WANAUME TUNACHANGIA KUUA HISIA ZA WAKE ZETU.

Related image

Ni tatizo,ni shiida kubwa kuliko maelezo,tunapowasema wanawake tugeukie na huku.
Kwa sababu ukweli thamani ya ndoa ni heshima,utii,uaminivu,uvumilivu na msamaha.
Yoote yakikosekana upendo unapotea,hisia zinapotea hata uwajibikaji kwenye haki yenyewe ya ndoa ni Kama sheria tu si kwa furaha Wala ubunifu.

KWA NINI WANAUME.
Ulionyesha upendo kwake ukiwa kwenye kampeni,umempata Sasa unamuona si kitu,huna mahaba nae,
Mnaishi kwa machukizo,hata huduma muhimu kwa familia hutoi,Mama achome vitumbua,mihogo auze genge kisa family iishi,, baba upo Kama picha ya baba,ulimuolea Nini?
Tendo unalitaka kwa ubabe,ujui lugha ya kuhitaji tendo,umeua hisia zake kwa matendo yako mabaya,hata kumuandaa utaki ni tendo la lazima,saa zingine mkavu wala ushtuki ukimaliza huna habari nae.

Maandalizi ya mwanamke Ni process sio kitu cha kubahatisha,ila Ni rahisi Kama una urafiki nae saana sio maisha ya Kila siku "mshenzi" Malaya,mbwa n.k.
Ukimfurahisha mkeo kuanzia nje mpaka ndani,kwa upendo dhati,hata magonjwa ya pressure,hasira,viuno na migongo umemsaidia,kumpa furaha mkeo unaokoa vitu vingi kwake.

Tunaposema mwanamke Ni Kama chungu cha kupikia,Kama pasi ya umeme tuna maana hisia zake sio za kukurupuka,zinaingia taratibu sio Kama bulb kwa wanaume fasta inawaka na kuzima.
Wanaandaliwa nje na ndani,usitegemee kumfikisha ilihali mmeshinda vibaya.

Wanaume wanao wafikisha wake zao kila mechi hongereni,tujipongeze Sana kwa sababu tunaokoa wake zetu kuwaza nje.
Ila kwa wanaume mnaobaka wake zenu Mungu anawaona mnawatengenezea Hali mbaya ya magonjwa.
Ukiona mkeo ana matatizo hayo Anza kubadilika tibu kwa show ya ubunifu,usimvamie,mpandishe kileleni,utaweza ukiwa na urafiki nae sio uadui.

MWISHO
Tunasema course ndio ndoa yenyewe,usilazimishe kugusa kiungo cha mwanamke asipotaka kuguswa,usikalili kung'ang'ana denda ilihali hapendi,tafuta swich on yake,sio Kila mwanamke wa dk 5 ameandalika.

Chapisha Maoni

0 Maoni