Niseme tena kwa kauli kubwa..

Related image


Niseme tena kwa kauli kubwa.. Songa mbele! Mahusiano yako yamevunjika, siku, mwezi, miezi au mwaka. Ex wako amesha move on na anafurahia maisha na mwingine. Wewe bado uko busy kumuombea mabaya ili kwamba ajute kukuacha.. kweli ? Hapana, wewe Songa mbele.

Haitajalisha ni kwa kiasi gani ulimpenda mtu na namna gani unavyojisikia vibaya kwa aliyokufanyia, jilazimishe kusahau na anza safari yako upya. Hakuna haja yoyote ya kumuombea mabaya.

Inatakiwa uelewe kuwa mahusiano yako yamefeli, kubaliana na hali hiyo, kama ni kuomba, omba Mungu akupe ujasiri wa kusonga mbele na kukupa moyo wa msamaha.

Ndio inauma sana, uliwekeza muda mwingi sana kwake, ulivumilia mengi na nia yako ilikua nzuri tu ya kuokoa mahusiano hayo. Ulifanya mambo ya msingi kabisa. Hivyo usijilaumu sana, unastahili kuwa na furaha.

Anza kufanyia kazi nafsi yako, jitathimini na anza upya. Maisha huwa hivyo, muda mwingine huja kwa namna ya kuumiza mno. Ila hatutapaswa kukata tamaa, hali unayopitia ni ya muda tu, hutabaki kama ulivyo!!! Ongea na watu walio kuzidi umri watakupa uzoefu wa hali
Unayoipitia..
Bado sana kuna mengi utajione bora kujihakikishia
Maisha yako binafsi kuliko ukiwa endelea kuumizwa huku hata
Huna misingi yako ya maisha bado tegemeze.. Bora uwe
Na maisha yako utaumizwa utaenda kwenye ATM
utatoa laki, utachukua marafiki zako utaenda kufurahia maisha sehemu...

Chapisha Maoni

0 Maoni