TANGA RAHA - 5

Related image


Chombezo : Tanga Raha
Sehemu Ya Tano (5)

Tukaipota sehemu na kutokea sehemu ambayo kuna eneo kubwa lenye moto mwingi.Watu wengi wakiwa wamo kwenye bwawa la moto.Miili yao inatobolewa na funza wakubwa walio nenepa sana na wana midomo inayo fanana na nng’e,Nikabaki nikijaribu kutazama kama nita-weza kujaa baadhi ya watu ila sikuweza kuzitambua sura zao kutokana ni nyeusi sana,Vilio vili-tawala katika kila sehemu ya bwawa la moyo
“Hawa nao wamefanya nini?”
“HAWA NI WALE WOTE WANAO ENDENDA KINYUME NA TARATIBU ZA HUKU KUZIMU”
“Kivipi?”
“KUNA WATU AMBAO WANAMUABUDU SHETANI,SIKU AMBAYO WANAVUNJA MASARTI YA SHETANI BASI HULETWA HUKU,NA HUWA WANAKUFA KWA SIKU ZAO WAO WENYEWE ILA SI ZILE ALIZO ZIPANGA MUNGU”
“Mmmmm,sasa ikifika siku zao za kufa inakuwaje?”
“WANATOLEWA HUMU NA KUPELEKWA KATIKA SEHEMU AMBAYO YUTAIENDELEA”
Kila sehemu ya ziwa la moto kunamiminika uji uji wa moto kutoka juu sana,sehemu ambayo ukiitazama huoni mwisho wake.Uji unafanana sana na uji wa volcano inayo toka kwa wingi.
“UNAWAONA WELE”
Mmoja wa watu wangu walio nizunguka aliunyoosha mkono kwenye upande wa kushoto wa sehemu tuliyopo.Nikaona kundi kubwa watu wakiwa wanalia kwa vilio vya ajabu sana na miili yao ikidonolewa na mandege makubwa mawili,yenye sura za kutisha sana.Midomo yao ikiwa ni mirefu sana na inafanana na misumeno mikubwa ya kukatia mbao
“WALE NI WATUMISHI WAONGO,KAMA WALE AMBAO UMETOKA KUWAKAMATA.NA WALE WANAPATA ADHABU TOFAUTI SANA NA WEZAO”
Hali ya mandege makubwa ikawa na kazi kunyofoa nyofoa nyama za miili ya watumishi hao,kiasi kwamba kila ninapowatazama nikajijihisi ndio mwili wangu ndio unavyo nyofole-wa,Tukaendelea kwenda mbele hapo ndipo nilipokutana na mavitu ya kutisha yenye minguru-mo mizoto kiasi kwamba nikabaki nikiwa nimeyatazama,
“Ni manini haya?”
“HAO NI MAJESHI WA HUKU KUZIMU,ENDAPO SIKU KUTATOKEA VITA KATI YA MALAIKA WA MUNGU GABRIEL AKIWA NA MAJESHI YAKE BASI UJUE ANAPAMBANA NA HAYA MA-DUDE.HAPA YAMELALA ILA YAKIPEWA NGUVU NA LILE JOKA NDIO UTAONA JINSI YANAVYO FANYA KAZI”
“Mmmmm.....!!”
“USIGUNE NDIO HALI ALISI”
“Na vita hivyo husababishwa na nini?”
“UTAJUA,DAKIKA ZETU ZIMEKWASHA TUNARUDI DUNIANI”
Tukaondoka zetu na kuanza kwenda juu kwa mwendo wa kasi,Tukatokea sehemu ya bahari ambapo tuliingilia mara ya kwanza.Wakanikabizi fimbo yangu ya dhahabu,wakanirudisha hadi nyumbani huku mkono mmoja nikiwa nimembebe mwanangu.Rahma akanishangaa baada ya kuniona nikiwa nikitokea kwenye msit ulipo karubu na nyuma yetu
“Eddy ulikuwa wapi?”
“Kuna sehmeu nilikwenda mara mara moja”
“Huyo mtoto umemtoa wapi?’
“Nimemuokota huku porini”
“Mmmmm mtoto mwenyewe mbona wa maajabu ajabu hivyo?”
“Hata mimi mwenye ninashangaa,Ndio maana niliamua kuja naye”
“Eddy,hembu wape hao viumbe vyako kumla huyo mtoto”
“Ili iweje?”
“Eddy ninamashaka kabisa na huyo mtoto.Nafsi yangu hainipi jibu kabisa juu ya huyo mtoto”
Nikataka kumjibu Rahma kwamba huyu ndio kiumbe wake aliye tolewa tumboni mwake Olvia Hitler kwa madai ya kumsaidia katika kumlea
“USIDHUBUTU KUNYANYUA KINYWA CHAKO KUMWAMBIA KWAMBA HUYO NI MWANAE”
Sauti ilinionya,Nikampita Rahma na kungia zangu ndani.Nikamlaza mtoto kitandani japo ni-meambiwa kuwa ni mwanangu ila hata mimi mwenyewe nikaanza kupata mashaka juu ya mto-to.
“Eddy,yaani huyu mwanao ndio umeamua kumlaza kwenye kitanda ambacho tunalala mimi na wewe?”
“Si mtoto jamani”
“Ahaaa hembu mtafutie sehemu umuweke.kumbuka kuwa mimi ndio mshauri wako mkubwa na hii pete nilivalishwa kwa kazi hiyo.Hembu naomba unisikilize mume wangu fanya hivyo”
Nikamnyanyua mwanangu na kumpeleka chumba cha pili na kumlaza kitandani,Nikamtazama kwa muda,kichwani kwachangu sikupata jibu la kueleweka.
“Labda ni kutokana na jinsi alivyo kaa tumboni mwa jini”
Nilijisemea mwenye kimoyo moyo.Nikaufunga mlango na kutoka nje.
“NI MUDA WA KUWAHUKUMU HAWA WOTE,AKGIZA WAPELEKWE KULE KWENYE LILE ZIWA LAMOTO.ILA HAWA WATAPATA MATESO MAKALI KULIKO WENGINE KWA MAANA WANAKWENDA KULE WAKIWA HAI”
“Wote”
“WOTE NDIO”
“Hawa viumbe vyangu watarudi kweli?”
“NDIO NITAKUWA PAMOJA NAO”
“Nahitaji siku na wewe nikuone,kwa maana tunazungumza pasipo mimi kukujua”
“UTANIONA”
Nikafanya kama suti ambayo inanishauri muda wote akilini mwangu,Nikawaagiza majini kuwachukua watumishi wote.Ndani ya dakika moja watumishi wote wakapotea mbele ya macho yangu.
“Eddy wanakwenda wapi wale?”
“Kutoswa baharini.”
“Eddy mbona unafanya kazi nyingine pasipo kunishirikisha?”
“Ahaa wacha wakafe”
“Sawa,twende ukashuhudie hicho kiumbe chako huko ndani”
“Si amelala?”
“Wewe twende ukajionee”
“Ngoja nitakuja”
Rahma akaondoka akiwa amenuna.Majini walio salia nikawaamuru kuingi kwenye handaki ambalo walikuwa wakiishi na sikuufunga mlango.Nikiwa ninarudi kwenda ndani nikastukia kumuona bibi aliye nitibu akiwa amesimama mbele yangu
“Bibi nini tena?”
“Kuna tatizo?”
“Tatizo gani?”
“Umewatoa sadaka viumbe vyako.Pili unaongozwa na roho potofu na huyo unaye zungumza naye ni yule mwanaume jini uliye tembea na mke wake?”
“Nani?”
“Hilda,Si unamkumbuka vizuri?”
Mapigo ya moyo yakanienda mbio kiasi kwamba nikawa sijui nifanye nini.Bibi akabaki akiwa ananitazama
“Bibi mbona sikuelewi?”
“Utanielewa,Kumbuka nilikupa kifimbo ambacho kingekutambulisha kwa kila ambaye unazun-guumza naye kama ni mbaya kwako au si mbaya kwako,ila umekiweka na kutumia hiyo fimbo kubwa japo ina uwezo ila si wautambuzi kama ilivyo kile kifimbo changu kidogo”
Nikashusha pumnzi nyingi.Gafla nikamuona Rahma akitoka ndani kasi huku akipiga ke-lele.Ikanibidi kukimbia na kwenda kumshika
“Nini wewe?”
“Nenda kajionee jitoto lako”
Nikakimbilia ndani na kwenda moja kwa moja nikaingia chumba alipo mtoto,Sikuyaamini ma-cho yangu kwani nilimkuta amekuwa mkubwa na kufikia ukubwa babu mtu mzima mwenye mandevu mengi na anatisha kupita maelezo,akanitazama kwa jicho lake kililo kubwa kama gololi za kuchezea pooltable
“NATAKA DAMU YAKO”

Nikabaki nikiwa nimesimama kama ninasubiri kupapigwa picha ya mnato,kukimbia ninataka ila miguu inashindwa,Nikajikuta nikitabasamu kama mtu aliye pumua kwa njia ya haja kubwa mbele ya mama mkwe.Likasimama na kuanza kunifwata kwa mendo wa taratibu kuja sehemu nilipo.Nikataka kurudi nyuma ila nikijikuta miguu inazidi kuwa mizito na kubaki nikiwa nime-simama kama mlingoti.Likanisogelea na kuushika mkono wangu wa kulia,akautazama sehemu ya giganja na gafla sehemu ya juu ya kiganja,akaing’ata na kuanza kuinyonya damu.Kitu kilicho nishangaza,sikuweza kupata maumivu ya aina yoyote japo ninaona damu zinanichuruzika pembeni.Kitu kilicho zidi kunishangaza,kila jinsi anavyozidi kunyonya damu yangu ndivyo jinsi anavyo badilika.kutoka katika uzee kurudi kwenye ukijana zaidi.Akaniachia mkono wangu na kuwa kijana mdogo kama wa umri wa miaka kumi na mbili huku akifanana na mimi kila kitu ambacho mimi ninacho,kuanzia sura
“Nikinyonya zaidi,damu yako nitarudi kuwa mtoto”
Alizungumza na kuzidi kunishangaza.Akanitazama kwa macho makali kisha akarudi na kukaa kitandani,akachukua shuka na kujifunga
“Baba njoo ukae hapa”
Alinionyesha sehemu ya kukaa,pembeni ya kitanda,taratibu nikajizoa zoa hadi kitandani na ku-kaa pembeni yake.Ukimya wa dakika kadhaa ukakatiza wakati wote nikiwa nikimtazama jinsi alivyo
“Baba,ninaamini kuwa mutakuwa munaniona kuwa mimi ni kiumbe cha ajabu sana kutokea kwenye maisha yanu”
“Hapaana,mwanangu”
Nilijikaza tuu kusema hiyo mwanangu ila kiukweli,sina imani naye kabisa huyu mtoto ambaye kwa sasa ninafanana naye na wala siwezi kupinga kitu cha aina yoyote.
“Baba mimi ni binadamu ila pia ni shetani”
Nikastuska kidogo,japo nimepewa mamlaka yakuwaongoaza viumbe wa aina hii,ila kwa hapa mapigo ya moyo yakapoteza kabisa muelekeo wake
“Usistuke,baba.Kwa jina munaweza kuniita Lusifah”
Kwa mara ya kwanza maishani mwangu kuona mtoto anajichagulia jina la kujiita tena jina le-nyewe ni lakishetani.
“Kwa nini nikuite hivyo?”
“Ndilo jina ambalo mimi nimepewa kabla ya kuzaliwa”
“Kabla ya kuzaliwa kivipi?”
“Kipindi nilipokuwa tumboni mwa mama yangu wa kwanza,sikuweza kuelewa kitu chochote ila baada ya kupelekwa tumboni mwa mama yangu wa pili hapo ndipo nilipo anza kusikia kila kitu ambacho kinaendelea duniani”
Nikashusha pumzi nyingi,Kigugumizi cha gafla kikatawala kooni mwangu.Hata nilicho hitaji ku-muuliza kikayayuka kichwani nikabaki nikiwa ninamtizama
“Naomba ukamuite mama”
“Mama?”
“Ndio mama yangu,Si Rahma”
Nikanyanyuka,kitendo cha kufungua mlango nikamkuta Rahma akiwa amesimama mlangoni akiwa analia.NikamtizamaLusifah kitandani kisha nikamtazama Rahma ambaye hakutaka hata kunitazama usoni
“Unaitwa huko ndani”
“Eddy,siwezi kuwa na toto kama hilo jibabu”
“Shiiii taratibu,atakusikia”
“Na anisikie,Eddy kumbe umenidanganya kuwa mtoto umemuokota ila kumbe ni lijibabu”
“Mama mimi sio babu”
Sote tulistushwa baada ya kumuona mtoto akiwa amesimama pembeni ya Rahma.Lusifah akamshika mkono Rahma na hapo ndipo nilipo muona Rahma akitetemeka mwili mzima hadi haja ndogo ikaanza kumtoka
“Baba na mama,nimekuja kuwaokoa kwa maana munapo elekea nyinyi ni kwenye vita ambayo nyinyi kama nyinyi hamuta weza kuimudu”
Rahma akazidi kutetemeka,kunishika akawa anatamani ila kimbebe mkono wake wakulia ume-shikwa na Lusifah.
“Mama usiniogope,mimi ndio mwanao uiye niweka tumboni kwa kipindi kifupi kabla sijatolewa na kwenda kulelewa kuzimu na shetani”
Kilio cha Rahma kikazidi kusikika kwani mara ya kwanza alikuwa akilia kimya kimya.
“Leo tumepatikana”
Nilijisemea kimoyo moyo,huku nikimuonea huruma Rahma wangu
“Baba wala hamjapatikana,ni woga wenu tuu.Ila mutanizoea”
Akaanza kutembea na Rahma kuingia naye ndani na kukaa naye kitandani.Kwa ishara akaniita nikae na mimi kitandani.Akaishika mikono yetu na kuikutanisha kwa pamoja
“Ninafuraha sana kuwa na nyinyi kwa wakati huu”
Alizungumza huku akiwa ameyafumba macho yake na sura yake akiwa ameigeuzia juu.
“Unalia nini na wewe?”
Nilizungumza kwa sauti ya chini sana huku tukitazamana na Rahma.
“Mama,kwa nini unanikana kuwa mimi sio mwanao?”
“Hapana”
Rahma alijibu huku mwili wake ukiendelea kumtetemeka hadi nikamuonea huruma,
“Nawapenda sana wazazi wangu”
“Hata mimi pia”
Nilijibu mimi mwenyewe pasipo Rahma kuzungumza chochote.Lusifah akatuomba tutok nje apumzike kwani tayari gizi lilisha tawala anga.Moja kwa moja Rahma akakimbilia chumbani kwetu,nikamfwata na kumkuta akipanga nguo zake kwenye kijiegi kidogo
“Unakwenda wapi?”
“Eddy mimi ninaondoka”
“Tatizo ni nini linalokufanya uondoke?”
“Eddy unadhani,hayo mambo niyakawaida?”
“Ila mke wangu,yule ni mtoto wetu?”
“Eddy mtoto gani,si alikuwa ni jizee la miaka hata tisini,sasa hivi unaliita mtoto”
Rahma alizungumza kwa sauti ya kufoka
“Sawa,basi kama ni kuondoka subiri hata kupambazuke ndio uondoke ila si huu usiku”
“Eddy,siwezi kulala tena hapa.Waala kuendelea kuishi hapa”
“Sasa mpenzi wangu......”
“Eddy hakuna cha sasa.Ninakupa uchague,Kati yangu na hao mapepo yako?”
Nikashusha pumzi na kupiga hatua za taratibu hadi sehemu ambayo Rahma yu-po.Nikamkumbatia kwa nyuma taratibu
“Mke wangu,unanipenda?”
Nilizungumza kwa sauti nzuri na nzinto kiasi iliyo jaa mahaba
“Hata kama Eddy,hilo sio swali la kuniuliza mimi?”
“Hapana,nijibu”
“Ndio,ninakupenda”
“Mimi ni nani yako?”
“Mume wangu”
“Una nisikiliza”
“Ndio,ila kwa hilo jitoto lako mimi sinto kusikiliza ng’oo”
Nikaipandisha mikono yangu hadi kifuani mwa Rahma na kuanza kuyashika maziwa yeke,ila akaitoa mikono yangu kwa nguvu.
“Eddy niache,sipo kwenye masihara”
Rahma akafunga zipu ya kibegi cheka,akafungua droo na kuchukua funguo za gari la mzee Ngo-da alilo kuja nalo siku ambayo alitafunwa na majini.Akatoka nje huku akiwa katika mwendo wa haraka.Sote tukafika sehemu yenye gari,kabla hajaingia ndani ya gari akanigeukia
“Nakuuliza kwa mara ya mwisho,UNANIPENDA MIMI AU HAO MAPEPO WAKO?”
“Ninakupenda wewe”
“Ingia kwenye gari”
“Ngoja kwanza”
Nikataka kuondoka ila Rahma akanishika mkono
“Ingia kwenye gari”
Nikaingia ndani ya gari,kila Rahma anavyojaribu kuliwasha gari likakataa kuwaka.Akajaribu kila mbinu anayo ijua yeye ila gari linawaka kidogo na kuzima
“Shuka basi usukume”
Nikashuka,nikaanza kusukuma.Ila gafla nikastuka kumuona Lusifah akiwa pembeni yangu aki-nisaidia kusukuma,Nikataka kuzungumza akakiweka kidole chake mkononi akinizuia nisizun-gumze chochote.Gari ikawaka,Lusifah akakunja ngumi mkono wake wa kulia akiniomba tuigonganishe mikono yetu,watu wengi wamezoea kusema nikampa Tano.Akaniomba niingie ndani ya gari
“Wewe nenda,nitawaangalia hawa wengieni”
Nikaingia ndani ya gari na kujifunga mkanda.Safari ikaanza huku njia nzima kila mtu akiwa kimya,Rahma akazidi kuongeza mwendo wa gari,japo ni usiku sana anajua jinsi ya kuyakwepa mashimo na madogo madogo yaliyopo barabarani.Tukafika barabara ya horohoro na kuendelea na safari yetu.Hadi tunaingia Tanga mjini muda ilisha timu saa tisa usiku.Jiji zima lipo kimya kila sehemu ambayo tunapia.Hata zile heka heka za watu wanao lala nje kwenye vibaraza vya watu hatukuweza kuwaona.
“Tunakwenda kwangu au wapi?”
“Tunakwenda kwetu”
“Kwenu kufanya nini?”
“Kule ni kwetu na nikwa wazazi wangu”
“Hembu simamisha gari kwanza”
Rahma akasimamisha gari pembeni na kulizima.
“Rahma,kumbuka kwenu tuliondoka vipi.Iweje leo unataka twende?”
“Eddy nisikilize kwa umakini.Nilikuvumilia kwa kipindi kirefu.Sasa nimechoka tena nimechoka”
“Umechoka na nini?”
“Eddy,huna mapenzi ya dhati na mimi “
“Haaaa hayo yote yametokea wapi tena?”
“Eddy,sikupendi na sikuhitaji tena katika maisha yangu.Niliona nikuzungumza hivi kule porini utanifanya chochote utakacho.Ila nipo nyumbani sasa,Sitaki unitafuta wala unisumbue kwa chochote”
Maneno ya Rahma yakanifanya niishiwe nguvu kabisa.Na jinsi Rahma anavyo zungumza anao-nekana hana masihara kabisa na kitu anacho kizungumza
“Wewe si mtu wa kutembea na Halida,wale walimu wezako machangudo.Nashukuru kwa kuni-leta ninacho kuomba ushuke ndani ya gari”
“Lakini Rahma ni nani aliye kuambia haypo mambo?”
“Ahaaa ulizani dunia ina siri.Kamuulize yule bibi yako uliye niacha naye nje pale”
“Ndio amekuambia haya maneno?”
“Jibu,swali.....”
“Shuka,ndani ya gari”
Rahma alizungumza huu akinisukuma sukuma nishuke kwenye gari.Hasira zikaanza kunipanda juu ya bibi aliye nitibu.Nikashuka ndani ya gari na Rahma akawasha gari na kuondoka kwa kasi.Maumivu makali yakakatiza kwenye moyo wangu,kwani kila kitu kinacho tokea kwenye maisha yangu ninaona kama ni ndoto.Sikujua ni kitu gani kilicho mpata Rahma.Sikuwa na jinsi zaidsi ya kwenda nyumbani kwangu.Nikiwa maeneo ya Mkwakwani gafla nikaanza kuhisi upeppo mkali ukija kwa kiasi mbele yangu.Radi nyingi zikaanza kutawala kwenye anga huku mawingu mazito ya mvua yakikusanyika kwa kasi.Ndani ya dakika kadhaa mvua kubwa iliyoongozana na radi kali ikaanza kunyesha.Nikatafuta sehemu ya kujibanza pembezeni ya ukuta ili kuacha mvua ipite
Nikiwa nimeuegemea ukuta niskastukia nikikabwa shingo kwa nguvu na mkono ulio tokeza kwenye ukuta nilio uegeme huku mkono huo ukiwa na kucha ndevu za kutisha

