
Wakati nakutana na huyu dada nilikua sina kitu, nilikua nimemaliza chuo sina ajira, yeye alikua kamaliza chuo pia na hana ajaira, lakini alikua na biahsara ya mitumba, tulipoanza mahusiano alinishawishi tuuze mitumba ile ya kurusha, tukawa tunanunua mabelo tunazunguka minadani tunarusha watu wanachukua.
Tulianza taratibu maisha yakawa mazuri, alipata ujauzito akaniambia kwakua yeye hawezi kuzunguka basi afungue biahsara ya vyomvo vya plastic ili auze na mimi nitafute kijana tuwe ttunazunguka. Alichukua milioni mbili na kufungua duka la vyombop, alianza taratibu ila baada ya kujifungua mtaji ulipanda mpaka ukafikia milioni 10, alipata dili la kuuza vyomvo vya mtumba, alianza taratibu, Biashara ikapanda akakutana na dada mmoja Zanzibar akawa ananunua mafriji ya mtumba, alizungusha mpaka kafikisha mtaji wa milioni 50.
Akaniambia niachane na mitumba tufungue uka jingine, tukafungua kweli na Biashara ilikua nzuri, nilianza kukamata pesa, ndugu zangu nao wakaingilia kati, ikaja ishu ya ndoa, kila nikitaka kufunga naye ndoa ndugu zangu wakawa wananiambia kuwa nisifunge naye ndoa kwani ana kakili kuliko mimi atachukua mali zote. Nilitafuta mwanamke mwingine na kwenda kufunga naye ndoa kimya kimya.
Wakati huo alikua na ujauzito wa miezi miwili wa mtoto wetu wapili, kuna kiwanja tulikua tumenunua tunamalizia kujenga na kilikua na jina langu na tulishanunua gari. Alipojua kuwa nimeoa mwanamke mwingine alitaka kuondoka, nilimuambia kama anaondoka basi nachukua kila kitu, nilitaka kubaki naye kama mke wa pili lakini aligoma. Nilipoona kuwa hataki kunisikiliza basi nilimfukuza, nikachukau Biashara zote na kuchukua kila kitu.
Kwakua duka lilikua na jina lake basi aligoma kuliachia, ndiyo duka lilikua na pesa nyingi, niliongea na Mama yangu ambaye alinitafutia mtaalamu, yule dada alianza kuumwa mguu, aliumwa sana mpaka ikafikia hatua ya kutaka kukatwa mguu, ndipo watu walimuambia kuwa sababu ni mimi, aniachie hizo mali, kweli aliahca kila kitu kikawa kama changu. Wakati anaondoka maduka yetu mawili yalikua na mtaji kama milioni mia mbili.
Nilimchukua dada yangu akawa anauza duka moja, jingine aliuza mke wangu na mimi nikwa ninasimamia tu. Sikuweza kuonana na yeye, aliondoka na mtoto na alienda kujifungulia kwao moshi, sikuwasiliana na yeye tena. Mwanzo mambo yalianza kwenda vizuri, lakini Biashara zilainza kuyumba, vitu vinaisha tunakua hatuna pesa ya kununulia mzigo mpya.
Katika kuhangaika niliambiwa kuwa ni yeye ananiloga, tulihangaika sana na dawa na kila kitu lakini mwisho nilikuja kugundua kuwa, kumbe dada yangu pes azote alikua na mwanaume anamhudumia, yeye hajaolewa ila ana mtoto na pesa zangu zote alikua anampelekea mwanaume ambaye ni mume wa mtu. Mke wangu naye niligundua kuwa anajenga kwao, anasomesha ndugu zake na ni mtu wa matumizi, niliamua kuwafukuza wote, nilimfukuza dada yangu na kumpa talaka mke wangu kwani waliniibia sana.
Pia mke wangu ni kama alikua hataki kuishi na mimi kwani nilikuja kujua kuwa kila akipata mimba alikua anazitoa. Niliamua kusimamia Biashara zangu mwenyewe lakini ukweli nikuwa nimeshindwa, Biashara nyingi alikua anazijua yeye, alikua anajuana na watu wengi sana kiasi kwamba kuna ambao walikua wana uwezo wa kumpa vitu kwa mali kauli. Mimi haiku hivyo kusema ukweli nimechanganyikiwa kwani nilikua na mkopo benki nimeshindwa kulipa na nyumba imeuzwa.
Niliamua kumtafuta yule mwanamke ili tufunge ndoa na tuishi kama familia mimi na wanangu lakini nimekuja kugundua kuwa ameolewa, alikua ni muisalamu kuna mwanaume wamekutana naye ni muikristo wamefunga ndoa ya kiserikali na wako vizuri. Anafanya Biashara ileile ya vyomvo na ana duka kubwa tu Arusha, anaishi na watoto wangu.
Usione kwanini nimekutafuta, nimeona kabisa kuwa huyo mwanamke anakusoma, na nimchangiaji wako mkubwa, najua ananipenda na najua kuwa watu wanakusikiliza. Kwanini aishi na mwanaume ambaye si wadini yake, mimi nipo tayari kumuoa, tuna watoto wawili yeye bado hajazaa na huyo mwanaume, natamani nikupe namba yake ili umuambie madhara ya ndoa ya serikali umuambie kuwa nipo tayari kurudiana naye kwani yeye ndiyo kila kitu kwangu.
JIBU LANGU; Kwa kawaida huwa naanza na pole, lakini kwako tuiweke pembeni kidogo, nitakujibu kistaarabu sana kwani habari za Azam zimeitengeneza siku yangu imekua nzuri. Iko hivi, katika maisha unatakiwa kujua kuwa kuna watu wana upepo wa pesa, yaani kuna mtu akigusa kit utu hata kama ni mavi basi yanapanda bei unashangaa yanageuka mbolea anapiga pesa.
Huyo mwanamke alikua na upepo wa pesa, ndiyo maana wewe ulihangaika wee ulipokutana naye ukakutana na upepo wake ukafanikiwa. Ukaona labda ni akili zako, dada zako ambao waliishi nawewe miaka nenda miaka rudi huna kitu eti umepata ndiyo wanakupangia namna ya kuzitumia, wanaume wenngi wanafanya hili kosa.
Unakuta kabla ya kuoa hana kitu, ana kazi, ana elimu lakini hana pesa,a anaoa mambo yanabdilika anafikiri ni yeye kumbe hata kama mkewe hafanyi kazi lakini kaja na upepo wa pesa. Mwanamke mwenye upepo wa pesa siku akiondoka basi jua kuwa anaondoka nazo. Sasa wako kaondoka nazo, umesema unataka niongee naye, sijui kama yeye ni mjinga kiasi hicho kuwa anamsoma Iddi Makengo halafu aje akuamini tena.
Lakini hata kama angekua mjinga kiasi hicho, kwamba aache ndoa yake aache kila kitu chake kurudi kwako. Lakini kama ukinipa namba yake, ukaniambia niongee naye, ningemuambia kuwa dada acha ujinga, huyo si mwanaume ni nuks,a chana naye ni bora usiolewe kwanimmbali nakuwa alikufanyia mambaya lakini ni mshenzi na mbinnafsi kiasi kwamba anataka uache ndoa yako ili ukampe mali. Hivyo najua kama ananisoma ashapata jibu, ila kwako, ile pole niliyoiweka pembeni mwanzo nikupe sasa tu kuwa POLE ndiyo maisha umepishana na gari ya mshara vumilia!
0 Maoni