AANGAIKI NA WEWE USIANGAIKE NAE.

Anae kuumiza uliyempenda saaana.
Jifunze kupotezea kwa maana si kila unachopenda moyo ni halali yako.
Moyo unatamani chochote hata kama kwa kuangalia kwa macho huwezi kukipata.

Kuna watu hawana time na wewe na ni wazi si jambo mpaka uambiwe utakiwi.
Mwenye lengo,nia na mpango na wewe hakosi kushikamana nawe kwa nyakati zoote,za furaha,za huzuni n.k.
Akosi kujua leo yako imeanzaje,imepitaje na mipango yako ya kesho na kuendelea.

AJABU YA MAPENZI.
Ajabu anaekupenda huna mpango nae,mwenye mpango nae hana mpango na wewe.
Haihitaji kwenda kwa mganga kujua,au Mungu akuoteshe kuwa ni wako au si wako.

Haijalishi mlianza vizuri,kuanza sio kazi,kazi ni kuendelea na kufika mwisho.
Kuna watu wanaingia kwenye mahusiano si kwa mpango wa Mungu,si kwa kufika mbali,ni vitamaa tu,pesa,mwili na sifa.
Angalia upime kwako nini amependa.

Usishangae wala usiangaike kuomba ushauri kama unaemuangaikia hana mpango na wewe.
Unaangaika wewe kwa sms,kwa simu,unamtaext asubuhi unajibiwa jioni,na uenda asijibu kabisa.
Yuko busy hakuna mfano,ila mwanzoni alikuwa busy na wewe muda wote.
Yuko online ajibu meseji zako na ameziona.

UTAMJUAJE.
Penzi lenye afya alihitaji kitu zaidi ya utu wako,tabia zake na zake zinajenga penzi imara la uhaminifu.
Leo anakuja anatangza shida zake,sio
Mwanaume anakuja anatanguliza faragha,vikao Guest.sio
Ni tamaa tamaa mwanzo mwisho.
Usipoteze muda kusubiri Treni Bandarini,unaelekea Kigoma unasota Bandari kungoja Treni,,? utachekwa

UNAJITOAJE.
Ukiamua kutoka utatoka tu.
Haijalishi kiasi gani unampenda.
Kuwa busy,usikumbuke mema yake,mazuri yake.
Usitafute taarifa zake ikiwezekana usiwe karibu nae au urafiki nae kwenye mitandao no facebook,no instagram,Twittern na mingine yoote,futa no yake na picha zake,yaaani full empty kila kitu chake kwako.
Anza mazoezi gym, nenda beach, nenda kwenye mchezo migeni ambayo huijui katizame
Usisikilize nyimbo za mapenzi au kuangalia movie za mahaba
Sio kitu rahisi ila kitapotea utamsahau.
Penda kitu moyo unapenda kurefresh mind,jichanganye na watu utoke ulipo.
Zaidi ya Yoote kwa Imani yako soma vitabu vitakatifu na kuomba Mungu.

Related image

Chapisha Maoni

0 Maoni