Cha kwanza kukiwahi ni kuishika shingo yangu kwa haraka na kuanza kuminyana na kiganja hiki kilicho ikamata shingo yangu,nikafanikiwa kujinasua kwenye kiganja,kitendo cha kugeuka nyuma nikakikuta kikimalizikia kuingia ndani ya ukuta.Nikataka kuondoka ila ujasiri mkubwa ukauvaa mwili wangu,nikarudi nyuma hatua chache na kuiangalia jinsi nyumba hii ilivyo kuan-zia juu hadi chini.Ni nyumba inayoonekana kujengwa miaka mingi ya nguma,kwani hata kuta zake ni zile zilizo jengwa kipindi cha ukoloni.Nikiwa ninaendelea na uchunguzi wangu wa macho nikaanza kuzisikia sauti za watu wakingong’oneza ndani ya ukuta ambao nilikuwa nimeuegemea.
Kila ninapojaribu kuitafsiri hii lugha siipatii jibu kwa maana,kinacho zungumza hakieleweki ila watu hao wanazungumza kwani wanaonekana wanamambishano ya wao na wao.Nikazunguka upende wa pili wa nyumba na kukuta milango na madirisha vikiwa vimefunga,gafla taa zilizokuwa zinawaka nje zote zikazima gafla na kiza kinene kikatawala kila eneo,huku mvua iliyo andamana na radi zikiendelea kurindima kwa kasi ya ajabu.Nikaanza kuondoka taratibu,hatua chache kutoka nyumba ilipo nikasikia jina langu likitajwa ndani kwa sauti ya juu na kunifanya nigeuke nikiwa na mshangao mkubwa
Nikatamani kurudi nyuma ila nikaanza kuondoka,kila ninapopiga gatua moja mble ndioyo sauto ya mtu anaye liita jina langu huku akilia ikizidi kuongezeka.Nikayaziba masikio yangu na kwenda mbele zaidi ila nikajikuta saut inayo niita ikizidi kongezeka.Wasasiwasi mwingi ukaanza kunitawala,niakageuka na kuanza kurudi sehemu ilipo nyumba,hadi ni nafika mlango ukafunguka na wala sikumuona mtu aliye ufungua mlango zaidi ya giza nene lililo tawala ndani ya nyumba.
“Njoo”
Sauti ambayo ilikuwa ikiniita ikaanza kuniiomba niingie ndani.Nikajitazama kuanzia juu hadi chini na kuanza kupiga hatua za taratibu na kuingia ndani,gafla mlango ukafunga kwa nyuma na nikaanza kuhisi vitu vikianza kunishika shika mwilini mwangu.Sikuwa na budi zaidi ya kuanza kupiga mayowe ya kuomba msaada,ujanja wote ukaniishia.Gafla taa za chemli zipatazo nne zikawaka kwenye kona zote za chumba.Sikuamini kuona watu wengi wakiwa wamerundikana kwenye nyumba hii ambayo kwa ndani haina vyumba kama nyumba nyingine.Watu ambao wapo humu ndani wanavuja damu kwenye miili yao
“Tusaidie.....”
Mmoja wao alizungumza huku sehemu ya bega lake ikiwa imenyofolewa badhi ya nyama.
“Kwani nyinyi ni kina nani?”
“Sisi ni watu ambao,tumetafunwa na majini,tusaidie mkuu”
Dada mmoja alizungumza huku machozi yakimwagika sana.Nikajikuna kichwa kwani sikujau hata nianzie wapi kwani kila ninaye mtazama amejeruhiwa kwenye sehemu ya mwili wake.
“Kwani,imekuwaje hadi mumeliwa hivi?”
“Kuna majini wametuteka huko nje,wametuingiza humu ndani.Humla yoyote kwa wakati wo-wote watakapo amua kufanya hivyo”
“Kuna watu wengi,wameliwa na muda huu wamekwenda kutafuta watu wengine wapya wa kuja kututafuna.Tafadhali tunakuomba utusaidie”
“Kwani munashindwa kutoka nje?”
“Hakuna mwenye uwezo wakutoka nje,hata mlango ukiwa upo wazi ukidhubutu kutoa mguu hata mmoja hapo nje unanata hapo hapo”
Nikabaki nikiwa nimesimama,sikujua hata ni vipi niwasaidie,katika kupitisha pitisha macho yangu nikawaona wazazi wa Rahma wakiwa wamejilaza kwenye moja ya pembe huku baba Rahma akiwa ametafunwa sehemu ya shavu la upande wa kulia.Katika kuangalia angalia tena nikaona baadhi ya waalimu wezangu wakiwa katika kundi hili la watu wanaosubiria kutafunwa na majini hao
Nikawafwata wazazi wa Rahma,walipo niona wakastuka hususani baba Rahma,ambaye hadi meno yake yanaonekana kwani nyama yote ya shavu imeliwa.Nikachuchumaa na kuwatizama kwa macho yaliyo huruma kwani hali zao zipo mbaya.Mara ya kamza sikumuona mama Rahma vizuri.Ila yeye ametafunwa sehemu kubwa ya mbavu zake
“Mwa....na..ngu,naku...omba utusaidie”
Kwa mara ya kwanza baba Rahma kuniita mwanangu,hapo ndipo nikaamini kuwa matatizo hayana mbabe,Japo alizungumza kwa shida ila niliweza kumuelewa.Nikasimama na kuwataza-ma watu wengine.Sehemu nyingi ya chini kuna mafuvu mengi na mifupa ya watu walio tafun-wa.Moyo ukazidi kuniuma sana baada ya kukuta baadhi ya wanafunzi wangu wakiwa wameje-ruhiwa vibaya wengine wapo katika hali ya mwisho katika maisha yao.Kitu kingine kinacho zidi kuwaumiza watu wa humu ndani ni njaa kali iliyo changiwa na kukaa kwa muda mrefu pasipo kula.
“Hayo majini wapo wangapi?”
“Wapo wengi tuu,kuna madogo dogo ambayo yanakuja kuja humu na kumchukua wanaye muona amenono na kumtafuna”
Dada mmoja alizungumza,kidogogo akionekana ananguvu nguvu.
“Sasa hivi wamekwenda kukusanya watu walio salia salia”
Nikasikia sauti ya baba Rahma ikiniita kwa shida,nikaenda hadi sehemu walipo na kuchuchumaa tena
“Mwa...nang...u mji mzim...a hauna....watu.Ila wewe ninakuele..kez..a Sehemu moja hivi?”
“Ni wapi baba?”
“Kweny...e nyumba ya...ngu,kuna chumba c...ha maktaba ya vitabu,Humo kuna kitabu ambacho kinaelezea maji...tu ya aiana hii.Ukikisoma hicho kitakusaidia kutuokoa sisi humu nd....ani”
“Sawa baba”
“Pia kuna sehemi,ina mishale....kama Rahma yupo hai muu...lize atakuo....nyesha”
Nikakaa kimya kwani kwa hali ambayo ninaambiwa juu ya hawa majini ninaimani ni lazima watakuwa ametafunwaa.Nikanyanyuka pasipo kumpa jibu lolote baba Rahma nikawafatwa watu ambao nilikuwa ninazungumzanza nao,kabla sijawauliza chochote nikaisikia sauti
“Wanarudi,”
Mzee mmoja alizungumza huku akichungulia nje kwenye uwazi mdogo sana.Moyo ukanipasuka ila watu wawili wakanikumbatia na kunipakaza damu zao na kuniambia nikae nyuma yao kwa ni majini hao wanautambuzi wa kiumbe kipya kinacho ingia ndani ya jumba lao,isitoshe mimi ni mtu wa pekee ambaye nimeweza kuingia ndani ya nyumba hii,wakazizima taa ambazo wameziwasha na giza kali likatawala.Mlango ukafunguliwa kwa fujo na yakasimama majini mawili yaliyo shiba huku mojalikitafuna kichwa cha mtu huku likimalizia malizia kuunyonya ubongo uliopo ndani ya kichwa alicho kishika.
Yakanza kunusa nusa na pua zao zilizo wafunuka kama visima visivyo toa maji kwa kipindi kirefu.Yakapiga hatua hadi mbele ya watu walio nificha nyuma yao,wakaendelea kunusa nu-sa.Kajacho kembamba kakanza kunimwagika,huku mapigo ya moyo nikiyasikilizia jinsi yana-vyokwenda kwa kasi,Gafla mtu aliye simaa kando yangu akashikwa kwa mkono mmoja na jijini hili na kuyanyuliwa juu,Bila ya huruma akamgawanyisha vipande viwili na damu zinazo toka jini likawa linajimwagia kwenye kichwa chake kilicho kaa vibaya na kina mabonde bonde mengi.
Likaanza kuutoa utumbo wa mtu aliye mchukua na kuanza kuutafuna kama linakula soseji,mwili mzima ukanisisimka,nikashindwa kuvumilia na kujikuta nikisimama kwa hasira,kitu ambacho kinanishangaza jini hili lianendela kuutafuna utumbo wa mtu huyu huku likinitazama na mijicho yake mikubwa.Mkono wangu wa kushoto ukaanza kunitetemeka,nikautazama vizuri na kuziona pete zikiwa zinawaka mwanga mkali ambao tangu nizivae sijawahi kuuona mwanga kama huu.Jini likamtupa mtu linalo mla na kuanza kuyaziba macho yake liliuogopa mwanga.Nikamnyooshea mkono wenye pete na jini likazidi kurudi nyuma na kuungana la jingine ambalo linakula ubongo.Nikazidi kuyafwta hadi sote tukatoka nje na mlango ukajifunga.Yakaanguka chini na kutulia gafla mwanga wa pete ukazima,nikashusha pumzi nyingi.Nikarudi kwenye mlango nikajaribu kuusukuma kwa ndani ila haukufunguka.Nikaitazama mijini na kupiga hatua za haraka hadi sehem ilipo angukia.
Nikaitazama kwa umakini,kusema kweli inatisha kwani miili yao imevimbiana vimbiana viyaya sana,Galfa jini moja likafumbua jicho lake na kunistua.Nikajaribu kuinyoosha pete yangu ila ha-kuna hata moja ambayo haikuwaka.Jini la pili nikafumbua macho yake na wote wakawa wananitazama huku wakikoroma kwa milio ya kutisha.Sikuwa na jinsi nyingine zaidi ya kuaza kukimbia,nikastukia jini mmoja likinipiga kofi lililo nitoa kabisa kwenye barabara na kunigongesha kwenye mti ulio pembezoni mwa barabara.Nikayashududia yakisimama huku yakionekana kuwa na hasira sana.
Picha ya mtu aliye katwa katika vipande viwili vya mwili muda mchache ulio pita ikanijia kich-wani.Nikayaweka maumivu kando na kusimam na kuanza kukimbia kwa kasi ambayo Mungu amenijali.Yakaanza kunikimbiza,hatua yao moja kwangu ni sawa na hatua kumi nikiwa nina-tembea kwa mwendo wa kawaidia.Ikanilazimu kukimbia kwa kasi kubwa huku,nikastukia ku-muona Lusifah akiwa pembeni yangu
“Habari yako baba?”
Lusifah alizungiumza huku naye akikimbia kwa kasi ambayo ninaikimbia mimi,nikashindwa hata kujibu salamu yake kutokana na pumzi kuanza kuniishia kifuani mwangu.Gagla nikalikwepa gari ambalo lilikuwa linakuja kwa kasi mbele yetu na likaenda kugonga majini ambayo yalikuwa yananikimbiza na kuyarusha pembeni.Nikazisikia breki za gari hili zikililazimisha gari hilo kusimama barabarani.Sikuwa na hata hamu ya kutazama nyuma zaidi ya kuendela kukimbia,sikumuoa Lusifah sehemu aliyo kwenda.Taa za gari zinazokuja nyuma yangu zikanifanya nilipishe.Hadi linafika usawa wangu ikanibidi nilitazamame
“Eddy ingia ndani ya gari”
Ni sauti ya Rahma ndio ilinisemesha na kujikuta nikijirusha ndani ya gari baada ya kunifungulia mlango wa gari.Kwa kupitia kioo cha pembeni nikayashuhudia majini yanayo tukimbiza yakitufwata kwa kasi.Nikamuona Lusifah akipambana nayo huku na yeye akiwa anabadilika badilika katika maombo tofauti.Rahma akatafuta sehemu iliyo tulia na kulisimamisha gari,tukaka kimya tukisubiriana kila mmoja aanze kuzungumza aanacho taka kuzungumza.
“Eddy wazazi wangu....”
Rahma alizungumza huku machozi yakianza kumwagika,nikajizuia kumuambia kuwa wazazi wake wapo kwenye jumba linalo mililiwa na majini,
“Eddy sehemu zote za mji zipo kimya,hakuana mtu hata mmoja,nyumba zimeharibiwa vibaya”
“Yote hii ni kwaajili ya hayo majini yako”
Rahma akaendelea kunilaumu,nikabaki kimya kwani sikujua nijitete vipi kwake.Rahma akanitazama kwa macho makali kisha akaupitisha mkono wake kweny shingo yake na kuanza kuuninyonya mdomo kwa fujo.Akauagungua mkanda wa siti aliokuwa amefunga na kunikalia mapajani huku akiaendelea kuninyonya midomo yangu.Rahma huwa akifika katika swala zima la mapezi huwa hana masihara hata kidogo,akaanza kulivuta shati langi hadi likakatika vifungo yote.Akaendelea kuninyonya kifua changu kwa hasira hadi akaanza kunikwaruza kwenye mbavu kwa kutumia kucha zake
“Mapenzi,fujo”
Nilijikuta nikiropoka hii ni baada ya Rahma kunikwaruza kwa nguvu kwenye mgongo wan-gu,akasitisha kulifanyan zoezi analo taka kulifanya,Akaniangali kwa macho ya makali na akani-piga kofi
“Eddy umesemaje?”
“Ahaaa....eende...”
Akanipiga kofi jengine huku akiniporomoshea matusi mengi,akaendelea kufanya anacho kifanya akaanza kuufungua mkanda wa suruali yangu,kabla hajamaliza nikstukia kuona jitu jengine kubwa na lakutisha,lenye mabawa likisimama mbele ya gari letu na kusababisha kishindo kikubwa hadi gari ikatingishika
Rahma akaniacha na nikamsukumia kwenye siti yake na tukabaki tukiwa tumetazamana na jitu hili ambalo linatisha kupita maelezo.Rahma kwa haraka akawasha gari na kuaanza kuirudisha nyuma kwa mwendo wa kasi,Cha kushangaza jitu hili halikuwa na habari na sisi zaidi ya kubaki likitutuzama.
“Tunaelekea wapi?” Nilimuuliza Rahma
“Hata mimi sijui”
“Twende kwenu”
“Kwetu!!?”
“Ndio kuna kazi nataka kwenda kuifanya”
“Kazi gani?”
“Wewe twende,utaiona huko huko”
Tulizungumza huku Rahma akiendelea kuongeza mwendo wa gari,Tukafika nyumbani kwao na kukuta geti likiwa wazi,Tukashuka ndani ya gari na kujibanza pembezoni mwa geti huku tulichungulia ndani kuangalia kama kuna hali yoyote ya watu kuwemo.Giza zito lililopo kwenye jumba la kina Rahma ikazidi kutopa hofo,Nikatangulia mbele huku Rahma akinifwata nyuma.Tukaingia ndani sote tukiwa makini,Hali ya kuzizima ndani ya nyumba ya kina Rahma ikatufanya tushindwe hata kuwasha taa,mwanga hafifu wa mbalamwezi unao pita kwenye madirisha makubwa ya kioo,unatusaidi kuona vitu vilivyomo ndani ya sable.
“Kipo wapi chumba cha kuhifadhia vitabu?”
Nilizungumza kwa sauti ya chini ya kumnong’oneza Rahma ambaya alinitazama kwa mshangao
“Eddy,umejuaje kwetu kuna chumba cha kuhifadhia vitabu?”
“Rahma hilo sio jibu ninalo litaka mimi.Wewe niambie ni wapi kilipo”
“Twende”
Tukapandisha ngazi za gorofani taratibu huku sote tukiwa makini sana.Tukaingia kwenye moja ya chumba kimoja na kukuta vitabu vingi vikiwa vimepangwa kwenye mbao zilizo pangiliwa vizuri ukutani,Nikabaki nikiwa nimeshika kiuno kwani sikujua ni wapi nianzie hii ni kutokana na wingi wa vitabu uliopo katika chumba hichi kikubwa
“Baby kwani unatafuta kitabu gani?”
“Kuna kitabu ambacho kinaelezea kuhusiana na majini”
“Kinaitwaje?”
“Hata mimi sijui”
“Sasa utatafutaje kitu usicho kijua?”
“Washa taa kwanza”
Rahma akawasha taa,tukaanza kushirikiana kutafuta kitabu kimoja baada ya kingine.Huku tu-kiwa tunatazama jina la kitabu na picha kama vinaendana na elimu ya majini.Zaidi ya nusu saa tukawa na kazi ya kutafuta ila hatukufanikiwa kukipata kitabu
“Eddy nimechoka ngoja nikanywe maji”
“Powa”
Raham akaondoka na mimi niakendelea kutafuta kitabu ambacho baba Rahma aliniagiza,Nikiwa ninaendelea endelea kutafuta kitabu nikastuka na kuhisi kuna kitu kinakatiza nyuma yangu,Nikageuka haraka na kukuta hakuna kitu
“Rahma”
Niliita ila sikusikia muitikio wa Rahma,kwa mbali wasiwasi ukaanza kuniajaa,Nikaendelea ku-chukua kitabu kimoja baada ya kingine,gafla taa ikazima.Nikazidi kustuka nikageuka nyuma na kutazama kama kuna kitu ambacho kimeizima taa ila sikuona chochote.Haikuwa ni umeme ku-katika kwani nyumba ya jirani inawaka taa.Nikapiga hatua za haraka hadi ilipo swichi na kuiwasha.Nikarudi kwenye msururu wa vitabu na kuendelea kutafut,na safari hii nikaongeza kasi ya kutafuta.Nikastukai vitabu kama sita vikianguka kutoka juu ya kabati lililopo eneo hili.Nikastuka ila baada ya kuoni ni panya ndio amevigusa vitabu hilivyo anguka kidogo nafsi yangu ikatulia
Nikavitazama vitabu vilivyo anguka na kukiokota kimoja kati ya sita vilivyo anguka,nikakutana na picha ya majitu yanato tisha huku juu yake kukiwa na maandishi makubwa yaliyo andikwa
“EVIL SPIRIT”(Nafisi ya kishetani)
Nikakifuta vumbi na kufungua kurasa ya kwanza,kitu kilicho nichanganya ni kukuta maandishi yakiwa yameandikwa katika luhga ya kifaransa japo jina limeandikwa kwa kingereza
“Umekipata”
Sauti ya Rahma ikanistua na kunifanya nimtazame kwa woga
“Ndio nimekipata,ila kimendikwa kwa lugha ya kifaransa”
“Unaijua kuisoma?”
“Hapana”
“Hembu nione”
Nikampa Rahma kitabu na akakitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kukisoma taratibu na kunitafsiria taratibu
“Dunia itabadilika na kutawaliwa na nguvu za shetani.Ambazo zitawateka watu wengi na ku-waweka katika sehemu moja.Utawala huu utaanzia katika bara la Afrika upande wa mashariki,utaendelea kusambaa kwa kasi kuelekea upande wa magharibi mwa dunia”
Rahma akameza mate kidogo na kuendelea kukisoma kitabu
“Watu watagawanyishwa miili yao kwa kunyofolewa baadhi ya nyama katika miili yao na ma-shetani yanayoitwa LUSIFA”
Moyo ukapoteza hata muelekeo baada ya kusikia jina la mwanangu ambaye wala simuelewi elewi
“He...hee mbu rudia hapo”
“Wapi?”
“Yanaitwaje?”
“Lusifa”
“Endelea”
“Halii hiyo itaendela kuwaangamiza wanadamu wote watakao kutana na majini hao wabaya.”
“Hembu nenda nenda mbele,Hakuna sehemu iliyo andikwa jinsi ya kuwazuia”
“Acha kihere here mtoto wa kiume kama ungekuwa unaweza kukisoma kifaransa ungekuja ku-kisoma”
“Haya mama”
“Hali hii inaweza kuondoka pale tu,mtu mwenye nyota kubwa na yenye nguvu na mamlaka kupita nyingine atakapo weza kufanya mambo makuu maane”
“Eheee” Nilizungumza huku nikishusha pumzi nyingi
“Kwanza awe ni jasiri katika kupambana na kila hali”
“Pili awe na msimama juu ya jambo analo liamua”
“Tatu aweze kutoa kiasi cha damu yake na kwenda kuimwaga katika bahari”
“Nne awe tayari kuyapoteza maisha yake kwa ajili ya wengine.Kwani nilazima afe”
Sikuwa na usemi zaidi ya kuguna tu,Rahma akaendelea kuzungumza
“Endapo hayo yote yataweza kufanikiwa kwa wakati mmoja basi watu wote ambao walipotezwa au kuuawa na majini hao wataweza kurudi katika hali ya kawaida.Pia na dunia itarudi katika hali yake ya kawaida”
Nikajikuta nikiikutanisha mikono yangu juu ya kichwa changu huku nikiwa nimemtazama Rahma kwa mshangao hata anacho endelea kukisoma sikuweza kukisikia kabisa zaidi ya neno la ‘LAZAMA AFE’ likiwa linajirudia rudia kichwani mwangu
“Eddy hivi unanisikiliza au ninajisomea mimi mwenywe?”
“Ehee”
“Nakuona haunisikilizi,nitaacha?”
“Endelea endele kusoma”
“Vita hiyo ni ya mtu mmoja tu,hapaswi kusaidiwa na mtu wa aina yoyote la sivyo akipata msaa-da wa aina yoyote.Hali hii itazi kuwa kubwa na dunia nzima itakuwa chini ya utawala wa Lusifa”
“Mpambanaji anatakiwa,kuwa na mishale kumi na mbili.Kila mshale atautumia katika kuanga-miza kichwa kimoja cha joka kubwa litakalo watanguliza wasaidizi wake ambao watauliwa kwa kutumia maneno haya”
“Bwana Eddy haya maneni sijui yameandikwa kwa kilugha gani?”
Rahma akanisogelea na kunionyesha maneno ambayo tangu nizaliwe ndio mara yangu ya kwanza kuyaona katika macho yangu
“Rahma”
“Bee”
“Nitakufa kwa ajili yako”
“Kwa nini ufe,mume wangu”
“Mtu ambaye anatakiwa kuifanya kazi hiyo ni mimi hapa”
“Ahaaa Eddy usinitanie”
“Sikutanii ila ni mimi hapa”
“Sasa itakuwaje”
“Sina jinsi,nitapambana na kitu chochote kitakacho kuja mbele yangu”
“Mmmmm,sasa Eddy.......”
“Hakuna cha sasa”
Nilizungumza kwa sauti iiyo maanisha kitu ninacho kizungumza ni cha kweli na hakina masihara ndani yake.Rahma akanikumbatia kwa huzuni,Gafla taa zote za mji mzima zikazima,na tetemeko la ardhi likaanza kutikisa sehemu zote za mji,Huku miale miale mingi ya kutisha ikiaanza kutoka ardhini huku ikiwa inafanana moto wa Volkano.Gafla jumba la kina Rahma likaanza kumeguka taratibu na kutufanya tuanze kukimbia kuelekea kwenye ngazi.
Kabla hatujaanza kushuka ngazi tukakutana na mtu aliye vaa mavazi meupe tupu akiwa amesi-mama mwazoni mwa ngazi katika sehemu ya kupandishia huku macho yake yakiwa yanawaka manga wa kutisha ulio ufanya mwili mzima kunisisimka,Tukiwa tunaendelea kumshangaa mtu huyo nyuma yetu tukasikia kishindo kikubwa kitendo cha kugeuka tukakutana na jitu lenye mabawa na meno yake yakiwa ni makali na yakutisha,na nyumba ikaendelea kumeguka vipande vipande

