
Pesa, magari, mume, mchumba, mke wote hao hawawezi kukupa amani ya moja kwa moja maana vyote hivyo vinamapungufu yake.
Mazingira yaliyothibitika kuwa na amani kubwa hata kama una matatizo kiasi gani ni yale mazingira ya maombi.. Hii ni kwa sababu katika maombi unakuwa unafanya mazungumzo na Mungu. Muda huo kelele za matatizo ambazo zimejaa kichwani kwako unakuwa umeziweka pending. Muda huo hata shetani mwenyewe anakuwa anakuonea wivu maana anajua fika umefanya maamuzi sahihi kuzungumza na Mungu wako.
Omba dua, sala zako mlalamikie mja wako utaona jinsi utavyokua
Na amani na kutua mzigo ulio nao.. Mungu pekee ambaye ukiongea naye kwa njia ya maombi, urasikia unasikilizwa na mambo yako yanafanyiwa kazi
Hebu acha kuhangaika na mwanadamu.. Acha kuhangaika na mtu hajibu sms zako
Acha kuhangaika na mtu anakuona hujitambui
Acha kuhangaika na mtu anakuona huna point kwake.
Mwambie Mungu akupe heshima ya kuonekana bora kuliko alivyokuchukulia
Sema Mungu mimi ni wako niliwapa nafasi wanadamu lakini wamekuja kuni chambua katika mapungufu yangu na kuniumiza
Sasa Mungu naomba uwashangaze, nataka nifanye biashara nataka nifuzu masomo nataka nipate kazi, nataka kipato changu kiongeze ili walivyo waza waone walikosea maana hata kabla ya kukutana nao wewe ndio ulikua ukifadhiri na kunipendezesha
.. Mimi @maisha_halisitz
Nakuambia utatua mzigo mkubea sana, utajiona mpya kabisa
Lalamika na Mungu ndio atakeye jibu sms zako na simu zako..
Uwe na wakati mwema.
0 Maoni