1. Digrii ya daraja la kwanza haitakufanya kuwa mke wa daraja la kwanza, bali utii na heshima ndivyo vinavyoweza kukupa hadhi hiyo.
2. Mwanamke anayemheshimu mumewe ndiye mke bora anayetamaniwa na kila mume.
3. Tabia na mwenendo wako vinaweza kumfanya mumeo ajivunie kuwa na wewe au ajutie kwa nini alikuoa.
4. Ili kuwa mke maridhawa, unahitaji zaidi kuwa na ufundi wa kudhibiti hasira kuliko kuwa fundi wa usumbufu na uropokaji.
5. Tofautisha kati ya maisha ya kazini na nyumbani. Kazini jitahidi kuwa kiongozi, lakini nyumbani jitahidi kuwa MKE.
6. Usishindane na mumeo, bali mpe hamasa na kumtia moyo. Mpambe na kumsifu.
7. Nguvu yako inapatikana katika unyenyekevu na utii wako, sio katika dharau na kiburi.
8. Usimuadhibu muneo kwa kumnyima chakula au tendo la ndoa, hilo linaweza kumsukuma kuvitafuta nje.
9. Hakuna ubaya kukubali kuwa umekosea pindi unapokosea.
10. Jiandae kumsamehe mumeo akikukosea. Mke msamehevu ni mbora kuliko mke mwenye visasi.
11. Amua kuwa mke mwema, hilo utalihitajia sana katika safari yako.
12. Jipambe kwa kuwa mke mbembezi.

0 Maoni