Rahma akazidi kuning’ang’ani mkono wangu kwani hali inazidi kuwa mbaya kadri jinsi muda unavyozidi kwenda,Mtu aliye vaa nguo nyeupe tupu akantonyooshea mkono kwa ishara ya ku-tuita tumfatwe,
“Agrrrrrrriiiii”
Jitu la nyuma lilinguruma kwa nguvu na kutufanya tushuke kwenye ngazi kwa haraka pasipo kupenda.Hadi tunamkaribia mtualiye valia nguo nyeupe naye akanza kupandisha ngazi kutuf-wata
“Edddyyy”
Rahma alipiha kelele, akimuogopa jamaa anaye panda.Nikajaribu kuunyanyua mkono wangu na kumrushia ngumi na kustukia akiuzuia pasipo kuushika na akapita pembeni yatu na kulifwata jitu lenye mabawa, na yakaanza kupambana.Tukashuka kwenye ngazi kwa haraka na kutoka nje ya jumba la kina Rahma huku tetemeko la ardhi likiendela tena safari hii likizidisha kasi,Ardhi ikaanza kupasuka vipande vipanda, kila sehemu inapo pasuka basi linatoka jidudu linalo fanana na ng’ee ila lina vichwa vyaviwili kimoja kikiwa cha simba na kingine kikiwa cha joka kubwa.
“Eddy mume wangu tunakufa”
Rahma alizungumza kwa wpoga huku akimwagikwa na machozi mengi
“Hatufi , futa wazo hilo”
Nilizungumza kumpa moyo Rahma ila ukweli ni kwama endapo tutafanya kitu cha kijinga nila-zima tufe tena kitakuwa kifo kibaya kupita vifo vyote vya watu walio tutangulia,tukaanza ku-kimbilia kuelekea baharini, huku tkijitahidi sana kukwepa mipasuko ya ardhi.Tukafanikiwa kufika kandokando ya bahari pasipo kujeruhiwa na madudu ambayo yanatisha kwa muonekano wake
“Kitabu kilisemeje?”
“Kilisema kuwa, damu imwage baharini”
Nikamtazama Rahma kwa macho makali kisha nikaanza kuangaza angaza chini kutafuta kitu chenye ncha kali, nikaokota kijiti cha mti wa mkoko chenye ncha kaliNikapiga hatua na kuingia ndani ya maji hadi sehemu ambayo, maji yananifikia kwenye magoti.Nikaunyoosha mkono wangu wa kushoto mbele na kujichoma kijiti kwenye moja ya mshipa wa damu, Damu nyingi zikaanza kunimwagika na taratibu zikaanza kuingia baharini na kusababisha maji kuanza kubadilika gafla na kuwa rangi ya damu.Nikatoka na kutazama jinsi maji ya bahari yanavyo chemka na kusababisha upepo ulio mkali sana.
Tetemeko la ardhi likaanza kutulia huku ardhi ikianza kijirudi kama kawaida,Hali ya upepo ika-zidi na kutulazimu kuweza kulala chini,Madudu ya ajabu yaakaanza kupeperushwa na kvutiwa habarini.Tukabaki kushangaa kuona yale majini ya kutisha nayo yakiwa yanavutwa na kuingizwa baharini.Hali ikazidi kuwa kwa viumbe hawa wa ajabu kuvutiwa bararini na taratibu hali ya upepo wa baharini ikatulia.
Nikasimama na kumpa mkono Rahma na kumnyanyua, tukakumbatiana kwa furaha huku tuki-pigana mabusu mfululizo ya mdomoni.
“Eddy umefanikiwa mume wangu”
“Ndio baby”
Nikamkumbatia kwa nguvu Rahma na yeye akafanya hivyo huku akiwa na furaha kubwa iliyo pitiliza kikomo.Tukiwa tunaendelea kukumbatiana gafla nikaona kitu kikubwa kinachomoza baharini, nikagundua ni joka kubwa ambalo lina vichwa kumi na mbili
“Rahma”
“Mmmm”
“Nenda kanisubirie nyumbani”
“Ehheee”
Nilizungumza huku kichwa cha Rahma nikiwa nimekielekezea nyuma yangu huku tukiwa bado tumekumbatiana, sikutaka Rahma aone chochote kitakacho endelea
“Nakuomba uende nyumbani, usiangalie nyuma utakapo ondoka hapa”
“Eddy mbona sikuelewi?”
Rahma akataka kujitoa mwilini mwangu ila nikamrudisha kifuani kwangu huku kichwa chake nikiwa nimekikandamiza begani mwangu na sikumpa nafasi ya kutazama nyuma
“Eddy do you love me?”(Eddy, unanipenda?)
“Yes my wife.....ila ninakuomba uondoke”(Ndio mke wangu........)
“Eddy hunipendi”
Rahma alianza kuzungumza huku akuanza akilia kwa uchungu
“Rahma nisikilize mimi, nakupenda na mimi ndio mume wako.Ila ninakuomba uondoke kwenda nyumbani”
Nilizungumza huku nikilitazama joka jinsi linavyozidi kujitokeza kwenye maji na kuanza kujitokeza kichwa kimoja baada ya kingine.Hadi muda huu limesha jichomoza vichwa viwili na kila linavyozidi kuchomoza kuelekea juu ndivyo jinsi vichwa vyake vinavyozidi kuchomoza.Nikaanza kurudi nyuma huku nikiwa nimemkumbatia Rahma
“Rahma ninakuomba uondoke sasa hivi”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali na kumfanya Rahma anitazame usoni mwangu, nikamuachia na akaondola taratibu huku akiendelea kumwagikwa na machozi, Rahma akapiga hatua kadhaa na kugeuka nyuma, macho yale akayatoa kana kwamba amakebwa na kitu kwenye koo.
“Nenda”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali huku nikimtazama kwa hasira
“Eddy mume wangu utakufa”
“Nimesema nenda, usije huku.Siwezi kufa niamini mimi”
Rahma akarudi kwa kasi na kunikumatia kwa uchungu, furaha ambayo ilitutawala muda mchache ulio pita ilitoweka.
“Eddy ninakupenda sana, siwezi kukuacha mume wangu ukafa.Ni bora tufe sote kuliko wewe peke yako”
“Rahma, niamini mimi, Siwezi kufa sawa”
‘Eddy unanidanganya”
“Sikudanganyi”
Joka likazidi kuchomoza vichwa vyake hadi sasa hivi tayari imechomoza vicha vyake vinavyo tisha sana.Nikambeba Rahma juu juu hadi sehemu ya mbali kidogo na bahari na kumnyonya midomo yake vya mwisho mwisho kwani kitabu kinaelezea ni lazima nife ili wengine wapone
“Rahma, niamini mimi siwezi kufwa hata kidogo.”
“Mimi ninajua tuu unanifariji”
“No sikufariji mke wangu, ninakuhakikishia siwezi kufa niombee kwa Mungu”
“Mishale utaitoa wapi?”
“Sijui, ila tafadhali ninakuomba unielewe.Kumbuka ukinisaidi ndio nitakufa, niache nifanye haya yote peke yangu”
Nilizungumza kwa sauti ya chini iliyo jaa upole na unyenyekevu mkubwa.Rahma akanikumbatia tena kwa uchungu
“Eddy nitakupenda maisha yangu yote”
“Hata mimi pia, nenda sasa”
Rahma akabaki akinitazama
“Nenda tafadhali”
Rahma akaanza kuondoka kwa mwendo wa taratibu huku akinipungia mkono, nikageuka na kukuta joka ndio linachomoza kichwa cha kumi.Nikaanza kukimbia nikielekea baharini kwa bahati mbaya nikajikwaa kwenye mizizi ya mti wa mkoko na nikaanguka chini kama gunia.Nikiwa ninajinyanyua nikaona podo lenye mishale likiwa limening’inizwa kwenye moja ya mti wa mkoko huku pembeni yake kukiwa na upinde pamoja na baadhi ya vitu ambavyo hutumika katika kufulia,Kwa haraka nikaviendea na kuchukua podo lenye mishale na kuliuvaa mgongoni mwangu.Nikaushika upinde mkono wa kushoto na kuvua shati langu na kubaki kifua wazi.Nilipo hakikisha nipo sawa nikachomoa mchale mmoja na kuuweka kwenye upinde, kitu kilicho nichanganya ni maneno ambayo yaliandikwa na sote hatukaelewa
“Vyovyote”
Niijisemea kimoyo moyo,huku nikitazama kichwa cha kumi na mili kikijichomoza kwenye maji, umbali mrefu kati yangu na joka kubwa ambalo nakumbuka nililiona kuzimu ukanipa ujasiri wa kijiamini zaidi ,nikataka kupiga hatua na kuingia ndani ya maji ila mwili wangu ukawa mzito kupiga hatua za kuingia ndani ya maji.Joka likaanza kutoa moshi mwingi kwenye pua za vichwa vyake na kilicho fwatia hapo akaanza kutoa moto mwingi kwenye midomo yake huku ukiwa unaelekea sehemu nilipo mimi
“In the name of Lord”(Kwa jina la bwana)
Nilijisemea huku nikiuvuta mshale nyuma kwa nguvu zangu nyingi huku nikitumia kamba ngumu ya manila iliyopo kwenye upinde.Nilipo hakikisha uvutaji wangu unaweza kuufanya mshale kwenda kwa kasi na mbali zaidi nikaachia huku nikiwa nimeuelekeza kwenye kicha cha sita.Kwa bahati nzuri mshale ukatua kwenye kichwa cha joka na kukifanya kichwa hicho kuanza kupaparika na kuchanguka na kusababisha joka kutoa ukelele mkali na mkubwa wa maumivu.Joka likazidi kutema moto mwingi kwa hasira, ambao hakunizuia kuifyatua mishale kuelekea vilipo vichwa vingine navyo vikapasuka
Joka likaanza kuja nchi kavu, huku likimwaga moto mwingi na sasa hivi moto wake akaanza kuutoa kwa mfumo wa madoge mabukubwa kama mpira yaliyo nfwata kwa kasi.Nikaanza kujirusha pembeni huku nikiwa ninayakwepa kwa utaalamu mkubwa, Sikubaki nyuma na kuzidi kuendelea kuifyatua mishale yangu, na kufanikiwa kuviangamiza vichwa nane na kuzidi kulizidisha hasira joka
Joka likazidi kunifwata huku likinitemea madonge donge ya moto yalito anza kubadilika na ku-wa kama mishale iliyoanza kuja kwa kasi.Nikaendelea kufyatua mishale hadi nikafanikiwa kuua vichwa viwili na kubadi kimoja, Joka likaruka juu na likazama ndani ya maji na kupotea gafla.Nikabaki nikiwa nimesimama kutazama ni wapi lilipo joka.
Nikasimama kama dakika tano na sikuona dalili yoyote ya kuwepo kwa joka, bahari nzima ikawa imetulia na upepo ukarudi katika hali ya kawaida.
“Yeeahaa”
Nikaanza kushangulia huku nikiruka ruka juu, nikaanza kupiga hatua nikiondoka baharini hu-ku nikiwa nimejawa na furaha sana.Gafla nikasutkisha nikastukia nikirushwa juu na nikiwa angani nikalishuhudia joka likiwa limeufumbua mdomo wake, huku likiningojea niingie ndai ya kinywa chake.Nikaanza kurudi chini kwa kasi kubwa huku nikipiga kelele nyigi na moja kwa moja nikaingia ndani ya mdomo wa joka

