
MDOGO WANGU
hakuna sehemu nyingine ambayo unaweza kumsoma mmeo / mkeo mtajiwa zaidi na kwenye urafiki na uchumba.
. Kama unaona ndoa yako sasa inakushinda jua kwenye uchumba ulikua nafuraha ya kuolewa hukua na muda wa kumsoma na kumwelewa mchumba wako ni mtu wa namna gani..
Maana ulipaswa uchumba ukushinde na wala si kusubiri ndoa ndio uje uone kua uliolewa na mtu asiye sahihi..
Katika maisha ya uchumba umakini unatakiwa sana tena sana.. Maana hapo ndipo palipo na hatima ya ndoa yako....
Ili ujue huyu mme au mke wako mtajiriwa ni sahihi kwako maswali yafuatayo ndio yakufanyia kazi kipindi cha uchumba
:-maana
Matatizo mengi yanaanza hapa, asilimia kubwa ya wachumba, hawana muda wa kuhakikisha anamfahamu mchumba wake vizuri. Kuna mambo ya kuangalia kwa undani katika uchumba.
1. Je mchumba wangu ni mtu wa namna gani?
2. Je mchumba wanagu anatambua thamani ya utu?
3. Je mchumba wangu ni mwelewa?
4. Je mchumba wangu ni mvumilivu?
5. Je mchumba wangu anaweza kujitoa kwa ajili yangu?
6. Je mchumba wangu anathamini furaha yangu?
7. Je mchumba wangu anaweza kuomba msamaha?
8. Je mchumba wangu anampenda Mungu?
9. Je mchumba wangu ni wa dini moja na mimi?
10. Je mchumba wangu yupo tayri kupokea majukumu yetu ya pamoja?
11. Je upo huru kwa mchumba wako kuongea naye jambo lolote?
12. Je mchumba wangu ni rafiki yak wa pekee?
13. Je mchumba wangu ni kimbilio langu?
14. Je mchumba wangu ananisikiliza au tunasikilizana?
15. Je mchumba wangu amerithika kuwa na mimi?
Lakini wengi wenu mnajua uchumba ni ule ukweli tu wa mtu wako kua anakuja kujitambulisha au yupo tiaria kwenda kujitambulisha basi
Lakini uchumba upo hapo kwenye maswali hayo juu
Je mchumba wako yupoje?
0 Maoni