MWIBA WA WIVU:SHAIRI.

MWIBA WA WIVU.
         
Mimi ni mjinga kwenye kujifunza lakini ni mwelevu kwenye kuukubali ujinga.Jana ilikuwa yako yenye furaha, ukaisaliti. Leo yenye upendo ukaichezea hukujua kama kesho ni yenye maumivu,alijali furaha yako kwa kutoa machozi yake. ukayapuuza.

Tabasamu la upendo wangu kwake linakuumiza, unatamani kufurahi naye wakati ulishindwa kumfurahisha hakuna kikubwa kwake ninachompa, bali ujinga ulioukataa mimi nimejivisha. Samahani kwako ulikuwa ni wimbo usiovutia, ajabu leo kwangu ndicho kinachomvutia mpaka mahaba anaugua.

   SHAIRI
1.Shilingi kwangu hajalamba,Kwako mpaka pochi Kachukua, 
  Ulijua pendo unamtunukia ,Kumbe sumu unamjengea,
  Ulipokosea ndipo ninapitia, Mungu akipenda nitakuachia, 
  Habari zilizokufikia kweli namchumbia, Ukipenda Hudhuria ukikerekwa potezea.

2.Mwanaume si kuonesha ubabe, Yakupasa penzi ulibebe. 
  Ufalme wa pendo umpende, Sio mateke umpige,
  Mwanamke  maua harufu inayovutia, Uliyachukia ndani nimeyafungia,
  Nakushangaa unavyoumia ,Mwenyewe uliniletea, 

3. Ulipomuacha hukufikiria kuwa anaweza kuolewa? 
    Ukweli nakuhurumia, Ila nikikuachia utazoea, 
    Nilimkuta analia, leo kutwa kucha anajichekea,
    Huzuni imemuondokea, Furaha imejitawalia,.

4. Kwako alififia, Kwangu amejinawilia, 
    Shepu amejitokea, Sura yake inavutia,
    Kilio alicholia ,Kwangu ameshajisahaulia,
    Kama anataka kuumia ,Kwako atarejea,

5.  Nauli nitampatia, Maumivu aje kujipatia, 
     Furaha niliyomjengea, Atakuja kukuigizia.
     Mwenzio nampikia, Wewe chakula ulingojea.
     Nguo zake namfulia,Kitanda namtandikia.

6. Mahabuba nampa mahaba, Akikunja sita namkunja saba, 
    Wewe ulimuona kahaba,Vibao ukamzaba,
    Furaha kwake ilikuwa haba, Kwangu apagawa na huba,
    Makosa yako yamenifunza, Penzini nateleza.

7. Huyu mtoto anaweza, Hivi kwanini ulimpoteza?,
    Jicho lake akizungusha, Mimi mihemo inaongezeka, 
    Nywele zake nikishika, Mwili wa msisimka, 
    Sauti anazonipa, Sichelewi kutapika,

8. Binti ameumbika, Talaka sitompa,
    Majina mengi nimeitwa, Ila kwake nimefika.
    Raha anazonipa, Sifikirii kumuacha.
    We mdomo vimbisha, Ila ujumbe umefika.

9. Pendo linaumiza, Dahari sitomliza,
    Daima nitamchombeza,Kwangu asijeondoka,
    Watoto nitampa, Akilini asije nifuta.
    Kwa penzi apenzika, Mwenyewe athibitisha.

10. Moto ungeukoleza, safari ungemfikisha
      Hatua yako moja, Pumzi zimekuisha.
      Njiani unamuacha, akiwa hajaridhika,
      Vyuma ninavyompa, sijui kama atakukumbuka.

      MWIBA WA WIVU UMEKUCHOMA, MAHABA YAMEKUISHIA.
Image result

Chapisha Maoni

0 Maoni