Kwa, haraka nikachomo mshale ulipo kwenye podo langu nililo livaa mgongoni, Nikiwa ninaendela kushuka katika tumbo la mwili wangu, huku nikiwa nimeibana pumzi yangu.Nikaukita mshale wangu kwenye tumbo la joka hili na kuanza kuuchana mwili wake huku nikimshale wangu kwenye tumbo la joka hili na kuanza kuuchana mwili wake huku nikiwa ninaendelea kushuka nao chini hadina kumfanya joka hili kuanza kubingiria bingiria huku maji mengi, ya bahari yakiwa yanakingia mwilini mwake
Wingi wa maji unao ingia mwilini mwa joka, yakanifanya niweza kupata nafasi ya kutoka nje ya joka hili ambalo bado linaendela kutapa tapa kwenye maji huku likitoa ukelele mkali.Jokaa likaanza kufutuka huku likiwa moto mkali, Kwa bahati mbaya likanipiga kikumbo, kwa kutumia mkia wake kilichorusha mbali na eneo alilo kuwepo na kunitoa nje ya bahari na kwabahai mbaya nikangukia kwenye kisiki cha mti wa mkono, na kutulia tuli huku giza zito likitawala macho yangu
***
“Eddy......Eddy”
Kwa mbali niliisikia sauti ya Rahma ikiniita,nikayafumbau macho yangu taratibu na kukutana na mwanga mkali ulio nipiga kwenye macho yangu, huku nikiwa, nimelala kwenye kitanda nikipelekwa nisipo pajua na pembeni yangu akiwepo Rahma naye akionekana akitembea huku machozi yakimwagika.Kila ninapojaribu kuyafumbua macho yangu, nikajikuta nikiona maruweruwe hata watu wanao kisukuma kitanda nilicho kilalia sikuweza kuwaona vizuri.Nikajikuta nikitawaliwa tena na giza kwenye macho yangu, na sikuelewa kilicho endelea.
Macho yangu yakaanza kupata mwangaza tena wakuona mwanga, nikajaribu kuyapitisha pitiasha kwenye kila kona ya chumba na kufanikiwa kutambua kuwa hapa nilipo ni hospitalini.Pembeni ya kitanda changu, kuna meza ndogo, na juu yake imejaa maua mengi pamoja na kadi nyingi, sikujua ni nani aliye ziweka, kwenye mkono wangu wa kushoto nimechomekwa mrija unaodondosha maji taratibu kwenye mishipa yangu.Tumboni kwangu kumefungwa bandeji lililo kaza, lililo zunguka sehemu nzima ya tumbo hadi mgongoni.Nikaiona kadi moja iliyo andikwa maandishi makubwa kwa kalamu ya wino
(Eddy tunakupenda sana endelea kuugua pole,MUNGU atakuponya)
Nikaunyoosha mkono wangu na kuchukua moja ya kadi na kulifungua ndani na kukuta maandishi yanayo nitakia mimi kuugua pole.Mlango ukafunguliwa na akaingia nesi akiwa amevalia mavazi mazuri.Baada ya kuniona akaachia tabasamu pana
“Habari yako kaka Eddy?”
“Salama mambo?”
“Salama, karibu tena duniani”
“Duniani kivipi?”
“Ni story ndefu, ila kwa muda huu pumzika kwanza”
“Sawa, ila Rahma wangu yupo wapi?”
“Amekwenda kupata chakula cha mchana”
“Kwani nesi, hapa nipo wapi?”
“Upo hospitali ya mkoa, Bombo”
“Sawa, ila ninaomba kama una namba ya Rahma mpigie”
“Usijali kwa hilo, kaka yangu”
Nesi alizungumza huku akionekana kuwa na furaha kubwa sana, akatoka baada ya muda kidogo akaingia Rahma, ila kitu kilicho nishangaza kidogo ni ukuaji wa Rahma.Kwani amebadilika kwa kiasi fulani, ameongezeka mwili na kuwa mrefu kidogo.Machozi ya furaha yakaanza kumwagika taratibu akapiga hatua hadi kitandani, akanikubatia huku akiendelea kumwagikwa na machozi ya furaha.Taratibu na mimi machozi yakaanza kunimwagika
“Eddy”
“Naam”
“Upo hai tena?”
“Ndio mke wangu”
“Asante sana Mungu kwa yale yoteuliyo nitendea kwenye maisha yangu, Wewe ndio muweza wa kila kitu.Ohooo asante sana MUNGU wangu”
Rahma alizungumza huku akiendelea kunikumbwatia kwa nguvu zake zote, tukakumbatia kwa dakika zaidi ya kumi huku macho yangu nikiwa nimeyafumba.Nikayafumbua macho yangu na kukutana, kama kumi na tano wakiwa na kamera za video na kamera za picha, huku kila mmoja akiendelea kuchukua tukio analo liona yeye linamfaa.
Taratibu Rahma akaniachia, akaanza kuninyonya midomo yangu taratibu huku akimwagikwa na machozi mengi.Hakujali kama kuna waandishi wa habari
“Nakupenda sana, Eddy wangu”
“Hata mimi pia mke wangu ninakupenda sana”
Baadhi ya waandishi wa habari wakaanza kupiga makofi wakifurahia tukio ambalo linaendelea kati yangu na Rahma.Mmoja wao akaguna mimi na Rahma tukamtazama
“Samahani, kwa kuwaingilia katika mazungumzo yenu”
“Bila samahani kaka” Rahma alijibu
“Kwajina ninaitwa Jumaa Hassan ni muandishi I.T.V, ningependa kujua, unajisikiaje bwana Eddy kwa sasa?”
“Mimi nipo vizuri tuu, najisikia sawa”
“Je, kwakipindi chote cha nyuma tunaweza kupata japo dondoo moja, mbili tatu hivi kwa yale yaliyo kukuta”
“Jamani samahani, natambua uwepo wenu hapa na ninawaheshimu sana ndugu zangu kwani bila nyinyi kushirikiana na watanzania wengine katika swala zima la kuendeleza maombi kwa mume wangu, leo asinge fikia hapa.Kitu amacho mimi ninawaomba kwa wakati huu.Mumuache mume wangu apumzike kidogo, na nitajaribu kupanga naye siku ambayo anaweza kuzungumza na nyinyi na mukamuhoji kila swali ambalo munalihitaji, SAWA NDUGU ZANGU”
Rahma alizungumza kwa sauti ya upole na unyenyekevu iliyowafanya waandishi wa habari kumuelewa, kila mmoja akanipa mkono wa kunitakia heri katika kupona na kutoka nje ya chumba
“Baby, hayo maua na makadi yametokea wapi?”
“Ni zawadi za watu ambao wanaendelea kukuombea kwa kipindi kirefu sasa”
“Kipindi kirefu?”
“Ndio mume wangu, ila tutazungumza siku nyingine juu ya hilo swala”
“Nidokezee japo kidogo mke wangu”
“Hapana Eddy siwezi kukuambia kuhusiana na chochote hadi madaktari wanihakikishie kuwa umepona vizuri”
“Baby mimi mbona nipo powa”
“Eddy, bado haijawa powa”
Rahma hakuweza kuniambia kitu cha aina yoyote, nikakaa hospitalini wiki mbili, huku kila sikuwatu wengi wakija kunitembelea hadi badhi ya viongozi wa ngazi za juu nchini akiwemo raisi wa nchi, nikaruhusiwa kutoka hospitalini.Siku ambayo ninatoka sikuamini macho yangu kukutana na wananchi wengi wakiwa nje ya hospitali wakinisubiri kwa hamu.Kila mmoja akaanza kushangilia kwa furaha na wengine hawakusita kuyazuia machozi yao.Baadhi yao wamevalia tisheti yeupe na yeusi zenye picha yangu huku zikiwa na maandi chini ya picha hiyo yaliyo andikwa
(EDDY WEWE NI SHUJAA WETU)
“Baby wapungie mkono watu”
Rahma aliniambia, nikawapungia watu mkono na kuwafanya wazidi kunishangilia.Kila kitu kinacho tokea kwenye maisha yangu ninaona ni kama ndoto ambayo sikutarajia kama ipo siku watu wengi watanipenda na kunishangilia kwa kiasi kikubwa kama hawa.Askari wakawa na kazi ya kuwazuia watu wasifike karibu yangu.Hadi ninaingia ndani ya gari la kifahari nikawa bado siamini kwa kile ninacho kiona.Waendesha wengi wa pikipiki wakatangulia mbele ya gari tulilo lipanda mimi na Rahma, huku likiendesha wa dereva ambaye simjui
Magari mengi nyuma yakawa yanalifwata gari letu, ikamlazima dereva kutembea kwa mwendo wa taratibu.
“Baby tunakwenda wapi?”
“Tunakwenda kwetu”
“Kwetu wapi?”
“Ni sapraiz mume wangu”
“Mmmm haya”
“Mbona umeguna, huamini au?”
“Naamini”
Rahma akanilalia kifuani kwangu, huku vidole vyake, vya mkono wa kulia, vikiwa na kazi ya kukikiminya minya kifua changu.Waendesha pikipiki wanao ongozwa mbele na gari ndogo ya polisi wakasimama kwenye jumba moja kubwa lililojengwa kwa aina yake, huku wakipiga honi nyingi, Taratibu gari yetu, ikingia ndani ya geti kubwa.Mandhari ya jumba hili yamepambwa kwa maua mazuri yakupendaza.Tukashuka kwenye gari na kwamsaada wa polisi nikaingia ndani kwani watu wengi wanatamani kuniona.Tukapandisha gorofani na kutokea kwenye sehemu ya mbele ya nyumba ambayo hata nikisimama watu wote wataniona
Sauti za wanawake zikilitaja jina langu zikaendelea kunishangilia huku wengine wakisema wananipenda sana
“Habari yenu”
Nilizungumza na watu wote wakashangilia kwa furaha
“Hatujambo”
“Jamani, sina mengi ya kuzungumza kikubwa ninachotaka kuwaambia ni kwamba ninawapenda sana na ninashukuru kwa ibada zetu mulizo zifanya kwa kipindi chote ambacho mimi nilikuwa ninaumwa hadi hapa nilipo fikia”
Watu wakaendelea kushangilia kwa furaha, kiasi kwamba nikajikuta machozi yakinimwagika na mimi.Nikashindwa kabisa kuzungumza kwa furaha niliyo nayo kwenye kwa wakati huu, rahma akanichukua na kunipeleka kwenye chumba ambacho kimejaa vitu vingi vya dhamani ya hali ya juu huku hata kitanda chake kikiwa kimetendgenezwa kwa muondo wa kipekee
“Rahma vitu vyote hivi, vimetokea wapi?”
“Ni zawadi kutoka kwa baba na mama”
“Wao mbona siwaoni?”
“Wamehamia Dubai”
“Baby, hawa watu wote wametokea wapi?”
“Eddy mume wangu, ni miaka miwili na miezi nane imepita tangu ulipo kuwa hujitambui, wala hujielewi.Sikukata tamaa juu yako ila, Mungu ni mwema hadi umerudi kwenye hali hiyo”
“Asante sana mke wangu”
Nilizungumza huku nikimvuta karibu Rahma, na akakilaza kifua kichwa chake juu ya kifua changu
“Ila mume wangu, ninasiri moja kubwa sana katika maisha yetu, ambayo inanisumbua sana kwenye kipindi chote cha maisha yangu”
“SIRI.....!!, Siri gani?”


“Nitakuambia tu mume wangu, subiri kwanza watu waondoke”
“Hapana, naomba uniambie mke wangu”
“Nitakuambia tu mume wangu, nakuomba uwe mvumilivu.Ngoja kwanza nikazungumza na hao watu nje, alafu nitarudi kukuambia”
Nikamtazama Rahma kwa macho makali ya kumchunguza, akayakwepesha macho yake katika kunitazama usoni.Akanipiga busu la shavu na akatoka nje, nikajilaza kitandani huku amani ikiwa imenitoweka kwani sijui ni siri gani ambayo Rahma anataka kuniambia.Nikasikia kelele za watu wakishangilia kwa furaha, sikujua ni kitu gani ambacho Rahma alizungumza hadi kuwafanya watu kushangilia kwa furaha namna hii.Nikanyanyuka kitandani na kuanza kutembea tembea ndani ya nyumba kutazama ubora wa chumba chetu, kusema ukweli kimetengenezwa kwenye hathi ya halil ya juu, kila kitu kimewekwa kwenye mpangilio mzuri wa kuvutia kwenye macho ya kila ambaye ataingia ndani ya hiki chumba
Nikaingia bafuni,na kukuta bafu zima, kuta zake zimesilibwa na vioo vigumu sana, Nikajitazama sura yangu na kukuta kidogo ninamabadiliko, kwini hali ya ukijana imeanza kupotea kwa mbali
“Duuu, kweli nimekuwa sasa”
Nilizungumza huku nikijichunguza vizuri, sura yangu
“Ni wakati wa mimi kuwa baba, mwenye familia bora”
Nilizungumza huku nikitabasamu, nikavua shati langu, na kubaki kifua wazi.Hapa ndipo nikaona kovu lililopo nyuma ya mgongo wangu.Nikakumbuka mara ya mwisho nilitua kwenye kisiki cha mti wa mkoko kipindi ninapambana na Joka kubwa.Nikiwa ninaendelea kujitazama kwenye kioo, gafla nyuma yangu nikaiona sura ya Olvia Hitler ikicheka pasipo kuwa na mwili, nikageuka kwa haraka huku nikihema kwa wasiwasi, ila sikuona kitu cha aina yoyote.Nikataka kupiga hatua mbele nikastukia mlango ukifunguliwa, akaingia Rahma
“Baby kumbe upo huku?”
Rahma alizungumza huku akinitazama usoni kwa umakini
“Mbona upo hivyo Eddy, kuna tatizo lolote?”
“Haa, hapana”
“Mbona kama una wasiwasi?”
“Hakuna kitu mke wangu”
Rahma akanisogelea na kunikumbatia, huku akiniminya minya mgongo wangu kwa kutumia vidole vyake
“Haumii, nikikuminya hapa?”
“Kwa mbali ninahisi maumivu, ukiniminya kwa nguvu kwenye hilo kovu”
“Pole mume wangu”
“Asante”
“Watu wako, wamesha ondoka”
“Hawajakuletea tabu?”
“Hapana, ila nimewaambia waje kesho kutwa, nitaandaa kasherehe ka kukukaribisha nyumbani”
“Sawa, mke wangu”
“Pia, nimewaambia waandishi wa habari waje wazungumze na wewe”
“Sawa mke wangu”
Rahma akafungua maji ya bomba, nne zilizo jengewa kwa juu kwenye kila kona ya bafu na zote zikaanza kuwaga maji kama mvua kubwa inayo nyeshe, Rahma akanza kuninyonya midomo yangu taratibu, huku na mimi nikianza kumvua nguo moja baada ya nyingine.Kila mmoja anaonekana kuwa na hamu na mwenzake, kwani ni kipindi kirefu sana kimepita pasipo kukutana kimwili.Tukaanza kupeana haki sahihi kama wapenzi wawili wanao penda, Utamu wa Rahma ukazidi kuongezeka, kila anacho nifanyia ninakiona kipya kutoka kwake.Mechi ikatawaliwa na furaha na matusi ya nguoni kwa kila mmoja alipojisikia kutoa tusi lake aliweza kufanya hivyo ili mradi kuongeza utamu wa mechi yetu.Hadoi tunamaliza kila mmoja, akabaki akiwa na tabasamu usoni
“Mume wangu, mbona umekuwa mtamu, umeutolea wapi?”
“Nikuulize wewe mke wangu, umekuwa zaidi ya kipindi cha nyuma”
“Ahaaa, ila asante sana mume wangu”
“Hata wewe asante mke wangu”
“Mume wangu, niliweza kuvumilia kwa kipindi chote ambacho wewe ulikuwa hospitalini, japo nilikutana na vishawishi vingi, ila Mungu aliweza kunisaidia hadi leo hii nakutana tena na wewe”
“Asante sana mke wangu, kwa maana niwanawake wachache sana wenye roho na moyo kama wako”
“Kweli mume wangu, mimi sikukutamani, nilikupenda na ninaendelea kukupenda.Kwenye maisha yangu sikuwahi kufikiria kumpenda mwanaume kama wewe, amini usiamini wazazi wangu wanakupenda tena sana, ile chuki kwao imekwisha kabisa”
“Kweli?”
“Ndio, hadi baba ametoa mamilioni yake kuijenga hii nyumba, ujue kweli kakupenda”
“Ehaaa, alafu nimekumbuka”
“Umekumbuka nini baby?”
“Naomba uniambie siri ambayo uliniambia inakusumbua?”
Rahma akanitazama usoni, sura yote ya tabasamu ikapotea nasura ya huzuni ikaaanza kuchukua nafasi yake, jambo ambalo likaanza kunipa wasiwasi wakujiuliza kuna kitu gani amabcho kimempata, Akaniachia mwili wangu na kutoa bafuni, ikanilazimu kumfwata nyuma.Sote tukakaa kitandani
“Mke wangu kuna, tatizo?”
Rahma hakunijibu na taratibu akaanza kumwagikwa na machozi, nikabaki nikiwa nimemtum-bua mimacho sijui ni kitu gani kinacho mwaga machozi
“Mume wangu, unanipenda?”
“Rahma ni swali gani ambalo unaniuliza, wakati unajua fika mimi ninakupenda kuliko kitu cho-chote kwenye maisha yangu”
“Eddy, sijui hata nianzie wapi?”
“Kivipi?”
Rahma akanitazama huku machozi yakiendelea kumwagika, hadi sura yake ikaanza kujawa na uwekundu fulani kwa mbali
“Eddy, nakupenda sana mume wangu, sipo tayari kukuona unakufa pasipo....”
“Pasipo kufanya nini?”
Rahma alizidisha kulia, na wasi wasi mwingi ukaanza kunijaa mwilini mwangu na kubaki nikiwa nimemtazama mke wangu huku kigugumizi kizito kikinijaa.Rahma akakiweka kidole kimoja kwenye lipsi zangu, kisha akanipiga busu zito la taratibu sana kisha akaendelea kuzungumza
“Eddy, na uzuri wangu wote huu.Ila sinto weza kukuzalia mtoto, sina kizazi mimi”
Nikabaki nikiwa nimeduwaa, kiasi kwamba kuzungumza ninatamani, kukaa kimya ninatama-ni.Taratibu nikajikuta nikinyanyuka kitandani na kuanza kutembea tembea ndani ya chumba bila ya kuwa na kituo maalumu
“Baby, siku ambayo nilipata mimba yako ya kwanza.Olvia alinitoa kizazi changu, na aliniambia kwamba sinto zaa maisha yangu yote”
Rahma alizungumza huku akisimama, akanishika mkono na kunitazama machoni huku akiendelea kuniangalia.Kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga, sikuamini kama Rahma anaweza kukosa kizazi isitoshe mtoto wa kwanza hakuwa binadamu aliye kamilika
“Nisamehe mume wangu”
“Hupaswi kuniomba msamaha mke wangu, tumuombe Mungu”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika, taratibu.Rahma akanikumbatia na kulala kifuani kwangu taratibu kisha akanipiga busu jengine la mdomoni, ambalo nikashindwa hata kulipokea vizuri
Siku nzima nikashinda nikiwa ninamawazo, japo usoni mwangu nikawa na kazi ya kuilazimisha furaha yangu kujengeka ila nikashindwa kufanya hivi nilivyo tegemea.Hata chakula sikukila kwa raha kabisa
“Mume wangu, nakuomba usiwaze sana juu ya kuta kupata mtoto”
“Ahaaa, usijali baby”
Rahma akawa na kazi ya kunifariji
“Hivi kipindi chote ninaumwa maisha yalikuwa yapo vipi?”
“Baby nilipitia sana maisha ya shida, nilihangaika huku na huku kutafuta njia ya kuweza kuyaokoa maisha yako, kusema kweli nilipata tabu sana kutokana hospitalini waliniambia kuwa wewe ni.....”
Rahma akanyamaza na kuniangalia kwa macho ya kuiba kisha akanitazama tena
“Waliniambia kuwa mimi nini”
“Waliniambia kuwa wewe ni mfu aliye hai”
“Kivipi, mbona sijakuelewa?”
“Waliniambia kuwa, ulisha kufa siku nyingi”
Nikabaki nikiwa nipo kimya, kama nimemwagiwa maji ya baridi, swali la kwanza kujiuliza kich-wani ni mbinu gani waliyo itumi hadi mimi leo nipo hai.Nikiwa ninaendelea kuliwazia ninalo liwaza nikamuona Olvia Hitler akiwa amesimama nyuma ya Rahma huku macho yake yakimwagikwa na machozi ya damu

