Usilazimishe kila mtu uliyekutana naye katika maisha yako ya MAPENZI awe wako milele.

Usilazimishe kila mtu uliyekutana naye katika maisha yako ya MAPENZI awe wako milele.
Wapo watu watakuja maishani mwako kukujenga kiakili na kifikra
Wapo wengine watakuja ili kukufundisha namna ya kuishi na mwenza wako
Wapo wengine watakuja ili kukupa mbinu za kumdhibiti mwenza wako kimahaba
Kuna wengine watakuja kukuimairisha kinafsi ili moyo wako usiishi kwa mateso
Lakini pia wapo ambao watakuja ili kukufanya uijue thamani yako ingawa wanaweza kuwa wa kupita tu
KWA HIVYO, Unalo jukumu la kukubaliana na majira ili kuweza kumpata yeye huyo atakaye kukuta umekomaa kiakili na mwenye ufahamu.
Unaponyanyasika sana kwenye mapenzi jua uko shuleni, kubali kufundishwa ili baadae uweze kuwa mhitimu.
Inaumiza sana kuona uliyempenda yeye alikuwa na sababu zake kwako LAKINI haina maana kuwa huwezi kumpata mwingine
Ziko nyakati ngumu zimeandikwa kwako lakini kwa imani yako kuna nyakati nzuri zitakuja na utasahau yaliyokuumiza.
Kuna wengi watakufanya ujifunze kauli za ki laghai na kuwajua matapeli wa mapenzi #MadamKasema
Kubali kudharaulika ili uheshimiwe, kubali kutupwa ili uokotwe, kubali kutemewa mate ili aje wa kukuosha, kubali kushushwa thamani yako ili ushikwe na wajuao thamani yako.
Si kila aliyesema NAKUPENDA alimaanisha, wengine walisema ili KUKUPUMBAZA.
LAKINI nikutie moyo haijalishi umeumizwa mara ngapi, umelia mara ngapi MTUMAINIE MUNGU, HAKUNA LA KUMSHINDA.

Related image

Chapisha Maoni

0 Maoni