SHAIRI:NAKUTUNUKU UPENDO

NAKUTUNUKU UPENDO

1.Upendo nakutunuku, ugomvi kwangu marufuku.
Moyoni nina shauku, lako shavu kulibusu,
Sauti yako ya kasuku, inaishinda ile ya zuku,
Nakutunuku upendo, ewe mzuri wa mwenendo.

2.Dini ya mola umeshika, pete hakika nakuvisha,
Stara yako dumisha, vile Rasool alivyofundisha,
Quraan kuishika, swala kunikumbusha,
Nakutunuku upendo, ewe mzuri wa mwenendo.
3.Nyingi dua naomba, kwa Jalali bila choka
Akulete mahabuba,uliyejawa mengi mahaba,
Unayetunza zangu shida, nje faida kutowapa,
Nakutunuku upendo, ewe mzuri wa mwenendo,

4.Jicho lako la mahaba, mwili wako wa huba,
Niondoe kwenye shida,kwa sauti nzuri ya kaswida,
Penzi lako sitoshiba,wanikanya kwa tasfida,
Nakutunuku upendo, ewe mzuri wa mwenendo.

5.Kidole changu nitunzie, Dini ya mola ikazanie,
Upole ujifunze, mazuri uniambie,
Dua zikufikie, mola wepesi akufanyie,
Nakutunuku upendo, ewe mzuri wa mwenendo.


6.Jikoni nitapika mie, wewe nguo nifulie,
Jina bwege wanipatie, ntaziba sikio nisisikie,
Shetani asinipitie, upweke ujisikie,
Nakutunuku upendo, ewe mzuri wa mwenendo.

7.Kosa niadhibu, kunikumbusha wangu wajibu,
We ni wangu tabibu, pale niwapo na gadhabu,
Usiku tusujudu, makosa yetu kutubu,
Nakutunuku upendo, ewe mzuri wa matendo.

8.Machozi ntakufuta, penzi la kweli kukupa,
Makosa yako nitafuta, kauli chafu sitokupa,
Mimi kwako kuruta, saluti kwako nakupa,
Nakutunuku upendo, ewe mzuri wa matendo.

9.Pamoja tuzeeke,kifo  kitupe upweke,
Kwa lako penzi niteke,moyoni nikuweke,
Nitekenye nicheke,nidekeze nideke
Nakutunuku upendo, ewe mzuri wa matendo

10.Mkweo mpambe, kwa zuri vazi atambe,
Mvishe na kitenge,mpe na kiloba cha sembe,
Usisikilize wapambe,wanao piga vijembe,
Nakutunuku upendo, ewe mzuri wa matendo.

Chapisha Maoni

0 Maoni