Nikabaki nikiwa nimeduwaa, pasipo kuzungumza kitu chochote, Olvie akaanza kutingisha kich-wa taratibu huku machozi ya damu yakiendelea kumwagika kwa wingi, akauinua mkono wake mmoja na kuanza kuniita taratibu, hapa ndipo nilipoiona mkono wake ukiwa umejaa damu nyingi.
“Walipo niambia kwamba umekufa, ikanilazimu kufanya kitu ambacho kingeurudisha uhai wa-ko, kutokana sikuhitaji uweze kupotea kiurahisi maishani mwangu, wakati bado sijaisha nawe vya kutosha”
Hata Rahma alicho kizungumza sikukitilia maanani kwa maani macho, na akili yangu zote zili-kuwa zipo kwa Olvia aliye simama nyuma ya mke wangu Rahma.Olvia Hitler akaunyanyua mkono wake wa pili juu na kuendelea kuniita kwa ishara kiasi kwamba nikazidi kuchanganyikiwa kwa vitendo vyake
“Niliamua kwenda, India kwa wanganga wanao tumia nguvu za kienyeji.Ambapo kuna mganga mmoja ambaye ni maarufu sana aliweza kunisaidia sana, hadi akaurudisha uhai wako”
Nikayahamishia macho kwa Raham, kisha nikayarudisha tena macho yangu kwa Olvia Hitler
“Mganga yule, alikupandikiza roho ya nyoka, na kila katikati ya mwaka na mwisho wa mwaka nilazima ugeuke kuwa.......”
Rahma alisita kidogo kuzungumza kitu anacho kizungumza na nikabaki nikiwa nimemtazama kwa umakini
“Utageukuwa kuwa nyoka mkubwa, na ninatakiwa kukupa watu wawili, uwale ili uweze kuon-geza maisha ya kuishi la sivyo utakufa kabisa na nitakukosa mume wangu”
Rahma alizungumza huku akimwagikwa na machozi, nikaanza kujitazama kiungo kimoja baada ya kingine kwa maana sikuamini kama hapa mimi nilipo nimekuwa na pumzi ya nyoka.Olvia Hitler akapiga hatua moja nyuma kisha akasogea hatua nyingine moja kushoto, hapo ndipo nikamshuhudia utumbo wake ukiwa umechomoza nje, na ameushika na mkono mmoja ili usiguse chini
“Eddy”
Olvia Hitler aliniita pasipo Rahma kuisikia sauti yake kwani, Rahma hakutikisika wala kugeuka nyuma.
“Nisaidie, tafadhali”
Olvie Hitler alizungumza kwa shida, huku machozi ya damu yakizidi kumwagika kwa wi-gi.Nikasimama kwenye kiti na kuanza kupiga hatua za kuelekea alipa simama Olvia Hitler, huku Rahma akibaki akiduwaa
“Eddy unakwenda wapi?”
Sikujiu swali la Rahma zaidi ya kumuacha akinishangaa, kabla sijamfikia Olvia Hitler, Rahma akanyanyuka kwa haraka na kinishika mkono
“Eddy, unakwenda wapi?”
“Eheee”
Nilizungumza huku macho yangu yote nikiyaelekezea alipo simama Olvie Hitler
“Baby, niangalie mimi”
Rahma akanigeuza kichwa changu na nikiwa ninamtazama yeye, akanishika mashavuni kwa viganja vyake vilaini na taratibu akajivuta, karibu yake na kunibusu mashavuni
“Eddy mume wangu, nimefaya hivyo kwa sababu ninakupenda sana.Sikuweza kuishi peke yan-gu, kama ningeishi peke yangu naamini hadi sasa hivi ningekuwa marehemu”
Rahma aliendelea kuzungumza huku machozi yakimwagika, Olvier Hitler akapotea kwenye uwepo wa macho yangu
“Eddy forgive my husband, I did not mean to get you to be so bad you are, But all is because of love”(Eddy nisamehe mume wangu, sikuwa na maana mbaya ya kukufanya wewe kuwa hivyo ulivyo, Ila yote ni kwasababu ninakupenda)
Rahma alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu, na kuuminya mwili wangu.Sikujua hata cha kumjibu zaidi ya mimi machozi kunimwagika, nikamnyanyua na kumbeba Rahma hadi chumbani kwetu.Tukapanda kitandani, kutokana na mawazo mengi kichwani mwangu sikuwa na hata hamu ya kumsogelea Rahma.Taratibu Rahma akanisogelea na kichwa chake kukilaza kifuani na sote tukapitiwa na usingizi mzito
***
Siku zikazidi kwenda mbele huku nikiwa ninafurahia maisha yangu ya ndoa nikiwa na mke wangu Rahma, nikaanza kusahau hata yale mambo magumu ambayo niliyapitia.Siku ya mkutano kati yangu na waandishi wa habari ikawadia.Waandishi wa habari wapatao ishirini kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakafika nyumbani kwangu huku wote wakiwa na furaha kubwa ya kuhitaji kuzungumza na mimi
Rahma akishirikiana na wafanyakazi watatu wa ndani, wakaandaa eneo zuri la kufanyia maho-jiano katika bustani yetu ya maua, iliopo katika eneo la jumba letu la kifahari, Rahma akanitolea suti nzuri iliyo nipendeza na kuniomba nivae, huku akinisaidia kuweka weka sawa sehemu za kola ya shati langu jeupe pamoja na tai nzri aliyo ichangua
“Mume wangu umetoka chikopa”
“Wacha wee”
“Eheee, ila kuwa makini kuna waandishi wa habari wadada wazuri wamekuja hapo sema tuu ndio hivyo tena”
“Acha wivu mke wangu”
“Wivu lazima, tena sana”
“Haya baby, wangu vipi wewe huojiwi?”
“Hapana, mimi nitasimama nyuma ya kamera zao”
Tukatoka, huku tuomeongozana na Rahma na kuwakuta waandishi wa habari wakiwa wamekaa kwenye viti wakinisubiria, huku kamera zao wakiwa wameziweka tayari za kuchukua kila tukio ambali litakalo tokea eneo hili
“Habari zenu”
Niliwasalimia, na wote wakaitikia kwa furaha.Nikakaa kwenye kiti changu ambapo mbele yake kuna meza ndogo ilio na maji pamoja na glasi, kisha na kuwatazama wote na wakatabasamu kwa mmoja mmoja
“Jamani karibuni, hapa ndio nyumbani kwangu na mpenzi wangu, mahabuba wangu, chocolate wangu, utamu wangu, pumzi yangu, ubavu wangu, chakula changu, mke wangu Rahma”
Maneno yote ya kumsifia mke wangu Rahma yakawafanya waandishi wa habari kupiga makofi kwa furaha
“Yaaa ninamependa sana mke wangu, na popote nikiwa nilazima nimtaje mke wangu kama mtu muhimu sana kwenye maisha yangu, japo hata wengine pia ni muhimu sana kwenye maisha yangu”
“Sasa ninakaribisha maswali”
Akanyoosha kidole muandishi wa habari mmoja na nikampa ruhusa akasimama huku akiwa ameshika kikaratasi kidogo mkononi mwake
“Kwa jina mimi ninaitwa Godwin ninatokea kituo cha habari ITV, kwanza ninashukuru sana bwana Eddy kwa kuweza kutujali na kutupa nafasi ya kuzungumza na sisi waandishi wa haba-ri.Kwana ninapenda kutanguliza pole kwa yale yote ambayo yalikupata, pia hongera kwa kuweza kujitoea kwa hali na mali katika kukuokoa mji wako”
“Swali ambalo ninapenda kukuuliza, ni jinsi gani uliweza kupambana na jola kubwa ambalo ku-sema kweli lilikuwa ni tishio kubwa sana kwa mji pamoja na dunia hii,ASANTE”
Godwin akakaa kwenye kiti chake
“Kwana, asante kwa pole ulizo nipa, nimezipokea.Hata asante pia nimezipokea.Niende kwenye jibu lako, kitu ambacho kilinisaidia ni Mungu tuu kwa maana kwa uwezo wangu wa kibinadamu nisingeweza kufanya kitu cha aina yoyote mbele ya joka hilo”
“Lilikuwa linafananiaje”
Dada mmoja aliniuliza na kuwafanya wezake kumgeukia
“Linatisha na lilikuwa na vichwa kumi na mbili”
“Kabla ya hapa nyuma, ninasikikia ulikuwa unamiliki majini, kuna ukweli wowote katika hilo”
Jamaa mmoja aliniuliza, nikamtazama kwa muda kisha nikamjibu
“Ukweli huo upo, nikweli nilikuwa ninawamiliki majini ila ni kutokana na kurisithwa”
“Ulirisithwa na nani?”
“Nikizungumza watu wengi hamuta amini ila, ndio ukweli wenyewe.Nilirithishwa na mfalme Suleiman”
Waandishi wa habari wakatazama
“Ila mfalme huyo si alifariki kipindi kirefu cha karne za enzi hizo, kabla ya kristo?”
“Ndio, ila yeye mwenyewe alidai kwamba hajafariki, ila watu wengi walizani kwamba amekufa”
“Ulikutana naye wapi?”
“Kwenye moja ya handaki la msitu ambao hadi sasa hivi siujui jina lake”
“Pia niliwahi kusikia kwamba mke wako alibeba ujauzito na kujifungua kiumbe cha ajabu”
Swala lamuandishi huyu wa kiume likanifanya nimtazame Rahma ambaye baada ya macho yetu kuyakutanishwa kwa pamoja akayaiinamisha kichwa chake chini
“Hapana, hakuwahi kubeba ujauzito”
“Kwa habari ambazo zinaendelea huko mtaani, kwamba wewe ulisha kufa siku nyingi?”
“Nani kakuambia?”
Sikujibu swali zaidi ya kumuuliza huyu muandishi wa habari, kwani swali lake limeanza kunikera moyo wangu
“Hii nikutokana na wajibu wa madaktari walio kupokea na kukupima vipimo vyote na kusadikika kwamba wewe ulikuwa mfu”
Nikakaa kimya kama dakika mbili, nikikosa jibu la kujibu
“Bwana Eddy?”
Muandishi mmoja aliiniita na kunifanya ninyanyue sura yangu kumtazama
“Sio kweli, laiti kama ningekuwa mimi ni mfua sidhani kama leo mungekuwa munanihoji, nina-hisi hao madaktari akili zao hazina akili”
“Je nasikia mke wako, alikuwa ni mwanafunzi wako?”
“Nani?”
“Rahma”
“Kwani kua ubaya?”
“Hapana”
“Basi ni ndio”
“Kutokana na kupendwa, sana na kujipatia umaarufu kwa wananchi wako wa mji wa Tanga, je unampango wa kugombania Ubunge kama wananchi wanavyo hitaji?”
“Siipendi siasa, na sidhani kama ninaweza kuwa mbunge”
“Je kuna ukweli wowote kwamba wewe umepandikizwa roho ya nyoka?”
Swali la muandishi huyu wa habari likanifanya niiname chini ya meza kwani nilijikuta nikikasi-rika sana jambo ambalo taratibu nikanza kuhisi mabadiliko kwenye mwili wangu, ubaridi mkali ukaanza kunitawala, huku ukiambatana na mikono yangu kuanza kubadilika jambo lililo anza kuniogopesha

Nikastukia nikifunikiwa na taulo mgongoni, kuangalia vizuri nikamkuta ni Rahma ndio amenifunika na taulo ambalo limelowana maji, kidogo nikaanza kujihisi vizuri hata ubaridi mkali na mabadiliko kwenye mikono yangu vikaanza kuputea taratibu hadi nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida
“Unajisikiaje mume wangu?”
Rahma aliniuliza kwa sauti ya chini ya kunong’oneza sana, ambayo sio rahisi kwa mtu yoyote kusikia
“Nipo powa”
“Twende basi ukapumzike ndani”
“Sawa”
“Jamani wapendwa Mr kidogo hali yake sio nzuri sana, ninawaomba mummpe muda kidogo, na mahojiano yataendelea jioni kwenye tafrija ndogo niliyo waandaliaa”
Rahma alizungumza na waandishi wa habari, taratibu akaninyanyua kwenye kiti, tarataibu tukaanza kuelekea ndani, Rahma kwa utaratibu akanilaza kitandani na kuniwashia feni lililopo pembeni ya kitanda changu
“Eddy vumilia, mume wangu”
“Mbona imekuwa hivi, sielewi?”
“Mume wangu pumzika kwanza nitakujibu baadaye”
Rahma alianza kunibembeleza taratibu, akaniacha na kwenda nje kuendelea na maandalizi ya tafrija fupi aliyo iandaa, nikaanza hihisi harufu ya tofauti ndani ya chumba changu, na taratibu nikaanza kunyanyuka kitandani mwangu, huku nikiongozwa na pua zangu, kunusa ni wapi harufu hiyo inapo tokea.Nikaanza kusikia vikopo vya kuwekea ,afuta vilivyopo bafuni vikianguka,
“Ni nini?”
Nilijiuliza kwa maana ndani kwat hakuna panya wala paka anayeweza kufanya uharibifu kama huo.Nikaendelea kutembea kwa umakini hadi bafuni na kukuta vikopo vyote vya mafuta na sabuni zikiwa chini, harufu nayo sikuihisi ndani mwangu tena.Nikaanza kuokota kimoja baada ya kingine, nikiwa nimeinama nikastukia kuiona miguu ya mwanake nyuma yangu, kupitia kioo kilichopo mbele yangu ikiwa inavuja damu nyingi, nikasimama na kugeuka na kukutana na binti wa miaka kama kumi na nane akiwa anavuja damu mwili mzima
Macho yake ameyatoa kiasi kwamba anaonekana kubanwa na kitu kwenye koo lake,
“Ni…nisa..idie”
Alizingumza kwa shida sana kiasi kwamba nikabaki nikiwa nimeshangaa kwani sikujua ameingiaje ingiaje ndani kwet na istoshe sikujua ni kitu gani kilicho mpata
“Wewe ni nani?”
“Ni…saaa iii..dieee”
Aliendelelea kuzungumza kwa shida sana, nikajaribu kuuinua mkono wangu ili nimpe, nikajihisi uzito mkubwa sana kutoka kwenye mkono wangu
“Ed….ddy nisai…diee”
Nikaanza kuulazimisha mkono wangu wa kulia kunyanyuka ila nikajikuta nikishindwa, kuunyanya na zaidi nikabaki nikiwa nimesimama kama namba moja, Gafla upepo mkali ukaanza kutawala ndani ya bafu na kunirusha na kuniangusha chini.Nikamuona Olvia Hitler akiwa amesimama katikati ya upepo unaozunguka mithili ya kimbunga kikali, gafla nikastukia Olvia Hitler akimvuta binti huyo na kumuingiza katikati ya upepo na kupotea mbele ya macho yangu
“Mmmmm”
Nilibaki nikiwa nimeguna tu kwani sikuelewa kitu kinacho endelea kati ya mtoto huyo na Olvia Hitler ambaye kwa mara ya kwanza nilimuona akiwa katika hali mbaya sana kwenye mwili wake, ila ujio wake wa sasa upo tofauti sana.Nikajinyanyua kwa msaada wa kishika kuta za kioo zilizopo bafuni mwangu, kisha nikaelekea chumbani na kujitupa kitandani
Hadi unafika wakati wa tafrija sikuwa na furaha moyoni mwangu, japo usoni mwangu ninajikaza kutabasamu mbele ya wageni waalikwa, akili yangu yute inakazi ya kumfikiria binti niliye muona bafuni mwangu
“Habari yako kaka Eddy”
Msichana mmoja aliye valia suti nyeusi alizungumza huku akinipa mkono
“Salama tu mambo vipi?”
“Salama tu, Mimi ninaitwa Rejina, nimuandishi wa vitau vya story kama huto jali ninaomba kuzungumza mimi na wewe”
“Sawa, tunaweza kuzungumza”
“Ombi langu kubwa ambalo ninahitaji kukuomba kwako ni kwamba, ninaomba niiandike story ya maisha yako ninaimani kitabu chako kitauza sana”
“Kwa nini umeamua au umependela kuandika kitabu cha maisha yangu na sichawatu wengine?”
“Wewe, umepitia mambo mengi sana kwenye maisha yako japo sisi watu tunatambua machache ila kusema ukweli wewe kama wewe utakuwa na mambo mengi sana ya kuniadisia na mimi nikayaweka kwenye maandishi na kuwa kumbukumbu nzuri hata kwavizazi vijavyo”
“Nipe muda nilifikirie hilo”
“Ila kaka Eddy, kuna kitu nakuona kinakukosesha raha?”
“Hapana, nipo sawa tu”
“Sawa hii ni kadi yangu inanamba za simu ukiwa tayari ninaomba uwasiliane na mimi”
“Poa”
Nikapokea kadi ya mawasiliano ya Regina na akanikumbatia na kuondoka zake, na kuniacha nikiangalia jinsi watu wanavyo sakata mziki, nikaanza kukisoma kikadi alicho nipa Regina na kukuta maandishi ya jina lake na kampuni anayo ifanyia kazi, nikakuta namba zake mbili za simu za mitandao tofauti.Nikakiingiza mfukoni mwangu na kugeuka upende wa kushoto na kumkuta Rahma akiwa amenitazamakwa macho makali, baada ya macho yetu kukutana Rahma akaachia msunyo mkali nakuondoka kwa hasira
“Anataka nini naye huyu?”
Nilijiuliza swali mimi mwenyewe, sikutaka kumfwatilia sana Rahma zaidi ya kumuwazia msichana niliye muona akiniomba msaada bafuni.Nikatafuta kiti nakukaa, wakaja baadhi ya wageni waalikwa wakakaa na mimi na tukaanza kupiga stori za hapa na pale, wengine wakinipongeza kwa kazi niliyo ifanya
Gafla nikamuoma msichana aliye nitokea bafuni akiwa amesimama kwenye geti la kuingialia ndani kwangu,
“Samahani jamani, ninakuja sasa hivi”
“Sawa muheshimiwa”
Nikaanza kunyanyuka na kupita pembezoni mwa bwala la kuogelea walilo jaa baadhi ya wageni waalikwa wakiburudika, sikutaka kuyakwepesha macho yangu sehemu yoyote zaidi ya kumfwata binti aliyepo mbele yangu,huku akiwa katika muonekano wake ule ule wa kuvunjwa na damu mwili mzima.Cha kustaajabisha nikaanza kumuona akiingia ndani, huku akipishana na watu wengine pasipo wao kumuona, nikazidi kuongeza mwendo wa kumfwatilia nikashangaa akielekea kweny vyumba vya chini akiacha kupanda vya ghorofani.
Akaingia kwenye moja ya chumba na mimi nikaingia pasipo kubisha hodi, gafla macho yangu yakakutana na Regina akiwa mtupu kama alivyo zaliwa huku mwili wake ukiwa umejaa maji, akionekana kutoka kuoga, nikatazama kila kona ya chumba na sikumuona binti ambaye nilikuwa ninamfatilia, Regina hakuonekana kushangaa wala hukuficha sehemu zake za siri, zaidi akabaki akiwa ametabamu na kuanza kupiga hatua za kunifwata, gafla nikastukia mlango ukifunguliwa nyuma yangu na nilipo geuka nikakutana na Rahma akiwa anatushangaa


