kusoma vizuri mjifunze na kubadilika mnanuna eti mbona ametaja wanawake tu anawapendeela wanaume. Achene kushindana kwenye ndoa, ndoa si mashindano eti kwakua mume kafanya hivi na wewe ufanye aisee, kuna vitu vya kushindana lakini si hivi vya kipuuzi,a cha kununa bila sababu, jifunze na badilika, hivi vitu vinavunja ndoa nyingi kwakua vinaleta visirani na wanaume hawavumiliagi visirani.
0 Maoni