TENDO LA NDOA BILA KILELE NI KUCHOSHANA

Image result for kujichua

(kwa ajili ya wanandoa tu na wapenzi na hii fanyia kazi Leo)
Kabla hujatamani kufanya tendo ni vyema tutambue umuhimu wa kufika kilele (mshindo)
Kwa wote wawili. (Me/ke)

Kufika kileleni au kufika mshindo kwa lugha ya kitabibu hujulikana kama orgasm na kwa lugha ya Kiingereza hujulikana kama ‘coming’ au ‘climaxing.’ Kwa mwanamke tendo hili humfanya aridhike na awe na amani moyoni mwake, Kwa mwanaume Tendo hili humpatia utulivu wa akili lakini humpa kujiamini zaidi kwa Mkewe/Mpenziwe.
Ni tukio ambalo linahusisha upitaji wa hatua kadhaa wa usisimuliwaji wa kimwili na kiakili.

Ni kawaida katika jamii kuwapo kwa malalamiko ya ndani kwa ndani kuhusiana na tukio zima la wenza wawili kutofika kileleni na kuridhika.
Tafiti zinaonyesha wanawake ndiyo wanapata zaidi tatizo hili kuliko wanaume. Na hii husababishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na yale ya kisaikolojia.
Kutokuandaliwa vyema, vinyongo na kutokuwa na hali ya msamaha kwa mwenza.Na mara nyingine husababishwa na Kuwa kwenye mahusiano na mtu ambae huna upendo wa kweli juu yake,...Mtu ambae uko kwake kwa sababu zako binafsi ambazo ni tofauti na upendo.
Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 10-15 ya wanawake duniani hawajawahi kufika kileleni.
Kufika kileleni ni msisimko wa kipekee unaoleta hisia nzuri kwa wenza wawili wanaowajibika kikamilifu katika tendo la ndoa. Hisia hizi hutokea kwa wenza wote kama ishara ya kufikia kilele cha tendo na kuridhika.

Hisia hizo huambatana na mtiririko wa matukio kadhaa yanayohusisha mfumo wa fahamu (ubongo na mishipa ya neva), damu na moyo, vichochezi na maeneo mengineyo ikiwamo viungo vya uzazi.

Wenza wanapofika kileleni mapigo ya moyo hubadilika, hudunda kwa haraka na huku upumuaji ukiwa ni wa kasi na kuvuta pumzi kwa nguvu.
Kwa wanawake hali hii huwa ni nzito na yakipekee, kufika kwao kileleni nakupata hisia nzuri huweza kuambatana na kujikunja ama kujikaza kwa misuli ya maeneo ya ukeni, nyumba ya uzazi na kiunoni.

Mwanamke anaweza kufika kileleni zaidi ya mara moja muda mfupi tu tangu alipofika kileleni mara ya kwanza na ataendelea kupata hisia hizo endapo ataendelea kusisimuliwa, hisia hizi hudumu kwa sekunde 40s

Chapisha Maoni

0 Maoni