*Eddy ndio unafanya nini hapo?”
Rahma alizungumza huku akinitazama kwa hasira,
“Kwani wifi wewe, unatuona tunafanya nini?”
Regna alimuuliza swali Rahma, ambalo likazidi kumkasirisha Rahma
“Koma wewe, sijazungumza na wewe, nimemuuliza mume wangu”
“Ndio unijibu sasa, umetukuta tumesimama unababaika, ungenikuta nimemuweka kifuani mwangu si ndio un-gekufa”
Regna alizungumza kwa dharau wala sikujua ujasiri kama huu ameutolea wapi, Rahma akanipiga kikumbo, ni-kastukia akimvaa Regna na kumuangusha chini, na kuanza kupigana, nikabaki nikiwa ninashangaa, sikujua hata nifanye kitu gani, Regna akamgeuza Rahma na kumkalia tumboni mwake, na kuanza kumtandika vibao vya ma-shavu, Rahma naye hakubaki nyuma, akajikakamua hadi akafanikiwa kumuweka Regna chini ambaye yupo uchi, na kuanza kunzaba makofi ya hasira.Nikamkimbilia Rahma na kumuwahi mikono yake, na kumchomoa mikono-ni mwa Regna
“Rahma, tulia mke wangu, mbona unataka kuleta aibu kwa wageni waliofika hapa”
Nilizungumza huku nikiendelea kumshikilia Rahma kwa nguvu
“Niache nimkomeshe huyo malaya wako”
Rahma alizungumza huku akijikakamua kutoka mikononi mwangu
“Malaya mwenyewe, hivi unadhani utaweza kuwa peke yako, na ninakuambia ni lazima nimchukue huyo mume wako, kwanza mwanamke mwenyewe huna kizazi, unadhani mume wako ataendelea kukaa na mwanamke tasa kama wewe? Uyooooo”
Maneno ya Regna yalizidi kunishangaza kwa maana si kawaida ya mtu anaye jitambua kuzungumza mambo ka-ma hayo
“Eddy niachie, nimfundishe adabu huyu malaya, hawezi kunvunjia adabu ndani ya nyumba yangu”
“Rahma tulia, ninakuomba utulie mke wangu”
“Unamtetea huyo malaya wako eheee, niache sasa”
Nikastukia Rahma akinipiga kisukusuku cha tumbo na kujikuta nikimuachia, akamvamia Regna na kumuangu-sha chini, kwa haraka nikafunga mlango, kuepuka watu wa nje kusikia kitu kinacho endelea ndani ya chum-ba.Rahma akazishika nywele nyingi za Regna na kuanza kukibamiza kichwe chake kwenye kwenye sakavu yetu ya kisasa, Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kumuona damu zikiwa zinasambaa chini, zikitoea kwenye kichwa cha Regna.Kwa haraka nikavuta Rahma kwa nguvu zangu zote na kumzuia kuendelea kumpigiza Regna kichwa chake chini
“Achaa,”
Nilizungumza huku nikimbeba juu juu Rahma na kukandamiza ukutani, tangu nianze kumjua Rahma sikuwahi kumuona akiwa na hasira kiasi hichi, Nikaendelea kumkandamiza Rahma ukutani, tukiwa tunatazama kwa ma-cho makali, kidogo hasira yake ikaanza kumtulia.Nikageuka nyuma na kumtazama Regna nikakuta akiwa ametu-lia kimya huku damu zikiendelea kusambaa kwenye sakafu, nikamfwata kwa haraka sehemu aliyo lala na kuki-weka kiganja vhangu kifuani mwake na kukuta mapigo yake ya moyo yakiwa yametulia kimya, nikazidi kuchan-ganyikiwa
“Ameshakufa”
Nilizungumza huku nikimtazama Rahma ambaye mwili wake wote unamtetemeka kwa woga
“Rahma umeua”
Niliendelea kuzungumza huku nikimpima mapigo ya moyo Regna ila hapakuwa na msukumo wowote, wa mapi-go ya moyo ulio endelea kwenye kwenye kifua chake, Nikasikia mlango ukigonjwa kwa nje ikiashiria kuna mtu anahitaji kuingia ndani ya chumba hichi
Tukatazamana na Rahma, na hakuna aliye yanyua kinywa chake kusikilizia hodi inayo gongwa, mtu anaye ene-delea kugonga mlango kama dakika tatu hivi kisha akaanza kuita jina
“Regna mke wangu fungua mlango, kuvaa gani masaa kumi”
Ilikuwa ni sauti ya kiume ambayo, ilizidi kuniogopesha, nikapeleka macho yangu kwenye mkono wa kushoto wa Regna na kukuta akiwa amevaa pete ya ndoa akiashiria ni mke halali na huyo anaye gonga mlango
“Wewe mwanamke mimi naondoka zangu, saa utakodi bajaji, nakwenda zangu home kulala muda umesha kwenda”
Jamaa alizungumza na kuzidi kutuchanganya akilia mimi na Rahma, Rahma akataka kuzungumza ila nikawahi kukiweka kidole changu kimoja mdomoni mwangu nikimuashiria kukaa kimya na asizungumze jambo la aina yoyoye.Nikasimama na kwenda kusimama mlangoni na kuliweka sikio langu kwenye mlango na kusikilizia kama jamaa atakua ameondoka.Nikastushwa na mlango kugongwa, tena kwa nguvu
“Wewe mama Junio, hunisikii humo ndani, au mimi ninaondoka”
Nikameza fumba jingi la mate na kubaki nikimtazama Rahma, ambaye sura yake yote imejaa machozi mengi, akijilaumu kwa kitu alicho kifanya.Nikasikia miguu ya mtu akija, na kusimama kwenye mlango
“Afande Denis mbona hapa?”
“Ahaaa si huyu wifi yeko ameingia humu kutoka, hatoke aliniambia kwamba amekuja kubadilisha nguo”
“Alaa labda ameshatoka, na kama nimepishana naye kule kwenye bustani anakutafuta wewe”
“Ahaaa, atakuwa ametoka saa ngapi?”
“Mpigie simu?”
“Simu yake imezima chaji na ninayo mimi”
“Hembu kamcheki kwenye bustani kule”
“Sawa”
Nikasikia miguu ya watu hao ikiondoka nje ya malango jambo lililo anza kunichanganya na kuhisi kwamba kuna mauza uza yanaendelea kwenye hii nyumba yangu
“Ngoja nakwenda nje mara moja, kaa humu ndani na ufunge mlango kwa nje sawa”
“Unakwenda wapi mume wangu?”
Rahma alizungumza huku akinyanyuka, kutoka sehemu alipokuwa amekaa
“Nimekuambia kaa humu ndani kuna kiitu ninakwenda kukitazama nje sawa”
“Unaniacha peke yangu, humu ndani na hii maiti?”
“Nimekuambia, kaa humu sawa”
Ilinibidi nizungumze kwa ukali kidogo na kumfanya Rahma kustuka na kubaki akiwa amesimama
“Funga mlango kwa ndani na usimfungulie mtu wa aina yoyota zaidi yangu sawa”
Rahma alinijibu huku akitingisha kichwa akionekana kunielewa na kukubaliana na mimi kishingo upande.Nikafungua mlango taratibu na kuchungulia kwenye kordo, sikuona mtu yoyote
“Funga sasa”
Nikatoka haraka, na kumuacha Rahma akifunga kwa ndani, nikapiga hatua za haraka kuelekea nje kwenye bus-tani, nikasimama sehemu ambayo nitaweza kuwaona watu wote waliopo kwenye bustani, ila sikumuona Regna wala mume wake
“Kaka Eddy unatafuta nini?”
Jamaa mmoja aliniuliza baada ya kuniona nikiwa ninapepesa macho yangu kila kona ya bustani yangu
“Kuna dada, hivi ni muandishi wa habari sijui unemuona?”
“Yupoje yupoje”
“Mrefu, kiasi na mwembamba fulani?”
“Huyo atakuwa ni Regna?”
“Eheee huyo huyo”
“Nimemuona akielekea kwenye parking za magari”
“Asante”
Nikaachana na jamaa na kuanza kupiga hatua za kwenda kwenye maegesho ya magari, nikakutana na gari moja aina ya Vitz, ikasimama pembeni yangu na kioo cha gari hilo kikashushwa
“Kaka Eddy, nilikuwa ninakutafuta nikuage”
Sauti ya jamaa ndio sauti ya jamaa aliyekuwa akigonga mlangoni, akimuita mke wake, nikabaki nikishangaa baada ya mlango wa upende wa pili wa dereva ukifunguliwa na akashuka Regna akiwa amevalia kama alivyo kuja kuniomba mara ya kwanza juu ya kuhitaji kuandika story ya kitabu kinacho husu maisha yangu
“Kaka Eddy, niagie kwa wifi yangu, na ile ishu ya story ninakuomba usisahau”
Regna alizungumza na kunifanya nibaki nikiwa nimemtazama kwa mshangao, nikashindwa hata cha kuwajibu
“Eddy, kaka Eddy”
Jamaa aliniita na kunifanya nistuke kwenye bumbuazi ambalo limenikamata gafla
“Yaaaa, sinto sahau”
“Sawa, ngoja sisi tukapumzike”
“Haya usiku mwema jamani”
Regna akanipungia mkono na kuingia ndani ya gari, wakaondoka na mume wake, nikashusha pumzi nyingi na kubaki nikiwa ninaisindikiza gari yao kwa macho hadi inatoka getini, gafla nikasikia kelele kubwa iliyo nistua na kunifanya nigeuke kuangalia walipo watu, nikawashuhudia wageni waalikwa wakikimbilia ndani inapo tokea kelele hiyo
Na mimi nikaanza kuchanganya miguu yangu kwa kasi kwenda kutazama ni kitu gani kinacho endelea ndani ya nyumba yangu.Jinsi ninavyozidi kwenda ndani ndivyo jinsi kelele ilivyozidi kuingia kwenye masikio yangu, nika-zidi kuchanganyikiwa kwani kelele hiyo ni sauti ya Rahma ikitokea kwenye chumba ambacho nimemuacha na maiti, nikakuta watu wakiwa wamekushanyika nje ya mlango wa chumba nilicho muacha Rahma,
Nikawaomba wanipishe njia, na wakafanyahivyo hadi nikafika kwenye mlango, nikaanza kugongwa kwa nguvu ulu nikiliita jina la Rahma, gafla moshi mwingi ukaanza kutoka chini ya mlango, ulio anza kutupalia watu wote tuliopo kwenye eneo hili la mlango

Moshi mwingi ukazidi kutoka ndani ya chumba alichopo mke wangu Rahma, ambaye hadi sasa hivi anapiga kekelele za kuomba msaada, nikajitaidi kuibana pumzi yangu, nisiendelee kuuvuta moshi unaotoka kwenye chumba alichopo Rahma na kuanza kuubamiza mlango kwa kutumia bega langu la mkono wangu wa kushoto, kwa nguvu zangu zote.Kelele za Rahma zikazidi kunichanganya kiasi cha kujikuta nikizidisha juhudi za kuuvunja mlango kwa kutumia nguvu zangu zote.Wanaume wezangu wakaanza kunisaidia kufanya kitendo ninacho kifanya mimi, cha kumshukuru Mungu, mlango ukavunjika na sote tukajikuta tukianguka nao baada ya kuurukia kwa nguvu zetu zote, Moshi mwingi tukakumbana nao, ulio ambatana na moto mwingi, nikamshuhudia msichana aliyekuwa amepigwa na Rahma akipotelea kwenye moshi mwingi ndani ya chumba, wezangu hawakumuona zaidi yangu
Nikakimbilia sehemu alipo Rahma na kumkuta akiwa amelala chini, huku hajitambui,
“Rahma, Rahma”
Nilimuita ila hakuitika zaidi ya kuendelea kuyafumba macho yake, tukasaidiana na wezangu kumnyanyua Rahma na kumtoa nje kwa haraka na kuanza kumpa huduma ya kwanza, rahaya ya sherehe ikanipotea kabisa na kuwa ni majanga mengine ambayo sikuyatarajia kama yatatokea katika siku hii ya leo, watu wengine wakaendelea kuuzima moto uiopo ndani ya chumba ambao hadi sasa hivi chanzo chake ni nini.Hali ya Rahma ikazidi kuwa mbaya kwani mapigo yake moyo yamekuwa ya kuhesabika na ndani ya dakika moja yanaweza kupiga mara tano au saba, ni tofauti na mapigo yamoyo yanavyopaswa kupiga kwa binadamu wa kawaida.Jamaa mmoja akajitolea gari lake, tukamuingiza Rahma ndani ya gari na kumuwahisha katika hospitali ya mkoa ijulikanayo kwa jina la Bombo.Akili na mwili vyote vimechoka kwa muda mmoja, kila daktari ambaye anatoka kwenye chumba anacho ingizwa mke wangu sikusita kumzuia na kumuuliza hali ya Rahma inaendeleaje ila hawakunipa jibu la kueleweka
“Mungu wangu”
Nilijikuta nikianza kumkumbuka Mungu, kadri muda ulivyo zidi kwenda, ndivyo idadi ya madaktari walivyozidi kuingia na kutoka katika chumba alichopo Rahma.
“Kaka Eddy jikaze atapona tuu shemeji”
Jamaa mmoja alizungumza kunifariji, masaa yakazidi kuyoyoma na saa yangu ya mkononi inaonyesha ni saa tisa usiku na hapakuwa na na jibu lolote la kunipa matumaini juu ya mke wangu.Akatoka daktari mmoja, mzee wa makamo, akaniomba tuelekee ofisini kwake, kuna baadhui ya marafiki zangu wakataka kutufwata ila daktari akawazuida.Tukaingia ofisini mwa daktari na kuniomba nikae kwenye moja ya kiti kati ya viti vitatu vilivyomo ndani ya ofosi yake, akafungua ndirisha kuruhusu hewa kuingia ndani
“Dokta usinitumbulie mimacho, niambie ukweli hali ya mke wangu inaendeleaje?”
“Tulia Mr Eddy, kwanza mke wako amepatwa na tatizo gani?”
Haaa dokta unaniuliza tena mimi, wakati nyinyi ndio munapaswa kujua mke wangu amepatwa na tatizo gani?”
“Hapana usinielewe vibaya Mr Eddy, kwa maana, mke wako amepatwa na ugojwa ambao tangu niaanze kufanya kazi huu ni mwaka wa thelethini, ila sijawahi kuuona huo ugonjwa”
Maneno ya daktari yakazidi kunichanganya akili yangu, nikaendelea kumtazama daktari kwa macho makali ambayo
“Labda niende kwe….”
Kabla dokta hajamalizia akaingia nesi akiwa ameshika, bahasha kubwa yenye rangi ya kaki na kumkabithi daktari
“Mumezipiga vizuri?”
“Ndio dokta”
Nesi akanondoka na daktari akachomoa picha, iliyo pigwa na mionzi mikali ijulikanayo y kwa jina la ‘X-RAYS’.Akaitazama na kunikabathi mimi na nikaanza kuiangalia pasipo kuielewa kwani kwa jinsi ilivyo pigwa sikujua imepigwa pigwa vipi
“Ndio nini, hii doktar?”
“Hiyo ni picha niliyo iliyo pigwa kwenye mwili wa mke wako, na chakushangaza hatujaona mfupa hata mmojamwilini mwake, jambo ambalo hata sisi tlimetuchanganya”
“Hamujaona mfupa?”
“Ndio atujaona mfapa kwa maana, hata fuvu la ndani, kwa mke wako hatujaliona, tulihisi ni vifaa vyetu ndivyo vimekosea, ila nikajaribu kupiga tena na majibu ya picha zote zipo kama hivyo”
Doktar alizungumza huku akitoa picha nyingine nne ambazo zinafanana na pica niliyo ishika mkononi mwangu.Kwa kawaida binadamu akipigwa picha ya X-Rays nilazima aonekane na mifupa ndani, ila sivyo ilivyo kwa Rahma, mwili wake mzima umejaa nyama tupu
Gafla mlango ukafunguliwa kwa haraka na kuingia daktari mwengine akivunjwa na damu
“Dokta tunakuhitaji haraka”
Alizungumza na kutoka ndani ya chumba, daktari akasimama na kufungua mlango na kutoka kwa kasi, na mimi nikapiga hatua za haraka kwenda kufungua mlango ila kabla sijaufungua nikasikia sauti ya kike ikiniita kikitokea dirishani.Nikageuka na kutazama dirishani na kumkuta Regina akiwa ananichekea na kunitazama kwa macho ya dharau
“Unaona hichi kichupa, ndio dawa utakayo mtibu mke wako la sivyo utampoteza”
Regna alinionyesha kichupa chenye maji ya rangi ya kijani na kunifanya nihairishe safari yakwenda alipo mke wangu na kunifanya nitokee dirishani ambalo ni lavioo na halina nondo, ambayo inaweza kunizuia.Ragina akaanza kukimbilia kwenye majengo mengine ya hospitalini na kunifanya nianze kumfukuza kwa haraka, kitu kilicho niacha hoi ni spidi kali anayo kimbilia Regna na kila ninavyo jitahidi kumkimbiza ndivyo jinsi alivyozidi kuchanganya miguu na kuniacha umbali mrefu kiasi.Nikamshuhudia Regina akiingia kwenye moja ya jengo, ambalo sikulisoma jina lake vizuri, kabla sijaingia ikanilazimu kurusdi nyuma hatau chache kuangalia maandishi makubwa yaliyo andikwa kwa herufi kubwa zilizo kolezwa kwa ramgi nyeusi
(JENGO LA KUHIFADHIA MAITI, MOCHWARY)
Sikutaka kuendele kutazama maandishi mengine kwani yatanipotezea muda, nikaisikia sauti ya Regina ikiniita ndani ya chumba hicho na kunifanya niingie pasipo kuogopa, nikamkuta akiwa amesisima mbali kidogo kwenye kordo na katika pende mbili, hizi kuna mafriji makubwa ya kuhifadhia maiti.
“Njoo ukichukue kichupa, ukamuokoe mke wako mpendwa”
Regina alizungumza kwa ujasiri huku, akiendelea kuniringishia kichupa alicho kishika.Nikaanza kupiga hatua za haraka kwenda alipo sima, Regna akapiga kofi moja na taa zote, zikazima na giza totoro likatawala ndani ya chumba na kuanza kunichanganya, kwani sikumuona sehemu alipo simama
“Eddy”
Nilisikia sauti ikiniita nyuma yangu, nikageuka haraka ila kutokana na giza sikumuona mti yoyoye,
“Eddy”
Nikasikia sauti ukiniita upande wangu wa kulia na kunifanya nigeuke kwa haraka huku nikitazama ni wapi alipo Regina.Akaanza kucheka vicheko vikali, nikasikia mlango ukijifunga kwa nguvu, na kelele za watu kucheka zikazidi kuongezeka ndani ya chumba nilichopo.
“Shiiiiii”
Nikasikia sauti ya Regina ikiwanyamazisha wezake anao cheka nao, na wakanyamaza, gafla taa zikawaka na kumkuta Ragina akiwa amesimama mbali kidogo na nilipo mimi, huku pembeni yake kukiwa na wasichana wengine wawili wakifanana naye kwa kila kitu
“Eddy nani unampenda kati yetu”
“Nisikilize wewe, mwanamke naomba hicho kichupa nikamponye mke wangu”
Nilizungumza kwa ujasiri huku nikiwa nimejikaza, kisabuni
“Ohoooo, Eddy unajua mke wako alicho kifanya kwetu?”
“Najua hujui, ila ukweli ni kwamba mke wetu alikuja kwetu na kutuomba tuweze kukurudisha wewe duniani, tukampa masharti ambayo alishindwa kukuambia, na muda wa mashati hayo umepita, sasa ni kipindi cha yeye kupata shida”
“Ni masharti gani mulimpa?”
“Swali zuri sana, kwanza jitambua kwamba wewe tayari ulisha kufa, pili hiyo pumzi sisi tumekupatia udumu dumu nayo kwa muda tu ila utakufa pia”
Naweza kuwaita maregina kwani, wanazungumza kwa kupokezana akimaliza huyu anazungumza mwengine kwa sauti zinazo fanana
“Niambieni hayo masharti mimi, niyafanye”
“Hhaahaaaa Eddy, acha kutuchekesha, unadhani ytayaweza masharti yetu”
“Niambieni, kwani nahitaji mke wangu apone”
“Hahaaaa, mke wako ni mjinga sana”
Regina mmoja alizungumza huku akinisogelea karibu na kuanza kunizunguka taratibu, huku mkono wake mmoja akikishika kiuno changu.
“Tulimuambia mke wako, baada ya siku thelethini ya wewe kuwa hai, tunataka ule watu watano kama sadaka ya kumshukuru Mungu wetu, ambaye yupo India, na siku ya Thelathini ilikuwa ni jana, ndio maana ukaanza kubadiila kuwa joka, ila mke wako alikuzuia, na ukashindwa kubadilika.Tulitaka uwatafune wale waandishi wa habari waliokuwa mbele yako, ila ndio hivyo tena ikashindika”
Maneno ya Regina yakazidi kunivunja nguvu, nikabaki nikiwa ninamtazama pasipo kumjibu kitu chochote.
“Na mke wako alivyo mjinga akadhubutu kunipiga, ulidhani alikuwa akinipiga kwa kunionea wivu, la hasha, ila alikua akinipiga akihitaji nife ila masharti yavunjike ndio maana na mimi nikaamua kumumpa ungonjwa ambao hata madaktarti wamtibu wakiwa wapo uchi, hawataweza kumponya na tunampa nusu saa, pasipo wewe kutekeleza tutakacho kuambia basi mke wako, ATAKUFA”
Regina alizungumza na kuanza kucheka huku akirudi sehemu walipo simama wezake, mwili mzima ulianza kunivuja kwa jasho , japo ndani ya hili jengo kuna hewe ya baridi ila haikufua dafu katika kulizuia jasho langu kunimwagika sana.
“Nipo tayari kwa masharti yenu”
“Waooooo, powa baby’s tuanzeni kazi”
Regina na wezake wakaanza kufungua friji moja baada ya nyingine na kutoa maiti zilizo pata ajali tofauti tofauti, zipatazo tisa nakuziweka mbele yangu.
“Unadakika kumi na tano kuzili maiti hizi zote uzimalieze”
“Eheee……!!!??”
“Unashangaa, tena tumekupungizia adhabu mbona”
“Naona anataka kumuwekee na vikorombezo ili aweze kuzila vizuri”
Regina mmoja alizungumza na kuanza kuishika maiti moja baada ya nyingine na ndani ya dakika moja zote zikawa zinatoa vunza wengi wakubwa wakubwa, walio nona pamoja na ujiuji mzito
“Hapo kuna mchuzi mzuri wa kukuwezesha kula hizo maiti”
Nikabaki nikizitazama maiti za watu, hawa, kumbukumbu za mke wangu Rahma zikaanza kunijia kichwani kwangu kwa kasi kubwa hadi nikaanz akujishangaa, nikaanza kukumbuka kila aliyokuwa akinifanyia ambayo nimema kwangu.
“Eddy, muda unakwenda”
Regina mmoja alizungumza na kunifanya nipige magoti chini na kuanza kuchukua maiti moja na kuanza kuinyafuafua nyama zake, na kadri nilivyo zidi kuitafuna ndivyo mwili wangu ilivyo anza kubadilika na kuwa katika mfumo wa joka, kasi ya kuzitafuna ikazidi kuongezeka kwani Regina mmoja alikuwa na kazi ya kuniambia muda uilio badilika.Hadi inafika dakika ya kumi na tano nikawa nimeshamaliza kumla maiti wa tisa, na kurudi katika hali yangu ya kawaida ya kibidanamu huku mdomo wangu mzima ukiwa umejaa damu tupu
“Waoooo kazi nzuri Eddy, ila kuna mmoja wa mwisho wa kumalizia, huyo ni mtamu sana kuliko hao wote”
Regina alizungumza huku akilisogelea friji moja na kulivuta nje, na kwakusaidiana na wezake, wakautoa mwili ambao hadi wanauweka chini nikabaki nikiwa ninashangaa kwani ni mwili wangu wote.
“Huyu ni wewe, halisi baada ya kufa wakakuleta huku ila wamejisahau na kujua wewe upo hai”
Regina alizungumza huku akiugeuza mwili wangu, ambao hauna nguo hata moja, nikaliona jeraha la kisiki kilichokuwa kimenichoma mgongoni, kipindi mkia wa joka kubwa ulivyokuwa limenipiga na kunirusha juu na kukiangukia kisiki hicho
“Jile mwenyewe, sasa au unataka tukuwekee rost kama la wengine ulio wala?”

Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama, Regina na wezake anao fanana nao.
“Moja, mbili, ta…..”
“Ngoja kwanza Regina”
“Ehee unsemaje?”
“Ninakuomba umsaidie mke wangu, hapa nilipo sijielewi kabisa, tafadhali ninakuomba ndugu yangu”
Regina wote watatu wakaanza kucheka kwa dharau huku wakianza kunizunguka kwa kasi sehemu ambayo ni-mechuchumaa na mwili wangu, ninaoa ambiwa niule.Wakasimama gafla huku macho yao na sura zao zikianza kubadilika, macho yao yamejaa miale ya moto iliyo ambatana na machozi ya damu, huku sura zao zikianza kusi-nyaa na kuwa nyeusi tii kama mkaa.
“KULAAAA”
Regina mmoja alizungumza na kunifanya niitazame maiti ya mwili wangu, nikajikuta nikisimama kiujasiri huku nikiwatazama Regina wote watatu, nikamtazama aliye shika kichupa chenye dawa, wakendelea kunitazama ki-sha nikachuchumaa chuni, na kuishika miguu ya maiti yangu, nikaibana vizuri kwa viganja vyangu, kwa kutumia nguvu zangu zote nikainyanyua haraka na kuizungusha, ikawapiga kwenye miguu yao na wote wakaanguka chi-ni, aliye shika kichupa chenye dawa akakiangushia karibu yangu.Nikajirusha kwa haraka na kukiokota kichupa, na kuanza kukimbia kuelekea nje, kabla sijafika mlangoni nikastukia kumuona Regina mmoja akiwa amesimama mbele yangu.Huku sura yake ikiwa imekasirika sana, akajaribu kunirukia ila nikamkwepa na kunipa nafasi ya kutoka nikiwa ninakimbia kuelekea kwenye jingo alipo mke wangu Rahma.Hata mimi mwenyewe nikaanza kuji-shangaa kwa maana mwendo wangu wa kukimbia upo kasi sana, kuwazidi wao, nikafika kwenye mlango wa kuingilia kwenye jengo alipo ingizwa Rahma, Regina na wezake wakasimama na kuninyooshea kidole, huku mmoja akinifanyia ishara ya kunichinja kichwa change.Nikatoa kitambaa mfukoni mwangu na kujifuta damu zi-lizopo mdomoni mwangu
Nikaanza kupiga hatua za haraka kwenda kilipo chumba, kitendo cha kujitokeza kwenye kona nikamkuta dada mmoja ambaye tulifika naye hapa hospitalini kipindi tunamleta Rahma, nikamkuta akiwa amekaaa chini huku analia kwa nguvu, huku baadhi ya rafiki zangu wakiwa, wanajifuta machozi kwa vitambaa vyao.Wasiwasi mwin-gi ukaanza kunijaa moyoni mwangu, nikaanza kupiga hatua za haraka, na kujikuta zikichanganya na kuzaa mwendo wa kukimbia hadi nikafika kwenye mlamgo wa chumba alichopo Rahma, sikumuuliza mtu zaidi ya ku-shika kitasa, nikafungua mlango na kukuta chumba kikiwa hakina mtu hata mmoja, mapigo ya moyo yakazidi kwenda mbio, nikatoka nje huku machozi yakianza kunilenga lenga
“Y..uuu..po wapi mke wangu?”
Niliuliza kwa kigugumizi kikubwa, na kuwafanya rafiki zangu, kuzidi kulia, hakuna ambaye aliweza kunijibu kitu cha aina yoyote.
“YUPO WAPI MKE WANGU”
Nilizungumza kwa sauti kubwa iliyo changanyikana na hasira kali sana, huku nikimshika rafiki yangu mmoja na kukandamiza ukutani
“Ame…”
Jamaa alichindwa kuimalizia sentesi yake, na kujikuta akimwagikwa na machozi mfululizo, moyo wa uchungu ulio amba-tana na machozi yenye hasira ndani yake, vikautawala mwili wangu.Nikaanza kupiga hataua za kuelekea ilipo ofisi ya dak-teri aliye niita mara ya kwanza, kabla sijafika ofisini mwake, nikawaona manesi wa ne wakisukuma kitanda kimoja, amba-cho juu yake amelala mtu aliye funikwa kwa shuka la kijani, kuanzia miguuni hadi kichwani mwake.Nikahairisha safari, na kuanza kukimbilia kwenda walipo manesi.Mmoja wao akaniwahi kunizuia nisikifikie kitanda, ila nikamsukuma na akaan-gukia pembeni na kuwafanya wezake kubaki wakiwa hawana la kufanya
Nikalishika shuka na kulifunua na kukuta maiti ya bibi mmoja mzee akiwa tayari amesha fariki dunia, nikabaki nikiwa ni-nashangaa sana.
“Kwani kaka vipi?”
Nesi mmoja aliniuliza
“Mke wangu yupo wapi?”
“Mke wako, anaitwa nani?”
“Anaitwa mke wangu”
Hata jina la Rahma nililisahau kichwani mwangu kwa jinsi nilivyo changanyikiwa, nikaachana na manesi na kuendelea na safari yangu kwenye ofisi ya madaktari, nikazidi kutembea kwa haraka hadi ninafika nje ya ofisi nikakutana na daktari aki-toka huku akiwa amechoka
“Doktar mke wangu yupo wapi?”
“Tulia kwanza bwana Eddy”
“Doktar hivi unielewi nimekuambia mke wangu yupo wapi, kama amefariki ninaomba munionyeshe maiti yake”
“Bwana Eddy tafadhali ninakuomba utilize jazba kwanz…”
Sikumruhusu daktari kuimalizia sentesi yake, nikalishika koti lake sehemu ya kifua na kumgandamiza ukutani
“Mke wangu yupo wapi?”
Nilizungumza kwa sauti nzito na kumfanya daktari kuanza kutetemeka, mwili mzima, hata miwani aliyo ivaa ikaanguka chini.
“Tumeshiindwa kuuuu…okoa maisha ya mke hadi ametutoka duniani”
Taarifa ya daktari ikanistua sana na kujikuta nikumuachia, mwili mzima ukahisi umepatwa na mstuko kama nilio upata siku ya kifo cha wazazi wangu walipo kufa shambani, machozi yakazidi kunitiririka mfululizo na kujikuta nikiwa nimekaa kwenye benchi lililopo pembeni ya mlango wa kuingilia kwenye ofisi ya daktari.
“Eddy tulijitahidi kadri ya uwezo wetu kuyaokoa maisha ya mke wako ila tukashindwa”
“Pia mke wako alituomba sana tukutafute, azungumze maneno ya mwisho na wewe ila hatukuona, na hatukujua ni wapi alipo”
Maneno ya daktari wala sikuyatilia msisitizo zaidi ya kuyatazama machozi yangu yanayo mwagika chini, kwenye sakafu.
“Mwili wake upo wapi?”
“Tuliupeleka mochwari”
“Twende ukanionyeshe”
“Labda asubuhi, kwa sasa ni ngumu kwenda mochari”
“Twende ukanionyeshe sawa”
Nilizungumza kwa msisitizo, hadi daktari akanijibu kwa kutingisha kichwa chake, akiashiria kukubaliana na mimi kwa kitu ambacho nimekizungumza.Nikanyanyuka kwenye benchi na kumshika mkono daktari na kumtanguliza mbele, akatoa si-mu yake mfukoni na kupiga sikujua anazungumza na nani
“Wee Merry maiti ya mgonjwa mumeiweka wapi?”
“Sanduku namba”
“Ahaa sawa, tangulia mochwar sisi tunakuja”
Akakata simu na kuidumbukiza kwenye mfuko wake wa koti alilo livaa, tukazidi kupigahatua za haraka hadi kwenye jengo la kuhifadhia maiti, nililo toka muda mchache ulio pita.Nikakuta nesi wawili wakiwa wamesimama nje ya mlango wa chumba cha maiti pamoja na mzee mmoja aliye valia mavazi meusi mkononi mwake akiwa ameshika jitochi kubwa
“Mbona kunagiza?”
“Daktari aliuliza?”
“Umeme umekatika, kuna shoti imetokea muda mchache ulio pita”
Mzee alijubu
“Ila maiti ya yule msichana muliiweka?”
“Ndio, tuliiweka”
Nesi mmoja alijibu, macho yangu yakatazama pande zote za eneo la jumba la kuhufadhia maiti, nilipo ridhika kwamba kina Regina hawapo, nikaanza kutangulia kuingia ndani
“Ahaaa wewe kaka subiri mlizi atangulie na tochi”
Nesi mmoja alizungumza huku akiniwahi kunishika mkono
“Giza halina maana mbele ya mke wangu”
Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikiutoa mkono wa nesi ulio nishika, mlinzi ambaye ndio yule mzee aliye valia nguo nyeusi, akafwatia kwa nyuma huku akimulika mulika kwenye madroo ya sehemu zilipo hifadhiwa maiti.
“Muliseme droo namba ngapi?”
Daktari aliuliza
“D-210 ipo kule mwisho”
Tukaelekea sehemu zilip droo, aliyo zungumza nesi, katika sehemu ambayo muda mchache nilikuwa na kina Regina haina uchafu wa aina yoyote na haionyeshi kama kuna tukio lolote lilifanyika siku hiyo.Mlizi akavuta droo alilo alekezwa na ma-nesi hawa, ambao ninashangaa wana ujasiri mkubwa kama wanaume.Macho yetu tote yakatua kwenye sura ya binti mmo-ja ambaye sote hatukumtambua
“Mmmm”
Nilisikia mguno mmoja ukitoka kwa nesi aliye alekeza sehemu alipo tuagiza tufungue droo
“Nini?”
Doktar aliuliza kwa mashangao
“Mbona siye?”
“Muna uhakika mumemuweka humu?”
“Dokta sisi tunauhakika tumemuweka humu, si yule dada wa kiharabu?”
“Ndio, au mumekosea?”
“Dokta hatujakosea, mimi ndio nilikuwa mtu wa mwisho kulisukuma hili droo, au mlinzi ninakosea”
“Kweli hata mimi mwenye ninashangaa”
“Sikieni nyinyi musiniletee ujinga mke wangu, yupo wapi?”
“Kweli kaka yangu mkeo tulimuweka huku”
Gafla tukasikia mtikisiko wa kabati moja lililopo upande wa pili, sote tukakaa kimya, mtikisiko huo upo kama kuna mtu aliye zinduka kutoka katika usingizi mzito na kujikuta yupo ndani ya eneo hilo.
“Shiii”
Niliwaonya wasizungumze chochote, nikaanza kupig ahatua za kuelekea lilipo sanduku alinali kurupuka, nikawatazama daktari na wezake kila mmoja akaonekana kuwa katika hali ya mshangao, huku mlizi mikono yake ikitetemea hadi tochi aliyo ishika mwanga wake ukaanza kucheza cheza.Nikafika kwenye droo, kabla sikaulifungua moshi ukaanza kutoka kwenye droo hilo, huku likizidi kutetemeka.
Kwa ujasiri mkubwa nikaupeleka mkono wangu hadi kilipo kishikizo cha kisanduku, na kulivuta taratibu, kabla sijamalizia kulifungua, nikastukia kitu kikianguka nyuma, ilanilazimu kugeuka haraka na kukuta tochi ya mlinzi ikiwa imeanguka na kusababisha mwanga wake kupiga katika sehemu nilipo simama huku ukitokea chini.Macho ya daktari na manesi yakaanza kushangaa sana
“Nini mbona munashangaa?”
Niliwauliza baada ya kuona mshangao wao unazidi, kidole kimoja cha nesi mmoja kikaniashiria nigeuke nyuma yangu kuangalia kitu kinacho toka kwenye droo nililo lifungua.Nikageuka kwa haraka, sikuamini macho yangu, hii ni baada ya kukutana na mtu niliye fanana naye kuanzia juu hadi chini, isitoshe nguo zake na zangu zimefanana sana, jambo lililo nistua kupita maelezo.Akaanza kupiga chafya nyingi, nikastukia kishindo nyuma yangu, nikageuka na kumkuta nesi mmoja akiwa ameanguka na kupoteza fahamu huku mlinzi naye akifwatiakuanguka na kukaa kimya
“Mambo Eddy”

Jamaa alinisalimia, na sauti yangu inafanana sana na sauti yangu, nikabaki mdomo wazi nisijue nini nimjibu


