
MWANAUME UKIKOSA MAARIFA LAZIMA MWANAMKE AKUTAWALE:
Mwanaume Huna Kazi, Huna Pesa, Huna muelekeo wowote wa maisha, Huna Nguvu ya kutongoza kwakua huna nyuma wala mbele.
Ukibahatika kupata mwanamke mwenye pesa, ukaoana nae, Lazima akutawale maana huna sauti juu ya chochote.
Mwanaume Huna msimamo, Huna maamuzi yenye tija, Huna akili ya kupambana, Huna mbinu za maendeleo, Huna mawazo yoyote ya kimaisha. Ukimpata mwanamke mwenye vyote hvyo lazima akutawale broo
Mwanaume Huna hekima, Huna busara, Hujui wajibu wako, Huwezi kuwa na tamko, Huwez kujiendesha, Akili yako imefika mwisho wa kuwaza.
Ukimpata mwanamke lazima akuendeshe
Mwanaume kuwa mtumwa wa kihisia, unapenda penda hovyo, hujui kucontrol upendo wako, mkeo hajui thamani ya upendo wako, Mke anakukalia kichwani.
Unaishi mjini kutengeneza Six Parks, Unaishi kweny ghetto za wenzio, kutembelea magari ya masela zako, maisha ya kuiga yasiyo na faida, Unasubiri upate mke wa kitajiri ukimuoa akulee, akutunze kwa utajiri wake. Utakuwa house boy broo.
Ebu jitume, tafuta kazi, pambana upate pesa, ukioa umeoa kweli sio unaoa mwanamke alafu mkifika ndani yeye ndio amekuoa.
Onyesha wew ni mwanaume, kuwa na msimamo wa maisha, weka misingi yako na mikakati ya kuendesha maisha yako, Hizo ndio nguvu halisi za kiume.
Kuwa mwenye hekima, Kuwa na maamuzi yenye tija, kuwa na kauli za kimsingi, Uwe mwenye uwezo wa kujiongoza na kuongoza wengine kama kichwa, Onyesha kuwa wew ni mwanaume kila mtu na atambue hilo.
Upendo wako uwe wenye msimamo, mambo ya kudanga danga yatakumalizia pesa, yatamiliki akili yako na maarifa ya kufanya maendeleo hutakuwa nayo. Elekeza hisia zako kwa mtu mmoja ambaye unaona ndie sahihi amebeba upendo wa moyo wako na sio matamanio, nawe hutadharaulika
Na tabia ya kuazima nguo kwa rfk zenu pia muache utadhalaulika pia mwaga jasho mwanaume usimame kama mwanaume haswa
JIULIZE PUNGUFU LAKO HAPA NI LIPI?
BADILIKA
0 Maoni