
Best
Mwanaume anayekupenda anajua afanye nini ili akufurahishe, sababu kitu pekee anachotamani kukiona usoni mwako ni tabasamu mwanana likiupamba uso wako.
Marumbano kwenye mapenzi ni jambo la kawaida, lakini siku zote amani kati yenu ndio kipaumbele chake.
Mapenzi ya kugombana kidogo na kununiana week nzima, kamwe hayana nafasi kwake.
Mwanaume anayekupenda anajua unamuhitaji, anajua unahitaji muda wake, unahitaji uwepo wake, unahitaji penzi lake, unahitaji akujali, unahitaji akupe kipaumbele na unahitaji faraja kutoka kwake.
Kamwe hawezi kusema yuko busy kiasi cha kushindwa kujua umeamkaje, umeshindaje, unaendeleaje, bila kusikia sauti yako, au hata kukaa na wewe kwa dakika kadhaa kukwambia kiasi gani anakumiss, na anakupenda.
Sababu siku zote upendo uliopo ndani ya mwanaume humfanya ahitaji kuwa karibu na yule ampendae aidha ana kwa ana, au kimawasiliano.
Mwanaume anayekupenda anajua ni jukumu lake kujitoa kwa kila kitu kwako, bila kujali anasacrifice vingapi kwaajili yako.
Na chochote anachotoa anatoa kutoka moyoni bila kuhitaji malipo kutoka kwako.
Acha kabisa kudanganyika kwa mtu ambaye chochote atakachokupa, anatarajia malipo ya sex na muda mwingine hatoi hadi umpe kwanza.
Mwanaume anayekupenda anajua wewe ndo chaguo lake la maisha yake, ana malengo na wewe.
Ndio maana haoni tatizo kushare ndoto zake za maisha na wewe, kukushirikisha na kupanga mipango ya kimaisha na wewe.
Mwanaume anayekupenda huwa caring, loving and overprotective.
Anajua wewe ni mali yake, na hataki kushare na mtu.
Anajua kukujali ni jukumu lake, na hataki kusaidiwa na mtu.
Anajua kukuonyesha upendo ni muhimu na ni lazima, na hujitoa kwa kila jambo ili uzidi kufurahi na kuhisi unapendwa.
Hujihisi raha kukwambia anakupenda, amekumiss, kukusifia na kukupamba kwa maneno matamu.
Sababu yote hutoka moyoni, hawezi zuia hisia zake juu yako.
Dada zangu, hebu mtazame mwanaume uliyenae.
Kama unaona ana tabia zifuatazo basi jua haupo na mwanaume, upo na mvulana asiyejitambua au upo na mwanaume lakini hakupendi. - Anaweza kaa week, mwezi bila kukutafuta na siku akikutafuta basi jua ana hamu na mwili wako.
Ukimuuliza why alipotea, anakwambia "Nilikuwa busy".
0 Maoni