Jamaa akatoka kwenye droo ya kuhifadhia maiti na kusimama karibu yangu, mwili mzimwa ukaanza kunitetemeka kwa maana katika maisha yangu sijawahi kukutana na vihoja kama hivi japo kuna matukio mengi ya kutisha yalisha wahi kupita kipindi cha nyuma ila la mtu anaye fanana na mimi kwangu limekuwa ni laajabu sana
“Usishangae sana”
Alizungumza huku akielekea walipo simama dokakta na nesi, akawatazama mlinzi na nesi ambao wamepoteza fahamu ki-sha akaachia tabasamu pana kidogo
“Hawa nao kilicho waangusha ni nini?”
Swali lake hapakuwa na mtu aliye lijibu zaidi ya sisi sote kubaki kimya tukimtazama, akachuchumaa na kumshika mlizi kichwani, gafla mlinzi akaanza kutoa chafya zilizo pelekea akazinduka na kukaa kitako na macho ya mlinzi yakabaki kuwa na mshanga kati yangu na Eddy mwenzangu.Macho yangu yakatua kwenye suruali ya dokta na kukuta ikiwa imelowa maeneo ya mbele, ikiashiria ameshindwa kuibana haja yake ndogo kutokana na woga wa kukutanan na jamaa.Akamshika nesi kama alivyo fanya kwa mlinzi na neshi fahamu zikamrejea na kuzinduka.
“Ninaamini nyinyi nyote mutakuwa munashangaa kwa nini mimi nipo hivi, jina langu ninaitwa Eddy ni pacha wa Eddy yule pale”
Eddy alizungumza huku akiwatazama manesi, akangeukia kisha akamshika bega dokata ambaye hadi sasa hivi mwili wake wote namtetemeka mithili ya mtu aliye pigwa shoti
“Mzee usiogope sana, mimi sio mtu mbaya, ila kazi yangu ni moja tu.Nimekuja kumsaidia Eddy katika swala zima la ku-mrudisha mke wake ambaye hajafa kama munafyo fikiria nyinyi, ndio maana kwenye droo muliyo muweka hamjamkuta”
“Amekwenda wapi?”
Nilimuuliza kwa kujiamini
“Eddy hilo swali nitakujibu baadaye na si mbele ya hawa watu”
“Jamani enendeni kwa amani ya bwana, ila hakikisheni hamuitoi siri hii ya kwamba kuna Eddy wawili.Yoyote atakaye toa siri hii basi atadili na mimi na sio Eddy yule sawa”
Jamaa alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo, na kuwafanya dokta na watu wake kutingisha vichwa kwamba wameelewa, akawaruhusu watoke ndani ya jengo la kuhifadhia maiti, wote wakatoka wakiwa wanakimbia kila mmoja akijaribu kuwahi kufika mlangoni na asiwe wa mwisho.Baada ya dokata na watu wake kutoka, Eddy akanifwata sehemu nilipo simama na kunishika bega
“Niambie ndugu yangu”
“Safi” nilijibu hiyo basi ila kwa mbali woga umenitawala
“Pole sana na matatizo”
“Nimeshapowa ndugu yangu”
Tulizungumza huku tukielekea nje, tayari kulisha anza kupambazuka, tukaanza safari ya kuelekea kwangu huku tukitem-bea kwa miguu cha ajabu njiani watu hawatushangai na mara nyingine baadhi ya watu walinisalimia mimi mwenyewe
“Mbona wewe hawakusalimii?”
“Mimi hawanioni, wakiniona watajikojolea kama yule dokta”
“Umefanya fanyaje hadi hawakuoni?”
“Ni mimi mwenye ndio najua jinsi nilivyo fanya, ila usiwe na shaka utajua tu”
Kwa njia za mkato, tukafika kwangu na moja kwa moja tukaingia ndani, tukakuta baadhi ya watu walio hudhuria kwenye sherehe wakiwa wamejilaza sebleni, wakisubiria kupambazuke waende makwao, wengine wakiwa na shahuku ya kutaka kujua hali ya mke wangu inaendeleeja
“Kaka Eddy shem anaendeleaje?” Jamaa mmoja aliniuliza baada tu ya kukaa kwenye sofa
“Muambie anaendelea vizuri”
“Anaendelea vizuri”
“Pole sana kaka”
“Asante”
Baadhi ya watu wakaanza kunihoji hiji maswali kadha na kila aliye niuliza swali, alijibiwa na Eddy mwenzangu huku wote wakiamini kwamba mimi ndio ninao wajibu maswali yao.Waalikwa wote wakondoka mida ya saa nne asubuhi na tukabaki mimi na Eddy
“Ngoja nifanye usafi wa nyumba”
Eddy alizungumza na kuanza kufanya usafi wa nyumba nzima, kitu kingine kilicho niacha hoi ni jinsi kasi aliyo itumia kui-safisha nyumba yangu, hapo ndipo nikaamini kwamba jamaa sio mtu wa kawaida
“Unashangaa nini?”
“Nashangaa jinsi ulivyo safisha jumba lote hili ndani ya muda mchache!!”
“Usishangae sana”
“Wewe ni nani haswa kwa maana sijakuelewa hadi sasa hivi japo unafanana na mimi?”
Eddy akaanza kucheka kicheko kikali kilicho anza kuyaumiza masikio yangu, alipo gundua ananiumiza masiko yangu akajifumba mdomo na kuandelea kucheka ndani kwa ndani
“Mimi ni Eddy, ila nimetoka sayari nyingine na sio duniani”
“Sayari gani?”
“Marsi, hii ni sayari ambayo inasadikika kwamba watu wanaweza kushi si ndivyo?”
“Sina uhakika”
“Una uhakika gani, wewe si ulikuwa mwalimu wa Sayansi au umesha jisahau?”
“Yaa nilikuwa ni mwalimu ila sio kama nilikuwa ninafwatilia maswala hayo”
“Basi ukweli ni kwamba sayari ya Marsi watu wanaweza kuishi, ila si watu kama nyinyi”
Eddy alizungumza huku akijirusha kwenye sofa na kupandisha miguu yake yenye viatu juu ya meza ya kioo
“Watu wote wanao ishi kule wanauwezo wa ziada, na kama maishani mwako ulishawahi kusikia viumbe vyenye uwezo mkubwa wa akili kupita binadamu wanaitwaje?”
“Ellians”
“Ndio, mimi ni miongoni mwao.Kipindi nipo kwenye matembezi yangu ya kuizunguka dunia kwa bahati nzuri nikakuona wewe, ukiwa unafanana na mimi, isitoshe hadi jina tukawa tunaonana.Usiku nilikuona jinsi unavyo muhangaikia mke wa-ko, ulivyo pambana na wale mabinti ila wale ndio walio muiba mke wako kipenzi”
“Tutampata vipi mke wangu?”
“Mke wako yupo mbali sana na hapa, hayupo chini wala hayupo juu”
“Sijuakuelewa vizuri, hayupo chini wala juu kivipi?”
“Kwa sasa huwezi kunielewa, ila kikubwa ambacho ninataka kukifanya kwako ni kuitoa hiyo pumzi uliyo pandikizwa”
“Ukiitoa si nitakufa?”
“Ndio utakufa, kwani unaogopa kufa”
Sikumuelewa Eddy ana maana gani na kila nilivyo mtazama mwenzangu hakuwa na wasiwasi hata kidogo, gafla akasima-ma na kuanza kunifwata katika sehemu ambayo nimesimama, nikajaribu kurudi nyuma ila akaniwahi kuukamata mkono wangu, gafla nikastukia nikirushushwa na kujibamiza kwenye ngazi na giza kubwa likatawala kwenye macho yangu, na kukaa kimya
***
Mwanga mkali ukaanz akupiga kwenye macho yangu, nikayafumbua macho yangu na kukutaa na sura ya Eddy akinitazama
“Karibu tena kwenye uhai, Eddy”
Nikajaribu kuinuka ila nikashindwa, nikajitazama pembeni na kukuta nikiwa nimefungwa kwenye kitanda, na mikanda migumu sana ambayo sio rahisi kwangu kunyanyuka, akaisogeza taa ambayo inanimulika usoni
“Unajisikiaje?”
“Vizuri”
Nikatizma pembeni na kukuta watu sita wali valia mavazi meupe wakiwa wamesimama, sura zao tofauti kidogo na bina-damu wa kawaida kwani vichwa vyao ni vikubwa kiasi na wanamacho makubwa, ila pia zao ni zakawaida na hata midomo yao ni yakawaida
“Eddy hao ni kina nani?”
“Hao ni madaktari ambao wamekufanyia, huduma ya kukutoa pumzi ya kinyoka na kukuwekea pumzi ya binadamu wa kawaida”
Madaktari hao wakatabasamu, na mimi nikaonyesha tabasamu, Eddy akazungumza nao kwa lugha ambayo sijawahi kuisi-kia hata siku moja kwenye maisha yangu.Wakanisogelea na kuifungua mikanda walio nifunga, Eddy akanipa mkono na ku-nyanyuka na kukaa kitako kitandani
“Pole Eddy”
“Asante”
Nilimjibu kwa sauti iliyo jaa furaha kwani, hali ninayo jihisi ni tofauti na pale nilivyo kuwa awali, macho yangu yakazungu-ka kwenye chumba kizima, ambacho kimejaa mitambo ya ajabu ajabu nisiyo wahi kuiona
“Eddy usishanga sana, hapa upo kwenye jengo la hospitali yetu sisi”
“Ni duniani kweli huku?”
“Hapana ila nitakurudisha duniani, huku ndipo ulipo mji wetu sisi ma elians”
Eddy akaanza kunitembeza kwenye maeneo ya jengo hili la hospitali lililo jengwa kwa vyuma vitupu, watu wake ni waaja-bu sana, kiasi kwamba muda mwengine nilijikuta nikiogopa
“Eddyunatambua kwamba imetuchukua muda wa mwaka mzima hadi wewe kurudi katika hali ya kibinadamu”
“Weee!!”
“Ndio, na haikuwa kazi ndogo kuifanya”
“Eddy asante sana”
“Usijali, ila kuna watu wezangu unatakiwa kwenda kuwapa shukrani”
“Kina nani hao”
“Utawaona”
Tukaingia kwenye moja ya jengo lenye mnara mrefu, tukaingia kwenye moja ya chumba na kukuta suti nyingi nzuri, Eddy akaniomba nichague suti nitakayo ipenda, nikachagua suti nzuri nyeusi, iliyo nipendeza sana.Tukatoka kwenye chumba na kuelekea kwenye majo ya lango kubwa lililopo humu ndani ya hili jengo na kuingia ndani nikashangaa kukutana majitu makubwa yenye misuli iliyo kaza vizuri, japo sura zao ni zakutisha ila inanibidi kuwazoea tuu, tukapita katikati yao na kwenda kusimama mbele ya mtu mmoja aliye kaa kwenye kiti kikubwa cha dhahabu tupu
“Huyu ni mkuu wa jeshi la Ellians wote ulimwenguni na nibaba yangu mzazi”
Eddy alizungumza huku akiinama kwa kusujudia, ikanibidi na mimi kufanya hivyo, mkuu huyo akasimama na kutuamuru sisi kusimama.Akatusogelea na kunipa mkono mimi huku akitabasamu, nikampa mkono wangu na akaanza kuutingisha huku akitabasamu
“Karibu sana bwana Eddy”
“Asante”
“Kuna zawadi yako tumepanga kukupatia”
“Zawadi?”
“Ndio”
Akaniachia mkono wangu, akapiga kofi moja na watu wate wakapiga goti moja na kusujudia, tukabaki tukiwa tumesimama sisi watatu, mlango mmoja mkubwa ulio tengenezwa kwa dhahabu ukafunguliwa, kundi kubwa la wasichana walio valia mavazi meupe wakatoka, na kuanza kutembea mwendo wa taratibu.Wakasimama mbele yangu na wote wakaipiga goti moja chini na akabaki mmoja wao akiwa amesimama na amevalia shele kubwa huku sura yake ikiwa imefunikwa
“Nenda kamfunue”
Eddy alizungumza, nikamtazam Eddy usoni, akaachia tabasamu pana.Nikapita katikati ya wasichana walio inama chi-ni.Nikasimama mbele ya msichana, taratibu nikamfunua kitambaa kilicho ziba sura yake, sikuamini macho yangu baada ya kukuta ni Rahma akiwa amepabwa vizuri sara yake
“Rahma!!”
“Eddy!!”
Tukakumbatiana kwa furaha huku machozi ya furaha yakianza kutumwagika kwenye sura zetu, hatukuona aibu yoyote taratibu tukaanza kunyonyana midomo yetu,
“Mmmm”
Mguno wa baba yake Eddy ukatufanya tuachiane huku sote tukiwa na furaha sana.
“Eddy mke wako tulimuokoa kutoka mikononi mwa mabinti walio kuwa wamemteka, na tulifanikiwa kuwaangamiza ma-binti wote na kwasasa mutaishi kwa amani na furaha kwenye maisha yenu”
“Asante sana baba”
Nilizungumza huku machozi ya furaha yakinimwagika usoni mwangu.Akatuomba tumsogelee sehemu alipo simama, akai-shika mkino yetu kwa pamoja kisha akamnyooshea Eddy mkono, Eddy akatoa visanduku viwili vidogo mfukoni mwake na kumkabithi baba yake, akatupa kila mmoja kisanduku chake na kutuomba tuvifungue.Macho yetu yakakutana na pete za dhahabu ambazo zinag’aa sana
“Munaweza kuvishana pete hizo”
Alizungumza, nikachukua pete iliyopo kwenye kisanduku changu na kumvisha Rahma, kisha Rahma naye akanivisha pete, shangwe na kelele za watu waliopo kwenye ukumbi huu zikatustua sote mimi na Rahma, maua mengi kutoka juu ya dari la jengo hili yakaanza kumwagika katika eneo zima la ukumbi.Machozi ya furaha yakaendelea kumwagika katika nyuso zetu zilizo jaa furaha.
“Nawatangaza rasmi kwamba mumekuwa mke na mume”
Baba Eddy alizungumza na shangwe zikaendelea.Eddy akatuchukua hadi kwenye moja ya kifaa cha kushangaza na kutom-ba tuingine sote wawili
“Jamani, ninawarudisha duniani”
Eddy alizungumza huku akikiwasha kifaa hicho, safari ya kwenda duniani haikuchukua muda sana kutokanana kifaa tuli-cho kipanda kwenda kwa mwendo mkali sana.Akatufikisha hadi kwenye eneo la jumba letu, tukashuka sote watatu na ku-kuta nyumba za taa zikiwa zimewashwa kutokana ni usiku
“Karibuni ndani”
Eddy alitukaribisha ndani, tukaingia hatukuamini kukuta nyumba yetu ikiwa imepabwa vizuri na kuwekwa vitu ambavyo kusema ukweli vimezidi kuipendezesha nyumba yetu
“Eddy na Rahma nninawatakia maisha mema”
Eddy alizungumza huku akiwa ametushika mikono yetu
“Muishi kwa amani na upendo, na watoto mutakao wapata siku moja moja nitakuwa ninakuja kuwatembelea”
“Hata wewe ninashukuru kwa msaada wako wote ulio tupatia”
Eddy akatukumbatia, akatuachia na kutoka nje, akaingia kwenye kifaa chake ambacho si kikubwa sana, na hakina mlio, akatupungia mkono wa kutuaga na kuondoka zake, nikambebe Rahma hadi gorofani kwenye chumba chetu, sote tukabaki tukishangaa baada ya kukuta chumba kikiwa na kitanda kikubwa kilicho tengenezwa kwa madini ya dhahabu huku kwenye ukuta kukiwa na picha yetu kubwa iliyokuwa ikituonyesha jinsi tulivyokuwa tunavishana pete, sakau nzima im-ejaa noti nyingi za dola mimi za kimarekani
“Eddy hii picha imefikaje hapa?”
“Hata mimi sijui”
“Na hizi el..”
Sikumpa ruhusa Rahma kuzungumza chohota, nikawahi kuinyonya midomo yake na sote tukaangukia kitandani na kuanza kuchojoana nguo moja baada ya nyingine, kama kawaida yetu tukaanza kupeana ile kitu roho inapenda huku kila mmoja akiwa na furaha ya utamu wa mwenzake
“Eddy”
“Mmmmm”
“Unajua kuwa mimi ndio nimekufundisha mambo haya”
“Nenda zako huko”
“Kweli”
Rahma alizungumza kwa utani huku akinikalia kiunoni mwangu na kuendelea na kupeana raha zetu.
Bada ya mwezi mmoja Rahma akaanza kuona dalili za ujauzito jambo liliozidi kujenga furaha ya upendo kati yetu, kazi yangu kubwa ikawa ni kumpeleka mke wangu cliniki kila kipindi cha yeye kwenda cliniki kilipo fika.Kipindi cha miezi ya Rahma kujifungua nikawadia, nikamkimbiza hospitalini kujifungua.Madaktari wakaniomba nisubiri nje ya chumba cha ku-jifungulia baada ya muda mlango ukafunguliwa
“Bwana Eddy, hongera sana”
Dokta zalizungumza huku akivua gloves zake mikononi na kujikuta nikiwa ninashauiku ya kutaka kujua ni nini dokta ana-taka kuzungumza
“Mke wako amejifungua salama, na amejifungua watoto mapacha wa kike, wanaafya nzuri na kilo za kutosha tu”
“Kweli dokta”
“Ndio, na mke wako amevunja rekodi ya hospiali yetu kwani haijawahi kutokea mwanake kuzaa watoto mapacha wenye kilo zaidi ya nne”
“Weeee!!! Naweza kumuona mke wangu na wanangu?”
“Ndio unaweza”
Dokta akaniruhusu kuingia ndani ya chumba ambapo nikamkuta Rahma akiwa amewabeba watoto wetu, Rahma alipo nio-na akaachia tabasamu pana huku akitabasamu, akanikabidhi watoto niwabebe, watoto watu wamechukua kila kitu kwetu, nywele zipo kama za mama yao ambaye ni muarabu, huku nyusi na macho yao yakiwa kama yangu.Mke wangu akakaa hospitali kwa kipindi cha wiki mbili tukaruhusiwa kurudi nyumbani, ambapo Rahma akwasiliana na wazazi wake wakaja kutoka Dubai, kila mmoja akafurahia kuona watoto watu ambao kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi walivyo zidi kuwa wazuri na afya nzuri
“Eddy unapendekeza waitwe majina gani?”
Rahma aliniuliza siku kadhaa kabla ya kwenda kuwabatiza
“Kurwa aitwe Xaviela na doto aitwe Xaviena”
“Sawa mume wangu”
Siku ya kuwabatiza watoto wetu ikawadia, sikuamini kuona watu wengi wakiwemo waandishi wa habari wakijumuika nani katika sherehe ya kuwabatiza watoto watu ambao kila mtu, anahamu ya kuwaona wengine wakitamani hata kuwashika jambo lililozidi kuifanya familia yangu kuwa maarufu katika jiji zima la Tanga na Tanzania kwa ujumla
“Mume wangu kweli TANGA RAHA”
Rahma alizungumza huku akiwa amembeba Xaviena
“Kwa nini?’
“Tazama watu walivyo kusanyika kwa kutuunga mkono sisi”
“Yaa wanupendo na sisi na watoto wetu”
Nilizungumza kwa furaha huku nikimrusha rusha Xaviela ambaye muda wote anatabasamua usoni mwake
“Nakupenda sana baba Xavina”
“Hata mimi pia ninakupenda sana mama Xaviela”
Nikampiga busu la mdomoni mke wangu kama ishara ya upendo kati yetu, jambo lilio fanya watu wengi kupiga makofi hu-ku wakishangilia kwa furaha.

MWISHO

Chapisha Maoni

0 Maoni