Muda wa usichana ni mfupi.

Image result for adrian mcdonald photography


Ni vema msichana ukajipanga kwa kipindi hiki cha umri wa usichana wako. Msichana unapaswa kuishi maisha sahihi, utunze mwili wako na uwe kielelezo bora au mfano wa kuingwa kwa wanaokutazama.

Elimu ya utambuzi ni kitu muhimu kwa binadamu aliyekamilika, pamoja na kujipa kipaumbele kwako wewe ni msichana wa kisasa. Uzuri ulio nao leo hii wewe msichana wa miaka 21, 22, 23... hautakuwepo miaka saba ijayo hasa kama utajiachia hovyo hovyo kwa wanaume na kuutumia mwili wako vile watakavyo.

Tunza usichana wako na ishi kwa stara ili kujiwekea mazingira mazuri kwa ajili ya maisha yako ya sasa na baadaye. Heshimu kila mtu anayekutana naye mbele yako naye atakuheshimu. Kuwa na msimamo thabiti kwa yeyote mwenye lengo la kuharibu mustakabali wa maisha yako.

Chapisha Maoni

0 Maoni