Image result for mchaichai

Leo kwenye safu yetu hii tutaona jinsi unavyoweza kumvutia mumeo kwa kutumia mchaichai ambao ni maalumu kwa kuleta mvuto kwa mwenye uhitaji.
Wanawake wengi humiminika kwa waganga kutafuta mvuto kwa ajili ya kumuweka mumewe karibu lakini wanasahau kuwa nyumbani kuna kiungo asilia ambacho unaweza kukitumia na kuutengeneza mvuto wewe mwenyewe.

Jinsi ya kufanya mchaichai huo ili uwe na mvuto?
Tafuta mchai chai mwingi uchemshe sana mpaka uwe na rangi yake. Chukua chumvi ya mawe nayo ichanganye kwenye maji hayo kisha nuia mvuto oga asubuhi na jioni.Kwanza utakuwa unanukia vizuri lakini pia utakuwa na mvuto wa aina yake kwani utanukia mwili mzima na mvuto wako utarejea kwa mumeo.Mbali na kutia mvuto, mchaichai ni kiungo chenye uwezo wa kuondoa mikosi yote.