Kuna tofauti kati ya kuwa mwana-ndoa na kuwa mume au mke. Unaweza ukawa mke lakini usiwe mwana-ndoa. Unaweza ukawa mume, lakini usiwe mwana-ndoa. Kuwa mwana-ndoa ni zaidi ya kuwa mke au mume.
Hata katika ulingo wa siasa kuna parliamentarian (mwana-bunge) na member of parliament (mjumbe wa bunge/mbunge).
Bibi mmoja wakati akiadhimisha miaka 60 ya ndoa yake aliulizwa:
"Umewezaje kuishi miaka yote katika ndoa yako hii?"
Akajibu:
"Kwa sababu nilizaliwa katika kizazi ambacho kitu kinapokorofika hatukitupi, bali tunakirekebisha na kuendelea kukitumia".
Naam, bibi huyo anatuonesha kuwa licha ya suhula zote za kimaada (material facilities) lakini hatujui kurekebisha vitu vyetu vinapokorofika. Hatujui NJIA bora za kushughulikia mambo. Tuna majibu mepesi kwenye mambo makubwa ya mahusiano yetu.
Linapotokea TATIZO, mwanandoa anapambana na tatizo. Lakini mke/mume anapambana na MTU.
Linapotokea tatizo, mwana-ndoa huwa kama daktari. Hapambani na MGONJWA, bali hupambana na UGONJWA.
Kuwa MWANANDOA ni zaidi ya kuwa MKE au MUME.

0 Maoni