MABUSU YANAVYOLETA HAMASA YA KUFANYA MAPENZI

Related image

Busu lina nini kinachoweza kubadilisha hisia kitu kinachofurahisha mpaka kukufanya uone raha ya kuvutia kabisa? Pengine ni hali ile ya kuwa karibu mno na mtu mwingine au hisia kali za mwili wako wakati wa kulidaka BUSU LA MPENZI!

Baadhi ya mabusu yanahusisha midomo yako na shavu la mtu Mwingine kama ishara ya mapenzi au unaweza kumbusu rafiki yako mdomoni kuonyesha mapenzi ya kirafiki. Hata hivyo wapenzi wanapobusiana, sio tu wanabusiana kwa shauku kubwa, wanaweza pia kuhusisha ulimi ambao unaongeza chachandu zaidi.

MAMBO YA KUZINGATIA.

Usitumie kila wakati wa kubusiana kama ni mwanzo wa tendo la ngono. Kubusiana, kwa lengo la kuishia hapo tu kuna raha yake! • Weka mdomo wako safi na hakikisha unapiga mswaki kabla ya kumbusu mwenzio . Hakuna kitu kibaya zaidi kama kumpiga busu mtu mwenye harufu mbaya mdomoni. • Midomo yenye unyevunyevu: Midomo yako iwe na unyevu kidogo unapopigana busu. Pitisha ulimi wako kwenye midomo kabla ya kupiga busu. • Baadhi ya magonjwa ya kujamiiana, ukiwemo UKIMWI yanaweza kuenezwa kwa kupitia mabusu mazito mazito kama una vidonda au michubuko mdomoni. Hakikisha kuwa mdomo wako ni safi kabisa kiafya na mafizi yako hayatoi damu, huna vidonda mdomoni kwa sababu kuwepo kwa damu kunakuongezea hatari ya upata maabukizi.“Busu linanipa hisia ambazo si rahisi kuzipata kutoka kitu kinginechochote. Busu linanihakikishia wakati wowote ninapokuwa na wasiwasi au sina hakika.

Chapisha Maoni

0 Maoni